< 列王紀下 12 >
1 耶戶第七年,約阿施登基,在耶路撒冷作王四十年。他母親名叫西比亞,是別是巴人。
Katika mwaka wa saba wa Yehu, utawala wa Yoashi ulianza; alitawala kwa mda wa miaka arobaini huko Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Sibia, wa Beersheba.
2 約阿施在祭司耶何耶大教訓他的時候,就行耶和華眼中看為正的事;
Yoashi akafanya yaliyo mema usoni mwa Yahwe siku zote, kwa sababu Yehoyada kuhani alimfundisha.
Lakini sehemu ya juu haikuchukuliwa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kuchoma ubani kwenye sehemu za juu.
4 約阿施對眾祭司說:「凡奉到耶和華殿分別為聖之物所值通用的銀子,或各人當納的身價,或樂意奉到耶和華殿的銀子,
Yoashi akamwambia kuhani, “Pesa zote zilizokuja kama sadaka takatifu kwenye nyumba ya Yahwe, pesa ya matumizi pesa ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na pesa yote aonayo moyoni mwake kuileta kwenye nyumba ya Yahwe-
5 你們當從所認識的人收了來,修理殿的一切破壞之處。」
makuhani watapokea pesa kutoka miongoni mwa mmoja wa watunza pesa na kutengeneza kila sehemu itakayoonekana imeharibika kwenye hekalu.”
6 無奈到了約阿施王二十三年,祭司仍未修理殿的破壞之處。
Lakini kama mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani hawakuwa wameandaa kitu chochote kwenye hekalu.
7 所以約阿施王召了大祭司耶何耶大和眾祭司來,對他們說:「你們怎麼不修理殿的破壞之處呢?從今以後,你們不要從所認識的人再收銀子,要將所收的交出來,修理殿的破壞之處。」
Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na kuhani mwingine; akawaambia, “Kwa nini hamjaandaa kitu chochote kwenye hekalu? Sasa msichukue tena pesa kutoka kwa walipa kodi wenu, lakini chukueni kile kilichokuwa kikikusanywa kwa ajili ya matengenezo ya hekalu na uwapatia wale wanaoweza kufanya matengenezo.
8 眾祭司答應不再收百姓的銀子,也不修理殿的破壞之處。
Hivyo makuhani wakakubaliana wasichukue pesa tena kutoka kwa watu na wasitengeneze wenyewe.
9 祭司耶何耶大取了一個櫃子,在櫃蓋上鑽了一個窟窿,放於壇旁,在進耶和華殿的右邊;守門的祭司將奉到耶和華殿的一切銀子投在櫃裏。
Badala yake, Yehoyada yule kuhani akachukua kasha, akatoboa tundu kwenye kifuniko chake, na kuliweka karibu na madhabahu, upande wa kulia kama mtu anaingia kwenye madhabahu ya Yahwe. Makuhani ambao walikuwa wakilinda mlango wa hekalu wakatumbukiza pesa zote ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe.
10 他們見櫃裏的銀子多了,便叫王的書記和大祭司上來,將耶和華殿裏的銀子數算包起來。
Ikawa walipoona kwamba kulikuwa na pesa za kutosha kwenye kasha, mwadishi wa mfalme na kuhani mkuu wakaja na kuweka pesa kwenye mifuko na kisha kuhesabu, pesa ikaonekana kwenye nyumba ya Yahwe.
11 把所平的銀子交給督工的,就是耶和華殿裏辦事的人;他們把銀子轉交修理耶和華殿的木匠和工人,
Wakawapa pesa ambayo ilikuwa imepimwa kwenye mikono ya watu ambao waliokuwa wanatunza nyumba ya Yahwe. Wakawalipa mafundi seremala na wajenzi ambao walikuwa wemefanya kazi kwenye nyumba ya Yahwe,
12 並瓦匠、石匠,又買木料和鑿成的石頭,修理耶和華殿的破壞之處,以及修理殿的各樣使用。
na waashi na wakata mawe, kwa ajili ya kununua mbao na kukata mawe kwa ajili ya kutengenezea nyumba ya Yahwe, na yote iliyokuwa inahitajika kulipwa kwa ajili ya kuitengeneza.
13 但那奉到耶和華殿的銀子,沒有用以做耶和華殿裏的銀杯、蠟剪、碗、號,和別樣的金銀器皿,
Lakini ile pesa iliyokuwa imeletwa kwenye nyumba ya Yahwe haikulipwa kwa ajili ya vikombe vya fedha, mabeseni, au dhahabu au fedha yoyote ya vyombo.
Waliwapa hizi fedha wale ambao waliokuwa wamefanya kazi ya kutengeneza nyumba ya Yahwe.
15 且將銀子交給辦事的人轉交做工的人,不與他們算賬,因為他們辦事誠實。
Pia, hakukuhitajika zile pesa zilipwe kwa ajili ya matengenezo ili kuwajibika kwa kuwa watu walizipokea nakuzilipa kwa watenda kazi, kwa sababu hawa watu walikuwa waadilifu.
16 惟有贖愆祭、贖罪祭的銀子沒有奉到耶和華的殿,都歸祭司。
Lakini pesa kwa ajili ya matoleo ya hatia na pesa kwa ajili ya matoleo ya dhambi hazikuwa zimeletwa kwenye hekalu la Yahwe, kwa sababu zilikuwa mali ya makuhani.
17 那時,亞蘭王哈薛上來攻打迦特,攻取了,就定意上來攻打耶路撒冷。
Kisha Hazaeli mfalme wa Shamu akashambuliwa na kupigana dhidi ya Gathi, na kuichukua.
18 猶大王約阿施將他列祖猶大王約沙法、約蘭、亞哈謝所分別為聖的物和自己所分別為聖的物,並耶和華殿與王宮府庫裏所有的金子都送給亞蘭王哈薛;哈薛就不上耶路撒冷來了。
Ndipo Hazaeli akageuka kuishambulia Yerusalemu. Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vitu vyote ambavyo Yehoshefati na Yehoramu na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, na kuviweka wakfu, na vile alivyokuwa ameviweka wakfu, na dhahabu zote zilizokuwa zimeonekana kwenye gala la nyumba ya Yahwe na la mfalme akawatuma kwenda kwa Ahazi mfalme wa Shamu. Kisha Hazaeli akaenda zake kutoka Yerusamu.
19 約阿施其餘的事,凡他所行的都寫在猶大列王記上。
Kama mambo mengine yanayomuhusu Yoashi, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
20 約阿施的臣僕起來背叛,在下悉拉的米羅宮那裏將他殺了。
Watumishi wake wakainuka na kupanga pamoja; wakamteka Yoashi katika Bethi Milo, kwenye njia ya kushukia kwa Sila.
21 殺他的那臣僕就是示米押的兒子約撒甲和朔默的兒子約薩拔。眾人將他葬在大衛城他列祖的墳地裏。他兒子亞瑪謝接續他作王。
Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakamshambulia na akafa. Wakamzika Yoashi pamoja na mababu zake katika mji wa Daudi, na Amazia, mtoto wake, akawa mfalme kwenye sehemu yake.