< 歷代志下 7 >

1 所羅門祈禱已畢,就有火從天上降下來,燒盡燔祭和別的祭。耶和華的榮光充滿了殿;
Sasa Selemani alipokuwa amemaliza kuomba, moto ukaja kutoka mbinguni na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, na utukufu wa Yahwe ukaijaza nyumba.
2 因耶和華的榮光充滿了耶和華殿,所以祭司不能進殿。
Makuhani hawakuweza kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, kwa sababu utukufu wake uliijaza nyumba yake.
3 那火降下、耶和華的榮光在殿上的時候,以色列眾人看見,就在鋪石地俯伏叩拜,稱謝耶和華說: 耶和華本為善, 他的慈愛永遠長存!
Watu wote wa Israeli wakaangalia juu moto uliposhuka chini na utukufu wa Yahwe ulikuwa juu ya nyumba. Wakalala kwa nyuso zao juu ya sakafu ya mawe, wakaabudu, na kutoa shukrani kwa Yahwe. Wakasema, “Kwa maana yeye ni mwema, kwa maana agano lake la kifame ladumu milele.”
4 王和眾民在耶和華面前獻祭。
Kwa hiyo mfalme na watu wote wakamtolea Yahwe sadaka Yahwe.
5 所羅門王用牛二萬二千,羊十二萬獻祭。這樣,王和眾民為上帝的殿行奉獻之禮。
Mfalme Selemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu na kondoo 120, 000 na mbuzi. Kwa hiyo mfalme na watu wote wakaiweka wakifu nyumba ya Mungu.
6 祭司侍立,各供其職;利未人也拿着耶和華的樂器,就是大衛王造出來、藉利未人頌讚耶和華的。(他的慈愛永遠長存!)祭司在眾人面前吹號,以色列人都站立。
Makuhani wakasimama, kila mmoja akasimama mahali pake pa kuhudumu; Walawi pia pamoja na vyombo vya muziki vya Yahwe, ambavyo mfalme Daudi alivitengeza kwa ajili ya kumpa shukrani Yahwe katika nyimbo, “Kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.” Makuhani wote wakapiga matarumbeta mbele yao, na Israeli wote wakasimama.
7 所羅門因他所造的銅壇容不下燔祭、素祭,和脂油,便將耶和華殿前院子當中分別為聖,在那裏獻燔祭和平安祭牲的脂油。
Selemani akaitakasa sehemu ya katikati ya kiwanja cha mfalme mbele ya nyumba ya Yahwe. Humo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba ambayo alikuwa ametengeza haikuweza kuzibeba sadaka, sadaka za nafaka, na za mafuta.
8 那時所羅門和以色列眾人,就是從哈馬口直到埃及小河,所有的以色列人都聚集成為大會,守節七日。
Kwa hiyo Selemani akaitisha sikukuu wakati huo kwa siku saba, na Israeli wote pamaoja naye, kusanyiko kubwa, kutoka Lebo Hamathi mpaka kijito cha Misiri.
9 第八日設立嚴肅會,行奉獻壇的禮七日,守節七日。
Siku ya nane wakaitisha kusanyiko la makini, kwa maana kwa siku saba walishika kuwekwa wakfu kwa ile madhabahu.
10 七月二十三日,王遣散眾民;他們因見耶和華向大衛和所羅門與他民以色列所施的恩惠,就都心中喜樂,各歸各家去了。
Katika siku ya ishini na tatu ya mwezi wa saba, Selemani akawatanya watu kwenda kwenye nyumba zao kwa furaha na mioyo ya shangwe kwa sababu ya wema aliokuwa ameuonesha Yahwe kwa Daudi, Selemani, Israeli, na watu wake.
11 所羅門造成了耶和華殿和王宮;在耶和華殿和王宮凡他心中所要做的,都順順利利地做成了。
Hivyo Selemani akaimaliza nyumba ya Yahwe na nyumba yake mwenyewe. Kila kitu kilichokuja katika moyo wa Selemani kwa ajili ya kukitengeneza katika nyumba ya mfalme na katika nyumba yake mwenyewe, alikitimiza kwa mafanikio.
12 夜間耶和華向所羅門顯現,對他說:「我已聽了你的禱告,也選擇這地方作為祭祀我的殿宇。
Yahwe akamtokea Selemani usiku na kusema kwake, “Nimesikia maombi yako, na nimeichagua sehemu hii kwa ajili yangu mwenyewe kama nyumba ya dhabihu.
13 我若使天閉塞不下雨,或使蝗蟲吃這地的出產,或使瘟疫流行在我民中,
Kama nitazifunga mbingu ili kwamba kusiwepo mvua, au kama nitaamuru nzige waimeze nchi, au kama nitatuma magonjwa kati kati ya watu wangu,
14 這稱為我名下的子民,若是自卑、禱告,尋求我的面,轉離他們的惡行,我必從天上垂聽,赦免他們的罪,醫治他們的地。
kisha watu wangu, ambao wameitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, kuomba, kuutafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya, nitasikia kutoka mbinguni, kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.
15 我必睜眼看、側耳聽在此處所獻的禱告。
Sasa macho yangu yatakuwa wazi na masikio yangu yatasikiliza maombi yanayofanywa katika sehemu hii.
16 現在我已選擇這殿,分別為聖,使我的名永在其中,我的眼、我的心也必常在那裏。
Kwa maana sasa nimeichagua na kauitakasa nyumba hii ili kwamba jina langu lipate kuwa humo milele. Masikio yangu na moyo wangu vitakuwako kila siku.
17 你若在我面前效法你父大衛所行的,遵行我一切所吩咐你的,謹守我的律例典章,
Kwako wewe, kama utatembe mbele zangu kama baba yako Daudi alivyotembea, ukitii yote nilyokuamuru na kuzishika sheria zangu na maagizo yangu,
18 我就必堅固你的國位,正如我與你父大衛所立的約,說:『你的子孫必不斷人作以色列的王。』
basi nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyosema katika agano na Daudi baba yako, niliposema, 'Mzaliwa wako hatashindwa kamwe kuwa mtawala katika Israeli.'
19 「倘若你們轉去丟棄我指示你們的律例誡命,去事奉敬拜別神,
Lakin ukigeuka, na kuzisahau sheria zangu na amri amabzo nimeweka mbele yenu, na kama utaenda kuabudu miungu wengine na kuwasujudia,
20 我就必將以色列人從我賜給他們的地上拔出根來,並且我為己名所分別為聖的殿也必捨棄不顧,使他在萬民中作笑談,被譏誚。
basi nitawang'oa kutoka kwenye nchi yangu amabayo nimewapa. Nyumba hii ambayo nimeitakasa kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali kutoka mbele zangu, na nitaifanya kuwa methali na utani miongini mwa watu wote.
21 這殿雖然甚高,將來經過的人必驚訝說:『耶和華為何向這地和這殿如此行呢?』
Ingawa hekalu hili hili zuri sana kwa sasa, kila mtu apitaye karibu yake atashangazwa na ataguna. Watauliza, 'Kwa nini Yahwe ameifanyia hivi nchi hii na nyumba hii',
22 人必回答說:『是因此地的人離棄耶和華-他們列祖的上帝,就是領他們出埃及地的上帝,去親近別神,敬拜事奉他,所以耶和華使這一切災禍臨到他們。』」
wengine watajibu, 'Kwa sababu walimsahau Yahwe, Mungu wao, ambaye alikuwa amewatoa babu zao nje ya nchi ya Misiri, na wakashikamana na miungu wengine na kuwainamia chini na kuwaabudu. Hii ndiyo maana Yahwe ameleta majanga haya yote juu yao”

< 歷代志下 7 >