< 撒母耳記上 9 >

1 有一個便雅憫人,名叫基士,是便雅憫人亞斐亞的玄孫,比歌拉的曾孫,洗羅的孫子,亞別的兒子,是個大能的勇士。
Basi kulikuwa na mtu mmoja kutoka Benyamini, mtu mashuhuri. Jina lake aliitwa Kishi mwana wa Abieli, mwana wa Zerori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini.
2 他有一個兒子,名叫掃羅,又健壯、又俊美,在以色列人中沒有一個能比他的;身體比眾民高過一頭。
Huyu alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Sauli, kijana mzuri wa uso. Hapakuwapo mwanaume mzuri wa uso kuliko huyu miongoni mwa watu wote wa Israeli. Kutoka mabegani kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wengine.
3 掃羅的父親基士丟了幾頭驢,他就吩咐兒子掃羅說:「你帶一個僕人去尋找驢。」
Na punda wa Kishi, baba yake na Sauli walipotea. hivyo Kishi akamwambia Sauli mwanawe, “Mchukue mmoja wa watumishi; uamke uende kuwatafuta punda,”
4 掃羅就走過以法蓮山地,又過沙利沙地,都沒有找着;又過沙琳地,驢也不在那裏;又過便雅憫地,還沒有找着。
Sauli akapita katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu na akaenda akapita katika nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona. Kisha walipita katika nchi ya Shaalimu, lakini hawakuwa huko. Baadaye alipita katika nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwaona wale punda.
5 到了蘇弗地,掃羅對跟隨他的僕人說:「我們不如回去,恐怕我父親不為驢掛心,反為我們擔憂。」
Na walipofika nchi ya Sufu, Sauli alimwambia mtumishi wake aliyekuwa naye, “Njoo na turudi, pengine baba aweza kuacha kuchunga punda na kuanza kutuhofia sisi.”
6 僕人說:「這城裏有一位神人,是眾人所尊重的,凡他所說的全都應驗。我們不如往他那裏去,或者他能將我們當走的路指示我們。」
Lakini mtumishi akamwmbia, “Sikiliza, Yupo mtu wa Mungu katika mji huu. Naye ni mtu wa kuheshimiwa sana; kila asemalo huwa kweli. Hebu twende huko; labda anaweza kutuambia tupitie wapi katika safari yetu.”
7 掃羅對僕人說:「我們若去,有甚麼可以送那人呢?我們囊中的食物都吃盡了,也沒有禮物可以送那神人,我們還有甚麼沒有?」
Ndipo Sauli akamwambia mtumish iwake, “Lakini kama tukienda kwake, twaweza kumpelekea nini? Maana hata mkate katika mfuko wetu umekwisha, na hakuna zawadi ya kumpelekea mtumishi wa Mungu. Tuna kitu gani?
8 僕人回答掃羅說:「我手裏有銀子一舍客勒的四分之一,可以送那神人,請他指示我們當走的路。」(
Huyo mtumishi akamjibu Sauli na kusema, “Hapa, ninayo robo ya shekeli ya fedha ambayo nitampa mtumishi wa Mungu, atuambie ni njia ipi yatupasa tuiendee.”
9 從前以色列中,若有人去問上帝,就說:「我們問先見去吧!」現在稱為「先知」的,從前稱為「先見」。)
(Zamani katika Israeli, mtu alipotaka kujua neno kuhusu mapenzi ya Mungu, alisema, “Njoo, haya twende kwa mwonaji.” Kwa maana nabii wa leo, zamani aliitwa Mwonaji).
10 掃羅對僕人說:「你說的是,我們可以去。」於是他們往神人所住的城裏去了。
Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, “Umesema vyema. Haya, njoo twende.” Basi wakaenda katika mji ambao mtu wa Mungu alikuwamo.
11 他們上坡要進城,就遇見幾個少年女子出來打水,問她們說:「先見在這裏沒有?」
Walipopanda mlima kuelekea mjini, walikutana na wasichana wakienda kuteka maji; Sauli na mtumishi wake wakawauliza, “Mwonaji hupo hapa?”
12 女子回答說:「在這裏,他在你們前面。快去吧!他今日正到城裏,因為今日百姓要在邱壇獻祭。
Nao wakawajibu, na kusema, “Yupo; tazameni, yuko mbele yenu. Harakisheni, kwa maana anakuja mjini leo, sababu leo watu wanatoa dhabihu zao mahali pa juu.
13 在他還沒有上邱壇吃祭物之先,你們一進城必遇見他;因他未到,百姓不能吃,必等他先祝祭,然後請的客才吃。現在你們上去,這時候必遇見他。」
Mara tu mtakapoingia mjini mtamuona, kabla hajapanda mahali pa juu kla chakula. Watu hawatakula hata atakapokuja, kwa sababu ndiye ataibariki dhabihu; na baadaye wale ambao wamealikwa hula. Basi pandeni, mtamuona sasa hivi.”
14 二人就上去;將進城的時候,撒母耳正迎着他們來,要上邱壇去。
Kwa hiyo walikwea kwenda mjini. Walipokuwa wakiingia mjini, walimuona Samweli akija mbele yao, akipanda kwenda mahali pa juu.
15 掃羅未到的前一日,耶和華已經指示撒母耳說:
Siku moja kabla Sauli hajafika, BWANA alikuwa amemfunulia Samweli:
16 「明日這時候,我必使一個人從便雅憫地到你這裏來,你要膏他作我民以色列的君。他必救我民脫離非利士人的手;因我民的哀聲上達於我,我就眷顧他們。」
“Kesho wakati kama huu nitakutumia mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe utamtia mafuta awe mfalme juu ya watu wangu Israeli. Atawaokoa watu wangu kutoka mkono wa Wafilisti. Kwa kuwa nimewaonea huruma watu wangu na kilio cha kutaka msaada kimenifikia.”
17 撒母耳看見掃羅的時候,耶和華對他說:「看哪,這人就是我對你所說的,他必治理我的民。」
Samweli alipomuona Sauli, BWANA akamwambia, “Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu.”
18 掃羅在城門裏走到撒母耳跟前,說:「請告訴我,先見的寓所在哪裏?」
Ndipo Sauli akaja karibu na Samweli katika lango na kusema, “Niambie nyumba ya Mwonaji iko wapi?
19 撒母耳回答說:「我就是先見。你在我前面上邱壇去,因為你們今日必與我同席;明日早晨我送你去,將你心裏的事都告訴你。
Samweli akamjibu Sauli akisema, “Mimi ndiye mwonaji. Tangulia mbele hadi mahali pa juu, nami nitakueleza kila kitu kilichomoyoni mwako.
20 至於你前三日所丟的那幾頭驢,你心裏不必掛念,已經找着了。以色列眾人所仰慕的是誰呢?不是仰慕你和你父的全家嗎?」
Kama punda wenu waliopotea siku tatu zilizopita, msihofu kuhusu hao punda, kwa kuwa wamekwishapatikana. Na yote yaliyotamanika kwa ajili ya Israeli yanamwangukia nani? Siyo kwako na nyumba ya baba yako yote?”
21 掃羅說:「我不是以色列支派中至小的便雅憫人嗎?我家不是便雅憫支派中至小的家嗎?你為何對我說這樣的話呢?」
Sauli akamjibu na kusema, Siyo mimi Mbenyamini, kutoka kabila lililo dogo sana kwa makabila ya Israeli? Siyo ukoo wangu ulio mdogo sana kwa kabila la Benyamini? Kwa nini basi unaniambia kwa namna hii?”
22 撒母耳領掃羅和他僕人進了客堂,使他們在請來的客中坐首位;客約有三十個人。
Hivyo Samweli akamchukua Sauli na mtumishi wake, akawaingiza ukumbini, akawakalisha mahali pa heshima pa wale walioalikwa, idadi yao takribani watu thelathini.
23 撒母耳對廚役說:「我交給你收存的那一分祭肉現在可以拿來。」
Samweli akamwambia mpishi, “Lete sehemu niliyokupatia, sehemu ambayo nilikwambia hivi, “Itenge.”'
24 廚役就把收存的腿拿來,擺在掃羅面前,撒母耳說:「這是所留下的,放在你面前。吃吧!因我請百姓的時候,特意為你存留這肉到此時。」 當日,掃羅就與撒母耳同席。
Basi mpishi alichukua paja lililokuwa limeinuliwa katika dhabihu na kile kilichokuwa pamoja nalo, akaitenga mbele ya Sauli. Kisha Samweli akasema, “Angalia kile kilichokuwa kimetunzwa kwa ajili yako! Kula, kwa sababu kilitunzwa hadi wakati maalum ufike kwa ajili yako. Na kwa sasa waweza kusema, 'Nimewaalika watu.”' Kwa hiyo Sauli alikula pamoja na Samweli siku hiyo.
25 眾人從邱壇下來進城,撒母耳和掃羅在房頂上說話。
Walipokuwa wamekwisha shuka chini kutoka sehemu ya juu na kuingia mjini, Samweli akazungumza na Sauli darini.
26 次日清早起來,黎明的時候,掃羅在房頂上。撒母耳呼叫他說:「起來吧,我好送你回去。」掃羅就起來,和撒母耳一同出去。
Na kulipopambazuka, Samweli alimwita Sauli darini na kusema, “Amka, kusudi nikusindikize uende zako,” Hivyo Sauli aliamka, na wote wawili, yeye na Samweli walitoka kwenda mtaani.
27 二人下到城角,撒母耳對掃羅說:「要吩咐僕人先走(僕人就先走了);你且站在這裏,等我將上帝的話傳與你聽。」
Walipokuwa wakienda nje ya viunga vya mji, Samweli akamwambia Sauli, “Mwambie mtumishi wako atanguliye mbele yetu(na alitangulia mbele), Lakini wewe sharti usubiri kidogo, nipate kukuambia ujumbe wa Mungu.”

< 撒母耳記上 9 >