< 列王紀下 14 >

1 以色列王約哈斯的兒子約阿施第二年,猶大王約阿施的兒子亞瑪謝登基。
Katika mwaka wa pili wa Yehoashi mwana wa Yehoazi, mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.
2 他登基的時候年二十五歲,在耶路撒冷作王二十九年。他母親名叫約耶但,是耶路撒冷人。
Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tanao wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu.
3 亞瑪謝行耶和華眼中看為正的事,但不如他祖大衛,乃效法他父約阿施一切所行的;
Mama yake alikuwa anaitwa Yehoyadani, wa Yerusalemu. Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa macho ya Yahwe, sio kama baba yake Daudi. Alifanya kila kitu ambacho Yoashi, baba yake, alichukuwa amekifanya.
4 只是邱壇還沒有廢去,百姓仍在那裏獻祭燒香。
Lakini sehemu ya juu haikuondolewa. Watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza ubani katika sehemu mahala pa juu.
5 國一堅定,就把殺他父王的臣僕殺了,
Ikawa mara utawala wake ulipokuwa imara, aliwaua watumishi ambao waliokuwa wamemuua baba yake, mfalme.
6 卻沒有治死殺王之人的兒子,是照摩西律法書上耶和華所吩咐的說:「不可因子殺父,也不可因父殺子,各人要為本身的罪而死。」
Ila hakuwaweka watoto wa wale wauaji kwenye kifo; isipokuwa, alifanya kutokana na kile kilichokuwa kimeandikwa kwenye sheria, kwenye kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamuru, akisema, “Wababa wasife kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasife kwa ajili ya makosa ya wazazi wao. Isipokuwa, kila mtu atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
7 亞瑪謝在鹽谷殺了以東人一萬,又攻取了西拉,改名叫約帖,直到今日。
Aliua maaskari elfu kumi wa Edomi kwenye bonde la chumvi; pia alimchukua Sela kwenye vita na kuiita Yoktheeli, ndivyo paitwavyo hadi leo.
8 那時,亞瑪謝差遣使者去見耶戶的孫子約哈斯的兒子以色列王約阿施,說:「你來,我們二人相見於戰場。」
Kisha Amazia akatuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akisema, “Njoo, tuonane kila mmoja macho kwa macho kwenye mashinadano.”
9 以色列王約阿施差遣使者去見猶大王亞瑪謝,說:「黎巴嫩的蒺藜差遣使者去見黎巴嫩的香柏樹,說:將你的女兒給我兒子為妻。後來黎巴嫩有一個野獸經過,把蒺藜踐踏了。
Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akawatuma wajumbe kurudi kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma kwa mwerezi katika Lebanuni, kusema, 'Mpatie mwanangu binti yako amuoe; lakini hayawani aliyekuwako Lebanoni akaukanyaga chini ule mbaruti.
10 你打敗了以東人就心高氣傲,你以此為榮耀,在家裏安居就罷了,為何要惹禍,使自己和猶大國一同敗亡呢?」
Umempiga sana Edomu, na moyo wako umekuinua. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani, kwa nini unataka kujisababishia mataizo na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?”
11 亞瑪謝卻不肯聽這話。於是以色列王約阿施上來,在猶大的伯‧示麥與猶大王亞瑪謝相見於戰場。
Lakini Amazia hakutaka kusikia. Hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakutana uso kwa uso huko Beth Shemeshi, ambayo ilikuwa ya Yuda.
12 猶大人敗在以色列人面前,各自逃回家裏去了。
Yuda walishindwa mbele ya Israeli, na kila mtu akakimbia nyumbani.
13 以色列王約阿施在伯‧示麥擒住亞哈謝的孫子、約阿施的兒子猶大王亞瑪謝,就來到耶路撒冷,拆毀耶路撒冷的城牆,從以法蓮門直到角門共四百肘,
Yehoashi mfalme wa Israeli, akamchukua Amazia, mfalme wa Yuda mwana wa Yehoashi mwana wa Ahazia, huko Beth Shemeshi. Akaja Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kutoka lango la Efraimu mpaka kwenye pembe ya lango, urefu wa mbali wa dhiraa mia nne.
14 又將耶和華殿裏與王宮府庫裏所有的金銀和器皿都拿了去,並帶人去為質,就回撒馬利亞去了。
Akachukua dhahabu na fedha zote, na vitu vyote ambavyo vilipatikana katika nyumba ya Yahwe, na vitu vya thamani kwenye nyumba ya mfalme, pamoja na mateka pia, na kurudi samaria.
15 約阿施其餘所行的事和他的勇力,並與猶大王亞瑪謝爭戰的事,都寫在以色列諸王記上。
Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoashi, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, na jinsi alivyopigana na Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Israeli?
16 約阿施與他列祖同睡,葬在撒馬利亞,以色列諸王的墳地裏。他兒子耶羅波安接續他作王。
Kisha Yehoashi akalala na wazee wake na ailizikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli, na Yeroboamu, mwanaye, akawa mfalme katika eneo lake.
17 以色列王約哈斯的兒子約阿施死後,猶大王約阿施的兒子亞瑪謝又活了十五年。
Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, akaishi miaka kumi na tano baada ya Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.
18 亞瑪謝其餘的事都寫在猶大列王記上。
Kama ilivyo kwa mambo mengine yanayomhusu Amazia, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?
19 耶路撒冷有人背叛亞瑪謝,他就逃到拉吉;叛黨卻打發人到拉吉將他殺了。
Wakafanya njama dhidi ya Amazia katika Yerusalimu, akakimbilia Lakishi. Akakimbia hadi Lakishi, lakini wakawatuma watu kumfuata hadi Lakishi na kumuua huko.
20 人就用馬將他的屍首馱到耶路撒冷,葬在大衛城他列祖的墳地裏。
Wakamrudisha kwa farasi, na alizikwa pamoja na wazee wake katika mji wa Saudi.
21 猶大眾民立亞瑪謝的兒子亞撒利雅接續他父作王,那時他年十六歲。
Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzaria, ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na minne, na walimfanya kuwa mfalme katika nyumba ya kifalme wa baba yake Uzaria.
22 亞瑪謝與他列祖同睡之後,亞撒利雅收回以拉他仍歸猶大,又重新修理。
Alikuwa Uzaria ambaye alijenga Elathi na kuirudisha kwa Yuda, baada ya mfalme Uzaria akalala pamoja na mababu zake.
23 猶大王約阿施的兒子亞瑪謝十五年,以色列王約阿施的兒子耶羅波安在撒馬利亞登基,作王四十一年。
Katika mwaka wa kumi na tano wa Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka arobaini na moja.
24 他行耶和華眼中看為惡的事,不離開尼八的兒子耶羅波安使以色列人陷在罪裏的一切罪。
Akafanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi zake za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye aliisababisha Israeli kuasi.
25 他收回以色列邊界之地,從哈馬口直到亞拉巴海,正如耶和華-以色列的上帝藉他僕人迦特希弗人亞米太的兒子先知約拿所說的。
Akairudisha mipaka ya Israeli kutoka Lebo Hamathi mpaka kwenye Bahari ya Araba, kufuata amri ya neno la Yahwe, Mungu wa Israeli, ambalo aliongea kupitia mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, yule nabii, ambaye alitokea Gathi Heferi.
26 因為耶和華看見以色列人甚是艱苦,無論困住的、自由的都沒有了,也無人幫助以色列人。
Kwa kuwa Yahwe aliyaona mateso ya Israeli, ambayo yalikuwa makali kwa kila mmoja, wote mtumwa na asyemtumwa, na kwamba hapakuwa na ulinzi kwa ajili ya Israeli.
27 耶和華並沒有說要將以色列的名從天下塗抹,乃藉約阿施的兒子耶羅波安拯救他們。
Basi Yahwe akasema kwamba hatoweza kulifuta jina la Israeli chini ya mbingu; badala yake, aliwaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.
28 耶羅波安其餘的事,凡他所行的和他的勇力,他怎樣爭戰,怎樣收回大馬士革和先前屬猶大的哈馬歸以色列,都寫在以色列諸王記上。
Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yeroboamu, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, jinsi alivyo pigana vita na kuipata tena Damaskasi na Hamathi, ambayo ilikuwa ya Yuda, kwa Israeli, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
29 耶羅波安與他列祖以色列諸王同睡。他兒子撒迦利雅接續他作王。
Yeroboamu akalala na mababu zake, pamoja na mfalme wa Israeli, na Zekaria mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.

< 列王紀下 14 >