< 列王紀上 1 >
Mfalme Daudi alipokuwa mzee sana, walimfunika kwa nguo, lakini hakupata joto.
2 所以臣僕對他說:「不如為我主我王尋找一個處女,使她伺候王,奉養王,睡在王的懷中,好叫我主我王得暖。」
Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, “Na tutafute msichana bikra kwa ajili ya mfalme bwana wetu. Ili amtumikie na kumtunza. Naye atalala kwenye mikono yake ili bwana mfalme wetu apate joto.
3 於是在以色列全境尋找美貌的童女,尋得書念的一個童女亞比煞,就帶到王那裏。
Kwa hiyo wakatafuta msichana mrembo katika mipaka yote ya Israeli. Wakampata Abishagi Mshunami wakamlte kwa mfalme.
4 這童女極其美貌,她奉養王,伺候王,王卻沒有與她親近。
Yule msichana alikuwa mrembo sana. Naye akamtumikia mfalme na kumtunza, Lakini mfalme hakumjua.
5 那時,哈及的兒子亞多尼雅自尊,說:「我必作王」,就為自己預備車輛、馬兵,又派五十人在他前頭奔走。
Wakati huo, Adoniya mwana wa Hagithi alijiinua akisema, “Nitakuwa mfalme.” Kwa hiyo akajiandalia magari na wapanda farasi hamsini ili wapige mbio mbele yake.
6 他父親素來沒有使他憂悶,說:「你是做甚麼呢?」他甚俊美,生在押沙龍之後。
Baba yake alikuwa hajawahi kumsumbua, kwa kusema, “kwa nini umefanya hili na lile?” Adoniya allikuwa mwanamume mzuri sana aliyezaliwa baada ya Absalomu.
7 亞多尼雅與洗魯雅的兒子約押,和祭司亞比亞他商議;二人就順從他,幫助他。
Akashauriana na Yoabu mwana wa Seruya na Abiathari kuhani. Wakamfuata Adoniya wakamsaidia.
8 但祭司撒督、耶何耶大的兒子比拿雅、先知拿單、示每、利以,並大衛的勇士都不順從亞多尼雅。
Lakini Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, nabii Nathani, Shimei, Rei, na watu mashujaa wa Daudi hawakumfuata Adoniya.
9 一日,亞多尼雅在隱‧羅結旁、瑣希列磐石那裏宰了牛羊、肥犢,請他的諸弟兄,就是王的眾子,並所有作王臣僕的猶大人;
Adoniya akataoa dhabihu za Kondoo, na ndama walionona kwenye jiwe la Sohelethi, ambalo liko karibu na Eni Rogeli. Akawakaribisha ndugu zake wote, watoto wa mfalme, wanaume wote wa Yuda, na watumishi wa mfalme.
10 惟獨先知拿單和比拿雅並勇士,與他的兄弟所羅門,他都沒有請。
Lakini hakumkaribisha nabii Nathan, Benaya, wanaume mashujaa, au ndugu yake Sulemani.
11 拿單對所羅門的母親拔示巴說:「哈及的兒子亞多尼雅作王了,你沒有聽見嗎?我們的主大衛卻不知道。
Kisha Nathani akamwambia Bethisheba mama wa Sulemani, akaisema, “Je, haujasikia kuwa Adoniya mwana wa Hagathi amekuwa mfalme, na Daudi bwana wetu halijui hilo?
12 現在我可以給你出個主意,好保全你和你兒子所羅門的性命。
Kwa hiyo sasa nakupa ushauri, ili kwamba uweze kuokoa maisha yako na maisha ya mwanao Suleimani.
13 你進去見大衛王,對他說:『我主我王啊,你不曾向婢女起誓說:你兒子所羅門必接續我作王,坐在我的位上嗎?現在亞多尼雅怎麼作了王呢?』
Nenda kwa mfalme Daudi; ukamwambie, 'Bwana wangu mfalme, Je, haukumwapia mtumishi wako, ukisema, “Hakika Sulemani mwanao atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?” Kwa nini basi Adoniya anatawala?'
14 你還與王說話的時候,我也隨後進去,證實你的話。」
Wakati ukiwa pale ukiongea na mfalme, Nitaingia baada yako na kuthibitisha hayo.
15 拔示巴進入內室見王,王甚老邁,書念的童女亞比煞正伺候王。
Kwa hiyo Bathisheba akaingia chumbani kwa mfalme. Wakati huo mfalme alikuwa mzee sana, na Abishagi Mshunami alikuwa akimtunza mfalme.
Bathisheba akaiinama kifudifudi mbele ya mfalme. Na kisha mfalme akasema, “Una haja gani?”
17 她說:「我主啊,你曾向婢女指着耶和華-你的上帝起誓說:『你兒子所羅門必接續我作王,坐在我的位上。』
Naye akamwambia, “Bwana wangu, ulimwapia mtumishi wako kwa jina la BWANA, Mungu wako, ukisema, 'Hakika Sulemani mwanao atatawala, baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha enzi.'
Sasa, tazama, Adoniya ni mfalme, na bwana wangu mfalme hajui jambo hili.
19 他宰了許多牛羊、肥犢,請了王的眾子和祭司亞比亞他,並元帥約押;惟獨王的僕人所羅門,他沒有請。
Ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, Abiathari kuhani, na Yoabu jemedari wa jeshi, lakini hajamkaribisha Sulemani mtumishi wako.
20 我主我王啊,以色列眾人的眼目都仰望你,等你曉諭他們,在我主我王之後誰坐你的位。
Mfalme bwana wangu, macho yote ya Israeli yako kwako, yakisubiri usemi wako juu ya nani atakayeti kwenye kiti cha enzi baada yako, bwana wangu.
21 若不然,到我主我王與列祖同睡以後,我和我兒子所羅門必算為罪人了。」
Vinginevyo itatokea, wakati bwana wangu atakapolala na baba zake, kwamba Mimi na mwanangu Sulemani kuhesabiwa wahaini.”
Wakati alipokuwa akiendelea na mfalme, nabii Nathani aliingia.
23 有人奏告王說:「先知拿單來了。」拿單進到王前,臉伏於地。
Watumshi wakamwambia mfalme, “Nabii Nathani yuko hapa,” Naye alipoingia mbele ya mfalme, akalala kifudifudi mbele ya mfalme na uso wake ukielekea chini.
24 拿單說:「我主我王果然應許亞多尼雅說『你必接續我作王,坐在我的位上』嗎?
Nathani akamwambia, “Mfalme bwana wangu, Je, umesema, Adoniya atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?
25 他今日下去,宰了許多牛羊、肥犢,請了王的眾子和軍長,並祭司亞比亞他;他們正在亞多尼雅面前吃喝,說:『願亞多尼雅王萬歲!』
kwani leo ameshuka na ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, jemedari wa jeshi, na Abiatahari kuhani. Nao wanakuka na kunywa mbele zake, na kusema, 'Mfalme Adoniya na aishi milele!'
26 惟獨我,就是你的僕人和祭司撒督,耶何耶大的兒子比拿雅,並王的僕人所羅門,他都沒有請。
Lakini mimi, mtumishi wako, Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, na mtumishi wako Suleimani, hajatukaribisha.
27 這事果然出乎我主我王嗎?王卻沒有告訴僕人們,在我主我王之後誰坐你的位。」
Je, bwana wangu mfalme amefanya haya pasipo kutuambia sisi, watumishi wako, ni nani atakayeketi kwenye kiti cha enzi baada yake?”
28 大衛王吩咐說:「叫拔示巴來。」拔示巴就進來,站在王面前。
Ndipo mfalme Daudi lipojibu na kusema, “Mwiteni Bathisheba arudi.” Naye akaja akasimama mbele ya mfalme.
29 王起誓說:「我指着救我性命脫離一切苦難、永生的耶和華起誓。
Mfalme akafanya kiapo akasema, “Kama BWANA aishivyo, ambaye ameniokoa toka tabu zote,
30 我既然指着耶和華-以色列的上帝向你起誓說:你兒子所羅門必接續我作王,坐在我的位上。我今日就必照這話而行。」
kama nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikisema, 'Sulemani mwanao atatawala baada yangu, naye ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha enzi, mahali pangu,' Nitafanya hivi leo.”
31 於是,拔示巴臉伏於地,向王下拜,說:「願我主大衛王萬歲!」
Kisha Bathisheba akalala kifudifudi na sura yake ikielekea chini mbele ya mfalme akasema, “Bwana wangu mfalme Daudi n a aishi milele!”
32 大衛王又吩咐說:「將祭司撒督、先知拿單、耶何耶大的兒子比拿雅召來!」他們就都來到王面前。
Mflme Daudi akasema, “Niitieni Sadoki kuhani, nabii Nathani na Benaya mwana wa Yehoyada.” Nao wakaja mbele ya mfalme.
33 王對他們說:「要帶領你們主的僕人,使我兒子所羅門騎我的騾子,送他下到基訓;
Mfalme akawaambia, “Uwachukue watumishi wangu, bwana wako, na umfanye Sulemani mwanangu apande juu ya nyumba yangu mimi na mkamtelemshe mpaka chini Gihoni.
34 在那裏,祭司撒督和先知拿單要膏他作以色列的王;你們也要吹角,說:『願所羅門王萬歲!』
Na Sadoki kuhani na nabii Nathani wamtawaze awe mfalme wa Israeli na tarumbeta zipigwe, 'Mfalme Suleimani na uishi milele!'
35 然後要跟隨他上來,使他坐在我的位上,接續我作王。我已立他作以色列和猶大的君。」
Kisha njoni mkiwa nyuma yake, naye atakuja na kukaa kwenye kiti changu cha enzi; kwani yeye ndiye atakayekuwa mfalme mahali pangu. Nimemchagua yeye kuwa mtawala wa Israeli na Yuda.”
36 耶何耶大的兒子比拿雅對王說:「阿們!願耶和華-我主我王的上帝也這樣命定。
Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, akasema, “Na iwe hivyo! Na BWANA, Mungu wa mfalme bwana wangu, alithibitishe hilo.
37 耶和華怎樣與我主我王同在,願他照樣與所羅門同在,使他的國位比我主大衛王的國位更大。」
Kama vile BWANA alivyokuwa na mfalme bwana wangu na awe na Sulemani hivyo hivyo, na kuifanya enzi yake kuwa kubwa kuliko zaidi ya enzi ya bwana wangu Daudi.”
38 於是,祭司撒督、先知拿單、耶何耶大的兒子比拿雅,和基利提人、比利提人都下去使所羅門騎大衛王的騾子,將他送到基訓。
Kwa hiyo Sadoki kuhani, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi na Wapelethi wakamfanya Sulemani akapanda juu ya nyumba ya mfalme Daudi; wakamleta Gihoni.
39 祭司撒督就從帳幕中取了盛膏油的角來,用膏膏所羅門。人就吹角,眾民都說:「願所羅門王萬歲!」
Naye Sadoki kuhani akachukua pembe lenye mafuta hemani akamtia mafuta Sulemani kisha wakapiga tarumbeta, na watu wote wakasema, 'Mfalme Sulemani na aishi milele!'
40 眾民跟隨他上來,且吹笛,大大歡呼,聲音震地。
Kisha watu wote wakamfuata, na watu wakapiga zomari wakafurahi furaha kubwa mno, kiasi kwamba dunia ikatetemeka kwa sauti zao.
41 亞多尼雅和所請的眾客筵宴方畢,聽見這聲音;約押聽見角聲就說:「城中為何有這響聲呢?」
Kisha Adoniya na wageni wake waliokuwa pamoja naye wakasikia hayo walipomaliza kula. Yoabu alipozisikia sauti za panda, akasema, “Kwa nini jiji lilko katika hali ya taharuki?”
42 他正說話的時候,祭司亞比亞他的兒子約拿單來了。亞多尼雅對他說:「進來吧!你是個忠義的人,必是報好信息。」
Wakati alipokuwa akiongea, Yonatahani mwana wa Abiathari kuhani alifika. Adoniya akamwambia, “Karibu, 'kwa kuwa wewe wastahili kutuletea habari.”
43 約拿單對亞多尼雅說:「我們的主大衛王誠然立所羅門為王了。
Naye Yonathani akamjibu Adoniya, “Mfalme bwana wetu Daudi amemfanya Sulemani kuwa mfalme.
44 王差遣祭司撒督、先知拿單、耶何耶大的兒子比拿雅,和基利提人、比利提人都去使所羅門騎王的騾子。
Na mfalme amemtuma pamoja naye Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi pamoja na Wapelethi. Wamempandisha Sulemani juu ya nyumba ya mfalme.
45 祭司撒督和先知拿單在基訓已經膏他作王。眾人都從那裏歡呼着上來,聲音使城震動,這就是你們所聽見的聲音;
Sadoki kuhani na nabii Nathani wamemtawaza kuwa mfalme kule Gihoni, na wametokea huko wakifurahi, ndiyo maana jiji liko katika taharuki. Na hizi ndizo sauti ulizosikia.
Pia, Sulemani ameketi kwenye kiti cha enzi cha ufalme.
47 王的臣僕也來為我們的主大衛王祝福,說:『願王的上帝使所羅門的名比王的名更尊榮;使他的國位比王的國位更大。』王就在床上屈身下拜。
Zaidi ya yote, watumishi wa mfalme walikuja kumbariki mfalme bwana wetu Daudi, wakisema, 'Mungu wako na alifanye jina la Sulemani kuwa zuri kuliko jina lako, na kuifanya enzi yako kuwa kubwa kuliko yako.' na mfalme akasujudu mwenyewe kitandani.
48 王又說:『耶和華-以色列的上帝是應當稱頌的;因他賜我一人今日坐在我的位上,我也親眼看見了。』」
Mfalme pia alisema, 'Abarikiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amempa mtu kuketi kwenye enzi yangu siku hii ya leo, na kwamba macho yangu yamejionea hilo.'”
Ndipo wageni wote wa Adoniya walipoogopa sana. Wakasimama na kila mtu akaenda njia yake.
50 亞多尼雅懼怕所羅門,就起來,去抓住祭壇的角。
Pia Adoniya alimwaogopa Sulemani na akasimama, na akaondoka, akachukua pembe la madhabahuni.
51 有人告訴所羅門說:「亞多尼雅懼怕所羅門王,現在抓住祭壇的角,說:『願所羅門王今日向我起誓,必不用刀殺僕人。』」
Kisha Sulemani akaambiwa hilo, wakasema, “Tazama, Adoniya amemwogopa mfalme Sulemani, kwa kuwa ameshikilia pembe la madhabahuni, akisema, 'Mfalme Sulemani na aniapie kwanza kuwa hatamwua mtumishi wake kwa upanga.'”
52 所羅門說:「他若作忠義的人,連一根頭髮也不致落在地上;他若行惡,必要死亡。」
Sulemani akasema, “Kama atajionyesha kuwa ni mtu wa kweli, hakuna hata unywele mmoja utakaoanguka duniani, bali kama uovu utaonekana kwake, atakufa.”
53 於是所羅門王差遣人,使亞多尼雅從壇上下來,他就來,向所羅門王下拜;所羅門對他說:「你回家去吧!」
Kwa hiyo mfalme Sulemani akatuma watu, waliomleta Adoniya kutoka madhabahuni. Naye akaja akapiga magoti kwa Sulemani, na Sulemani akamwambia, “Nenda nyumbani kwako.”