< 撒母耳記下 8 >
1 此後,大衛攻打非利士人,把他們治服,從他們手下奪取了京城的權柄;
ikawa baada ya haya Daudi aliwashambulia Wafilisti na kuwashinda. Hivyo Daudi akaichukua Gathi na vijiji vyake kutoka katika mamlaka ya wafilisti.
2 又攻打摩押人,使他們躺臥在地上,用繩量一量:量二繩的殺了,量一繩的存留。摩押人就歸服大衛,給他進貢。
Kisha akaishinda Moabu na akawapima watu wake kwa mstari kwa kuwafanya walale chini juu ya ardhi. Alipima mistari miwili ya kuua, na mstari mmoja kamili kuwahifadhi hai. Hivyo Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakaanza kumlipa kodi.
3 瑣巴王利合的兒子哈大底謝往大河去,要奪回他的國權。大衛就攻打他,
Kisha Daudi akamshinda Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, Hadadezeri aliposafiri kuurudisha ufalme wake katika mto Frati.
4 擒拿了他的馬兵一千七百,步兵二萬,將拉戰車的馬砍斷蹄筋,但留下一百輛車的馬。
Daudi aliteka magari 1, 700 ya farasi na askari ishirini elfu waendao kwa miguu. Daudi akawakata miguu farasi wa magari, lakini akahifadhi wakutosha magari mia moja.
5 大馬士革的亞蘭人來幫助瑣巴王哈大底謝,大衛就殺了亞蘭人二萬二千。
Wakati Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadeziri mfalme wa Soba, Daudi akaua katika Washami watu ishirini na mbili elfu.
6 於是大衛在大馬士革的亞蘭地設立防營,亞蘭人就歸服他,給他進貢。大衛無論往哪裏去,耶和華都使他得勝。
Daudi akaweka ngome huko Shamu ya Dameski, na Washami wakawa watumishi wake na wakaleta kodi. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alikokwenda.
7 他奪了哈大底謝臣僕所拿的金盾牌,帶到耶路撒冷。
Daudi akachukua ngao za dhahabu walizokuwa nazo watumishi wa Hadadezeri naye akazileta Yerusalemu.
8 大衛王又從屬哈大底謝的比他和比羅他城中奪取了許多的銅。
Mfalme Daudi akachukua shaba nyingi kutoka Beta na Berosai, miji ya Hadadezeri.
Wakati Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri,
10 就打發他兒子約蘭去見大衛王,問他的安,為他祝福,因為他殺敗了哈大底謝(原來陀以與哈大底謝常常爭戰)。約蘭帶了金銀銅的器皿來,
Tou akamtuma Hadoramu mwanawe kwa mfalme Daudi kumpa salamu na kumbariki, kwa kuwa Daudi alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda, maana Hadadezeri alikuwa amepiga vita dhidi ya Tou. Hadoramu akaja pamoja na vitu vya fedha, dhahabu, na shaba.
11 大衛王將這些器皿和他治服各國所得來的金銀都分別為聖,獻給耶和華,
Mfalme Daudi akaviweka wakfu vitu hivi kwa ajili ya Yahwe, pamoja na fedha na dhahabu kutoka katika mataifa yote aliyokuwa ameyashinda-
12 就是從亞蘭、摩押、亞捫、非利士、亞瑪力人所得來的,以及從瑣巴王利合的兒子哈大底謝所掠之物。
kutoka Shamu, Moabu, Waamoni, Wafilist, Waamaleki, pamoja na nyara zote alizoziteka kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.
13 大衛在鹽谷擊殺了亞蘭一萬八千人回來,就得了大名;
Jina la Daudi likajulikana sana alipowashinda washami katika bonde la Chumvi, pamoja na watu wao wapatao elfu kumi na nane.
14 又在以東全地設立防營,以東人就都歸服大衛。大衛無論往哪裏去,耶和華都使他得勝。
Akaweka ngome katika Edomu yote, na Waedomu wote wakawa watumishi wake. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.
Daudi akatawala juu ya Israeli yote, naye akatenda kwa haki na usawa kwa watu wote.
16 洗魯雅的兒子約押作元帥;亞希律的兒子約沙法作史官;
Yoabu mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mwenye kuandika taarifa.
17 亞希突的兒子撒督和亞比亞他的兒子亞希米勒作祭司長;西萊雅作書記;
Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Seraya alikuwa mwandishi.
18 耶何耶大的兒子比拿雅統轄基利提人和比利提人。大衛的眾子都作領袖。
Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa washauri wa mfalme.