< 歷代志下 29 >
1 希西家登基的時候年二十五歲,在耶路撒冷作王二十九年。他母親名叫亞比雅,是撒迦利雅的女兒。
Hezekia alianza kutawala alipokuwa na umri wa miaka ishirini na mitano; alitawala miaka ishini na nane katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Abiya; alikuwa binti wa Zekaria.
2 希西家行耶和華眼中看為正的事,效法他祖大衛一切所行的。
Alifanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi baba yake alivyofanya.
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, katika mwezi wa kwanza, Hezekia aliifungua milango ya nyumba ya Yahwe na kuikarabati.
Akawaleta ndani makuhani na Walawi, na akawakusanya pamoaja katika uwanda upande wa mashariki.
5 對他們說:「利未人哪,當聽我說:現在你們要潔淨自己,又潔淨耶和華-你們列祖上帝的殿,從聖所中除去污穢之物。
Akawaambia, “Nisikilizeni, ninyi Walawi! Jitakaseni wenyewe, na itakaseni nyumba ya Yahwe, Mungu wa babu zenu, na uondoeni mbali uchafu kutoka kwenye sehemu takatifu.
6 我們列祖犯了罪,行耶和華-我們上帝眼中看為惡的事,離棄他,轉臉背向他的居所,
Kwa kuwa babu zetu walikosea na kufanya kilichokuwa uovu katika macaho ya Yahwe Mungu wetu; walimsahau, wakageuzia mbali nyuso zao kutoka sehemu ambapo Yahwe anaishi, na kuigeuzia migongo yao.
7 封鎖廊門,吹滅燈火,不在聖所中向以色列上帝燒香,或獻燔祭。
Pia waliifunga milango ya ukumbi nakuziweka nje taa; hawakufukiza uvumba au kutoa sadaka za kuteketezwa katika sehemu takatifu kwa Mungu wa Israeli.
8 因此,耶和華的忿怒臨到猶大和耶路撒冷,將其中的人拋來拋去,令人驚駭、嗤笑,正如你們親眼所見的。
Kwa hiyo hasira ya Yahwe ilikuwa imeshuka juu ya Yuda na Yerusalemu, na amewafanya kuwa kitu cha wasiwasi, cha hofu, na cha kudharauriwa, kama mnavyoona kwa macho yenu.
9 所以我們的祖宗倒在刀下,我們的妻子兒女也被擄掠。
Hii ndiyo maana mababu zetu wameanguka kwa upanga, na wana wetu, binti zetu, na wake zetu wako katika utumwa kwa sababu ya hili.
10 現在我心中有意與耶和華-以色列的上帝立約,好使他的烈怒轉離我們。
Sasa ni katika moyo wangu kufanya agano na Yahwe, Mungu wa Israeli, ili kwamba hasira yake kali iweze kugeukia mbali nasi.
11 我的眾子啊,現在不要懈怠;因為耶和華揀選你們站在他面前事奉他,與他燒香。」
Wanangu, msiwe wavivu sas, kwa kuwa Yahwe amewachagua kwa ajili ya kusimama mbe yake, kwa ajili ya kumwabudu yeye, na kwamba muwe watumishi wake na kufukiza uvumba.”
12 於是,利未人哥轄的子孫、亞瑪賽的兒子瑪哈,亞撒利雅的兒子約珥;米拉利的子孫、亞伯底的兒子基士,耶哈利勒的兒子亞撒利雅;革順的子孫、薪瑪的兒子約亞,約亞的兒子伊甸;
Basi Walawi wakainuka; Mahathi mwana wa Amasai, na Yoeli mwana wa Azaria, wa watu wa Kohathi; na wa watu wa Merari, Kishi mwana wa Abdi, na Azaria mwana wa Yehaleleli; na wa Wargeshoni, Yoa mwana wa Zimna, na Edeni mwana wa Yoa;
13 以利撒反的子孫申利和耶利;亞薩的子孫撒迦利雅和瑪探雅;
wa wana wa Elisafani, Shimri na Yeueli; wa wana wa Asafu, Zekaria na Matania;
14 希幔的子孫耶歇和示每;耶杜頓的子孫示瑪雅和烏薛;
wa wana wa Hemani, Yehueli na Shimei; na wa wana Yeduthuni, Shemaya na Uzieli.
15 起來聚集他們的弟兄,潔淨自己,照着王的吩咐、耶和華的命令,進去潔淨耶和華的殿。
Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa wenyewe, na wakaenda ndani, kama alivyoamru mfalme, wakifuata maneno ya Yahwe, kwa ajili ya kuisafisha nyumba ya Yahwe.
16 祭司進入耶和華的殿要潔淨殿,將殿中所有污穢之物搬到耶和華殿的院內,利未人接去,搬到外頭汲淪溪邊。
Makuhani wakaenda kwenye sehemu za ndani ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kuisafisha; wakaleta nje uchafu wote walioukuta ndani ya hekalu la Yahwe katika uwanja wa nyumba. Walawi wakauchukua kuubeba nje ya hadi kwnye kijito cha Kidroni.
17 從正月初一日潔淨起,初八日到了耶和華的殿廊,用八日的工夫潔淨耶和華的殿,到正月十六日才潔淨完了。
Sasa wakaanza utakaso katika siku ya kwanza ya mwezi. Katika siku ya nane ya mwezi wakaufikia ukumbi wa Yahwe. Kisha siku nane zaidi wakaitakasa nyumba ya Yahwe. Katika siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza wakamaliza.
18 於是,他們晉見希西家王,說:「我們已將耶和華的全殿和燔祭壇,並壇的一切器皿、陳設餅的桌子,與桌子的一切器皿都潔淨了;
Kisha wakaenda kwa Hezekia, mfalme, ndani ya ikulu na kusema, “Tumeisafisha nyumba yote ya Yahwe, madhabahu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa pamoja na vifaa vyake vyote, na meza ya mkate wa uwepo, pamoja na vifaa vyake vyote.
19 並且亞哈斯王在位犯罪的時候所廢棄的器皿,我們預備齊全,且潔淨了,現今都在耶和華的壇前。」
Kwa hiyo tumejiandaa na tumevitakasa vitu vyote ambavyo Mfalme Ahazi aliviondoa wakati alipoenda kwa ukengeufu katika kipindi cha utawala wake, ona, viko mbele ya madhabahu ya Yahwe.”
20 希西家王清早起來,聚集城裏的首領都上耶和華的殿;
Kisha Hezekia mfalme akaamka mapema asubuhi na kuwakusanya viongozi wa miji; akaenda kwenye nyumba ya Yahwe.
21 牽了七隻公牛,七隻公羊,七隻羊羔,七隻公山羊,要為國、為殿、為猶大人作贖罪祭。王吩咐亞倫的子孫眾祭司,獻在耶和華的壇上,
Wakaleta ng'ombe waume saba, kondoo waume saba, wanakondoo saba, mbuzi waume saba kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya mfalme, kwa ajili ya patakatifu, kwa ajili ya Yuda. Akawaamuru makuhani, wana wa Haruni, kuwatoa sadaka juu ya madhabahu ya Yahwe.
22 就宰了公牛,祭司接血灑在壇上,宰了公羊,把血灑在壇上,又宰了羊羔,也把血灑在壇上;
Kwa hiyo wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu na kuinyunyiza juu ya madhabahu. Wakawachinja kondoo dume, na kunyunyiza damu juu ya madhabahu; Pia wakawachinja wanakondoo na kuinyunyiza damu juu ya madhabahu.
23 把那作贖罪祭的公山羊牽到王和會眾面前,他們就按手在其上。
Wakawaleta mbuzi kwa ajili ya sadka ya dhambi mbele ya mfalme na kusnyiko; wakaweka mikono yao juu ya hao mbuzi.
24 祭司宰了羊,將血獻在壇上作贖罪祭,為以色列眾人贖罪,因為王吩咐將燔祭和贖罪祭為以色列眾人獻上。
Makuhani wakawachinja, na wakafanya sadaka ya dhambi kwa damu yao juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote, kwa maana mfalme alikuwa ameamuru kuwa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya dhambi lazima zifanywe kwa ajili ya Israeli wote.
25 王又派利未人在耶和華殿中敲鈸,鼓瑟,彈琴,乃照大衛和他先見迦得,並先知拿單所吩咐的,就是耶和華藉先知所吩咐的。
Hezekia akawaweka Walawi katika nyumba ya Yahwe wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, akiwapanga kwa amri ya Daaudi, Gadi, mwonaji wa mfalme, na Nathani, nabii, kwa maana amri ilitoka kwa Yahwe kupitia manabii wake.
Walawi wakasimama na vyombo vya Daudi, na makauhani wakasimama na matarumbeta.
27 希西家吩咐在壇上獻燔祭,燔祭一獻,就唱讚美耶和華的歌,用號,並用以色列王大衛的樂器相和。
Hezekia akawaamuru kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Sadaka zilipoanza, wimbo wa Yahwe ukaanza pia, kwa matarumbeta, pamoja na vyombo vya Daudi, mfalme wa Israeli.
28 會眾都敬拜,歌唱的歌唱,吹號的吹號,如此直到燔祭獻完了。
Kusanyiko lote wakaabudu, waimbaji wakaimba, na wapiga matarumbeta wakapiga; yote hayo yakaendele hadi sadaka za kuteketezwa zilizipokwisha.
Walipomaliza kutoa sadaka, mfalme na watu waliokuwepo pamoja naye wakainama, na kusujudu.
30 希西家王與眾首領又吩咐利未人用大衛和先見亞薩的詩詞頌讚耶和華;他們就歡歡喜喜地頌讚耶和華,低頭敬拜。
Vile vile, Hezekia, mfalme, na viongozi wakawaamuru Walawi kuimba ili kumsifu Yahwe kwa maneno ya Daudi na ya Asafu, mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama chini wakasujudu.
31 希西家說:「你們既然歸耶和華為聖,就要前來把祭物和感謝祭奉到耶和華殿裏。」會眾就把祭物和感謝祭奉來,凡甘心樂意的也將燔祭奉來。
Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe. Njoni hapa na mlete sadaka na dhabihu za shukrani katika nyumba ya Yahwe.” Kusanyiko wakaleta sadka na dhabihu za shukrani, na wote waliaokuwa na moyo wa kuhiyalika wakaleta sadka za kuteketezwa.
32 會眾所奉的燔祭如下:公牛七十隻,公羊一百隻,羊羔二百隻,這都是作燔祭獻給耶和華的;
Hesabu ya sadaka za kuteketezwa ambazo kusanyiko walileta ilikuwa ng'ombe sabini, kondoo waume mia moja, na wanakondo waume mia mbili. Wote hao walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe.
Sadaka za kuwekwa wakfu zilikuwa ng'ome mia sita na kondoo elfu tatu.
34 但祭司太少,不能剝盡燔祭牲的皮,所以他們的弟兄利未人幫助他們,直等燔祭的事完了,又等別的祭司自潔了;因為利未人誠心自潔,勝過祭司。
Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuchuna sadaka zote za kuteketezwa, kwa hiyo ndgugu zao, Walawi, wakawasaidia hadi kazi ilipoisha, na hadi makuhani walipoweza kujitakasa wenyewe, kwa maana Walawi walikuwa makaini sana kujitaksa wenyewe kuliko makuhani.
35 燔祭和平安祭牲的脂油,並燔祭同獻的奠祭甚多。這樣,耶和華殿中的事務俱都齊備了。
Zaidi ya hayo, palikuwa na sadaka za kuteketezwa nyingi sana; zilitolewa pamoja na sadaka za mafauta za amani, na kulikuwa na sadaka za vinywaji kwa kila sadaka ya kuteketezwa. Kwa hiyo huduma ya nyumba ya Yahwe ikawekwa katika utaratibu.
36 這事辦的甚速,希西家和眾民都喜樂,是因上帝為眾民所預備的。
Hezekia akafurahia, na watu pia, kwa sababu ya kile ambacho Mungu alikuwa ameandaa kwa ajili ya watu, kwa maana kazi ilikuwa imekamilika haraka.