< 列王紀下 25 >
1 西底家背叛巴比倫王。他作王第九年十月初十日,巴比倫王尼布甲尼撒率領全軍來攻擊耶路撒冷,對城安營,四圍築壘攻城。
Ilitokea kwamba katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedekia, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya huo mwezi, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote kwa ajili ya kupigana dhidi ya Yerusalemu. Akaweka kambi kuelekeana nayo, na wakajenga ukuta kuizunguka.
Hivyo mji huo ulizungukwa mpaka miaka kumi na moja ya utawala wa Sedekia.
3 四月初九日,城裏有大饑荒,甚至百姓都沒有糧食。
Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa huo mwaka, njaa ilikuwa kali sana kwenye huo mji kwamba hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu wa nchi.
4 城被攻破,一切兵丁就在夜間從靠近王園兩城中間的門逃跑。迦勒底人正在四圍攻城,王就向亞拉巴逃走。
Wakati huo ule mji ulikuwa umebomoka ndani, na wapiganaji wote wakakimbia usiku kwa njia ya lango kati ya kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wote wameuzunguka mji. Mfalme akaenda kuelekea upande wa Araba.
5 迦勒底的軍隊追趕王,在耶利哥的平原追上他;他的全軍都離開他四散了。
Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuata mfalme Sedekia na kumchukua katika tambarare ya bonde la Mto Yoradani karibu na Yeriko. Jeshi lake lote lilitawanyika wakamwacha.
6 迦勒底人就拿住王,帶他到在利比拉的巴比倫王那裏審判他。
Wakamkamata mfalme na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, ambapo walipitisha hukumu juu yake.
7 在西底家眼前殺了他的眾子,並且剜了西底家的眼睛,用銅鍊鎖着他,帶到巴比倫去。
Kama kwa watoto wa Sedekia, wakawachinja mbele ya macho yake. Kisha akamtoa macho Sedekia, wakamfunga pingu, na kumpeleka hadi Babeli.
8 巴比倫王尼布甲尼撒十九年五月初七日,巴比倫王的臣僕、護衛長尼布撒拉旦來到耶路撒冷,
Basi katika mwezi wa tano, katika siku ya saba ya mwezi, ambapo ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, mtumishi wa mfalme wa Babeli na amrijeshi wa walinzi wake, wakaja hadi Yerusalemu.
9 用火焚燒耶和華的殿和王宮,又焚燒耶路撒冷的房屋,就是各大戶家的房屋。
Akaichoma moto nyumba ya Yahwe, nyumba ya mfalme, na nyumba zote za Yeruselemu; pia kila jengo la muhimu katika mji akayachoma.
10 跟從護衛長迦勒底的全軍就拆毀耶路撒冷四圍的城牆。
Kama kwa kuta zote zilizoizunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli ambao walikuwa chini ya amrishi wa walinzi wakaziharibu.
11 那時護衛長尼布撒拉旦將城裏所剩下的百姓,並已經投降巴比倫王的人,以及大眾所剩下的人,都擄去了。
Basi watu waliokuwa wamebaki ambao walikuwa wameondoka katika mji, wale waliokuwa wameasi kwa mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu-Nebuzadani, amiri jeshi wa mlinzi, wakachukuliwa kwenda utumwani.
12 但護衛長留下些民中最窮的,使他們修理葡萄園,耕種田地。
Lakini amiri jeshi wa mlinzi aliwaacha baadhi ya maskini wa nchi ili wafanye kazi kwenye shamba la mizabibu na kulima.
13 耶和華殿的銅柱,並耶和華殿的盆座和銅海,迦勒底人都打碎了,將那銅運到巴比倫去了,
Na zile nguzo za shaba ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, na misimamio na bahari ya chuma ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakazivunja vipande vipande na kubeba shaba kuirudisha Babeli.
14 又帶去鍋、鏟子、蠟剪、調羹,並所用的一切銅器,
Masufuria, mabeleshi, makasi, vijiko, na vyombo vyote vya shaba ambavyo kuhani alivyokuwa amevitunza kwenye hekalu-Wakaldayo wakavichukua vyote.
Masufuria ya kuhamisha majivu na mabakuli ambayo yalikuwa yametengenezwa kwa dhahabu, na yale yaliyotengenezwa kwa fedha-yule nahodha wa mlinzi wa mfalme akavichukua pia.
16 所羅門為耶和華殿所造的兩根銅柱、一個銅海,和幾個盆座,這一切的銅,多得無法可稱。
Zile nguzo mbili, ile bahari, na vile vitako ambavyo Suleimani alivitengeneza kwa ajili ya nyumba ya Yahwe shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.
17 這一根柱子高十八肘,柱上有銅頂,高三肘;銅頂的周圍有網子和石榴,都是銅的。那一根柱子,照此一樣,也有網子。
Urefu wa ile nguzo ya kwanza ulikuwa ridhaa kumi na nane, na kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Na urefu wa kichwa ulikuwa ridhaa tatu, pamoja na mapambo ya wavu na makomamanga yote yakizunguka kwenye hicho kichwa, vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa shaba. Na ile nguzo nyingine ilikuwa vivyo hivyo kama ile ya kwanza pamoja na wavu wake.
18 護衛長拿住大祭司西萊雅、副祭司西番亞,和三個把門的,
Yule amiri jeshi wa mlinzi akamchukua Seraya kuhani mkuu, pamoja za Sefania, yule kuhani wa pili, na walinzi watatu wa kwenye lango.
19 又從城中拿住一個管理兵丁的官,並在城裏所遇常見王面的五個人和檢點國民軍長的書記,以及城裏遇見的國民六十個人。
Kutoka mjini akamchukua mlinzi, afisa mmoja ambaye aliyekuwa msimamizi wa maaskari, na watu watano ambao walikuwa wakimshauri mfalme, ambao walikuwa bado katika mji. Pia alimchukua mfungwa wa afisa jeshi la mfalme, kwa ajili ya kuandika watu kwenye jeshi, pamoja na watu sitini muhimu kutoka hiyo nchi ambao walikuwa katika mji.
20 護衛長尼布撒拉旦將這些人帶到在利比拉的巴比倫王那裏。
Kisha Nebuzaradani, amiri wa mlinzi, akawachukua na kuwapeleka kwa mfalme Babeli huko Ribla.
21 巴比倫王就把他們擊殺在哈馬地的利比拉。這樣,猶大人被擄去離開本地。
Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaiacha nchi yake kwenda utumwani.
22 至於猶大國剩下的民,就是巴比倫王尼布甲尼撒所剩下的,巴比倫王立了沙番的孫子、亞希甘的兒子基大利作他們的省長。
Na wale watu waliokuwa wamebakia katika nchi ya Yuda, wale ambao Nebukadreza mfalme wa Babeli aliwaacha, akamuweka Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, msimamizi wao.
23 眾軍長和屬他們的人聽見巴比倫王立了基大利作省長,於是軍長尼探雅的兒子以實瑪利、加利亞的兒子約哈難、尼陀法人單戶蔑的兒子西萊雅、瑪迦人的兒子雅撒尼亞,和屬他們的人都到米斯巴見基大利。
Kisha wakati maamiri wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemfanya Gedalia kuwa liwali, wakaenda kwa Gedalia huko Mispa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka-wao na watu wao.
24 基大利向他們和屬他們的人起誓說:「你們不必懼怕迦勒底臣僕,只管住在這地服事巴比倫王,就可以得福。」
Gedalia akafanya kiapo kwa watu wake na kuwaambia, “Msiwaogope Wakaldayo. Muishi katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vema kwenu.”
25 七月間,宗室以利沙瑪的孫子、尼探雅的兒子以實瑪利帶着十個人來,殺了基大利和同他在米斯巴的猶大人與迦勒底人。
Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, kutoka familia ya kifalme, wakaja na watu kumi na kumshambulia Gedalia. Gedalia akafa, pamoja na watu wa Yuda na Wababeli ambao walikuwa pamoja nae huko Mizpa.
26 於是眾民,無論大小,連眾軍長;因為懼怕迦勒底人,都起身往埃及去了。
Kisha wale watu wote, kutoka chini kwenda juu, na maamiri wa jeshi, wakainuka na kwenda Misri, kwasababu walikuwa wanawaogopa Wababeli.
27 猶大王約雅斤被擄後三十七年,巴比倫王以未‧米羅達元年十二月二十七日,使猶大王約雅斤抬頭,提他出監;
Ilitokea baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa utumwa wa Yekonia mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki mfalme wa Babeli akamtoa Yekonia mfalme wa Yuda kutoka gerezani. Hii ilitokea katika mwaka ambao Evil-Merodaki alipoanza kutawala.
28 又對他說恩言,使他的位高過與他一同在巴比倫眾王的位,
Akaongea naye kwa ukarimu na kumpatia kiti kizuri zaidi kuliko kile cha wafalme wengine ambao walikuwa pamoja naye Babeli.
Evil-Merodaki akamvua Yekonia nguo za gerezani,
30 王賜他所需用的食物,日日賜他一分,終身都是這樣。
na Yekinia akala siku zote kwenye meza ya mfalme katika maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia.