< 哥林多後書 5 >
1 我們原知道,我們這地上的帳棚若拆毀了,必得上帝所造,不是人手所造,在天上永存的房屋。 (aiōnios )
Tunajua kwamba kama maskani ya ulimwenguni ambayo tunaishi humo yanaharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu. Ni nyumba isiyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, bali ni nyumba ya milele, katika mbingu. (aiōnios )
2 我們在這帳棚裏歎息,深想得那從天上來的房屋,好像穿上衣服;
Kwa kuwa katika hema hii tunaugua, tukitamani kuvikwa kwa maskani yetu mbinguni.
Tunatamani kwa ajili ya hii kwa sababu kwa kuivaa hatutaonekana kuwa tu uchi.
4 我們在這帳棚裏歎息勞苦,並非願意脫下這個,乃是願意穿上那個,好叫這必死的被生命吞滅了。
Kwa hakika wakati tuko ndani ya hema hii, twaugua tukilemewa. Hatutaki kuvuliwa. Badala yake, tunataka kuvalishwa, ili kwamba kile kilicho kufa kiweze kumezwa na uzima.
5 為此,培植我們的就是上帝,他又賜給我們聖靈作憑據。
Yule aliyetuandaa sisi kwa kitu hiki ni Mungu, ambaye alitupa sisi Roho kama ahadi ya kile kitakacho kuja.
6 所以,我們時常坦然無懼,並且曉得我們住在身內,便與主相離。
Kwa hiyo muwe na ujasiri siku zote. Muwe macho kwamba wakati tuko nyumbani katika mwili, tuko mbali na Bwana.
Kwa kuwa tunatembea kwa imani, sio kwa kuona. Kwa hiyo tunaujasiri.
Ni bora tuwe mbali kutoka kwenye mwili na nyumbani pamoja na Bwana.
9 所以,無論是住在身內,離開身外,我們立了志向,要得主的喜悅。
Kwa hiyo tunaifanya kuwa lengo letu, kama tukiwa nyumbani au mbali, tumpendeze yeye.
10 因為我們眾人必要在基督臺前顯露出來,叫各人按着本身所行的,或善或惡受報。
Kwa kuwa lazima wote tuonekane mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kwamba kila mmoja aweze kupokea kile kinachostahili kwa mambo yaliyofanyika katika mwili, ikiwa ni kwa uzuri au kwa ubaya.
11 我們既知道主是可畏的,所以勸人。但我們在上帝面前是顯明的,盼望在你們的良心裏也是顯明的。
Kwa hiyo, kwa kuijua hofu ya Bwana, tunawashawishi watu. Jinsi tulivyo, inaonekana wazi na Mungu. Ninatumaini kuwa inaeleweka pia kwenye dhamiri zenu.
12 我們不是向你們再舉薦自己,乃是叫你們因我們有可誇之處,好對那憑外貌不憑內心誇口的人,有言可答。
Hatujaribu kuwashawishi ninyi tena kutuona sisi kama wakweli. Badala yake, tunawapa ninyi sababu ya kujivuna kwa ajili yetu, ili kwamba muweze kuwa na jibu kwa wale wanaojivunia kuhusu mwonekano lakini sio kile kilicho ndani ya moyo.
13 我們若果顛狂,是為上帝;若果謹守,是為你們。
Kwa kuwa ikiwa kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu. Na kama tuko kwenye akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu.
14 原來基督的愛激勵我們;因我們想,一人既替眾人死,眾人就都死了;
Kwa kuwa upendo wa Kristo watushurutisha, kwa sababu tuna uhakika na hili: kuwa mtu mmoja alikufa kwa ajili ya wote, na kwa hiyo wote wamekufa.
15 並且他替眾人死,是叫那些活着的人不再為自己活,乃為替他們死而復活的主活。
Na Kristo alikufa kwa ajili ya wote, ili kwamba wale wanaoishi wasiishi tena kwa ajili yao wenyewe. Badala yake, lazima waishi kwa ajili yake yeye ambaye alikufa na alifufuliwa.
16 所以,我們從今以後,不憑着外貌認人了。雖然憑着外貌認過基督,如今卻不再這樣認他了。
Kwa sababu hii, kuanzia sasa na kuendelea hatumuhukumu mtu kulingana na viwango vya wanadamu, ingawa hapo kwanza tulimtazama Kristo katika namna hii. Lakini sasa hatumuhukumu yeyote kwa namna hii tena.
17 若有人在基督裏,他就是新造的人,舊事已過,都變成新的了。
Kwa hiyo, ikiwa mtu yeyote yuko ndani ya Kristo, yeye ni kiumbe kipya. Mambo ya kale yamepita. Tazama, yamekuwa mapya.
18 一切都是出於上帝;他藉着基督使我們與他和好,又將勸人與他和好的職分賜給我們。
Vitu vyote hivi vyatoka kwa Mungu. Alitupatanisha sisi kwake mwenyewe kupitia Kristo, na ametupatia huduma ya upatanisho.
19 這就是上帝在基督裏,叫世人與自己和好,不將他們的過犯歸到他們身上,並且將這和好的道理託付了我們。
Hiyo ni kusema, katika Kristo, Mungu anaupatanisha ulimwengu kwake mwenyewe, sio kuhesabu makosa yao dhidi yao. Anawekeza kwetu ujumbe wa upatanisho.
20 所以,我們作基督的使者,就好像上帝藉我們勸你們一般。我們替基督求你們與上帝和好。
Kwa hiyo tunateuliwa kama wawakilishi wa Kristo, kana kwamba Mungu alikuwa anafanya rufaa yake kupitia sisi. Tunawasihi ninyi kwa ajili ya Kristo: “Mpatanishwe kwa Mungu!”
21 上帝使那無罪的,替我們成為罪,好叫我們在他裏面成為上帝的義。
Alimfanya Kristo kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye ndiye ambaye hakutenda dhambi. Alifanya hivi ili tuweze kufanyika haki ya Mungu katika yeye.