< 歷代志下 10 >

1 羅波安往示劍去,因為以色列人都到了示劍,要立他作王。
Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa maana Isaraeli wote walikuwa wanakauja Shekemu kwa ajili ya kumfanya yeye mfalme.
2 尼八的兒子耶羅波安先前躲避所羅門王,逃往埃及,住在那裏;他聽見這事,就從埃及回來。
Ikatokea kwamba Yeroboamu mwana wa Nebati akasikia haya (kwa maana alikuwa katika Misiri, ambako alikuw amekimbilia kutoka kwenye uwepo wa Mfalme Selemanai, lakini Yeroboamu akarudi kutoka Misiri).
3 以色列人打發人去請他,他就和以色列眾人來見羅波安,對他說:
Kwa hiyo wakatuma na kumuita yeye, na Yeroboamu na Israeli wote wakaja; wakamwambia Rehoboamu na kusema,
4 「你父親使我們負重軛做苦工,現在求你使我們做的苦工負的重軛輕鬆些,我們就事奉你。」
“Baba yako aliifanya nira yetu ngumu. Kwa hiyo sasa, ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa rahisi, na ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu, na sisi tutakutumikia wewe.”
5 羅波安對他們說:「第三日再來見我吧!」民就去了。
Rehoboamu akawaambia, “Njoni kwangu tena baada ya siku tatu.” Kwa hiyo watu wakaondoka.
6 羅波安之父所羅門在世的日子,有侍立在他面前的老年人,羅波安王和他們商議,說:「你們給我出個甚麼主意,我好回覆這民。」
Mfalme Rehoboamu akaomba ushauri kwa wazee ambao walikuwa wamesimama mbele ya Selemani baba yake wakati alipokuwa hai; akasema, Mnanishauri niwape jibu gani watu hawa?”
7 老年人對他說:「王若恩待這民,使他們喜悅,用好話回覆他們,他們就永遠作王的僕人。」
Wakasema kwake, Ikiwa wewe ni mwema kwa watu hawa na uwapendeze, na sema maneno mazuri kwao, basi siku zote watakuwa watumishi wako.”
8 王卻不用老年人給他出的主意,就和那些與他一同長大、在他面前侍立的少年人商議,
Lakini Rehoboamu akapuuza ushauri wa wazee ambao walimpa, na akashauriana na wanauame vijana ambao walikuwa wa rika lake, ambao walisimama mbele yake.
9 說:「這民對我說:『你父親使我們負重軛,求你使我們輕鬆些』;你們給我出個甚麼主意,我好回覆他們。」
Akawaamabia, “Mnanipa ushauri gani, ili kwamba niwajibu watu waliozungumza kwangu na kusema, “Ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu'?”
10 那同他長大的少年人說:「這民對王說:『你父親使我們負重軛,求你使我們輕鬆些』;王要對他們如此說:『我的小拇指比我父親的腰還粗;
Wanaume vijana mabaoa walikuwa rika la Yeroboamu wakasema kwake, wakisema, “Hivi ndivyo utakavyosema kwa watu waliokuambia kwamba baba yako Selemani aliifanya nira yao nzito, lakini kwamba lazima uifanye nyepesi. Hivi ndivyo utakavyosema kwao, 'Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.
11 我父親使你們負重軛,我必使你們負更重的軛;我父親用鞭子責打你們,我要用蠍子鞭責打你們。』」
Kwa hiyo sasa, ingawa babab yangu aliwatwika nira nzito, nitaiongeza nira yenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini nitawaadhibu kwa nge.”
12 耶羅波安和眾百姓遵着羅波安王所說「你們第三日再來見我」的那話,第三日他們果然來了。
Kwa hiyo Yeroboamu na watu wote wakaja kwa Rehoboamu katika siku ya tatu, kama aliavyosema mfalme, “Rudini kwangu katika siku ya tatu,”
13 羅波安王用嚴厲的話回覆他們,不用老年人所出的主意,
Yeroboamu akasema kwa kwao kwa ukatili, akiupuuza aushauri wa wazee.
14 照着少年人所出的主意對他們說:「我父親使你們負重軛,我必使你們負更重的軛;我父親用鞭子責打你們,我要用蠍子鞭責打你們。」
Akasema kwao akiufuata ushauri wa wanaume vijana, akisema, “Baba yangu aliifanya nira yenu nzito, lakini mimi nitaiongeza. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini mimi nitawaadhibu kwa nge.”
15 王不肯依從百姓;這事乃出於上帝,為要應驗耶和華藉示羅人亞希雅對尼八兒子耶羅波安所說的話。
Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa lilikuw tukio lililoletwa na Mungu, kwamba Yahwe aweze kulitimiza neno lake ambalo Ahiya Mshiloni alikuwa amemwambia Yeroboamu mwana wa Nebati.
16 以色列眾民見王不依從他們,就對王說: 我們與大衛有甚麼分兒呢? 與耶西的兒子並沒有關涉! 以色列人哪,各回各家去吧! 大衛家啊,自己顧自己吧! 於是,以色列眾人都回自己家裏去了。
Israeli wote, walipoona kwamba mfalme hakuwasikiliza, watu wakamjibu na kusema, “Tunasehemu gani katika Daudi? Hatuna urith katika wana wa Yese! Kila mmoja wenu anapaswa kwenda katika hema yake, Israeli. Sasa kila mtu aone nyumba yake, Daudi.” Kwa hiyo Israeli wote wakarudi kwenye hema zao.
17 惟獨住在猶大城邑的以色列人,羅波安仍作他們的王。
Lakini kwa watu wa Yuda walioishi katika miji ya Yuda, Yeroboamu akatawala juu yao.
18 羅波安王差遣掌管服苦之人的哈多蘭往以色列人那裏去,以色列人就用石頭打死他。羅波安王急忙上車,逃回耶路撒冷去了。
Kisha mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, ambaye alikuwa msimamizi wa wafanya kazi, lakini watu wa Israeli walimuua kwa kumpiga mawe. Mfalame Rehoboamu akaingia haraka ndani ya gari lake kwenda Yerusalemu.
19 這樣,以色列人背叛大衛家,直到今日。
Kwa hiyo Israeli wakawa waasi dhidi ya nyumba ya Mungu hadi leo.

< 歷代志下 10 >