< 列王紀上 16 >

1 耶和華的話臨到哈拿尼的兒子耶戶,責備巴沙說:
Neno la BWANA lilimjia Yehu mwana wa Hanani kinyume cha Baasha, likisema,
2 「我既從塵埃中提拔你,立你作我民以色列的君,你竟行耶羅波安所行的道,使我民以色列陷在罪裏,惹我發怒,
Ingawa Nilikuinua kutoka kwenye mavumbi na kukufanya kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli, Lakini umetembea katika njia za Yeroboamu na umewafanya watu wangu Israeli kufanya dhambi, ili kunikasirisha dhidi ya dhambi zao.
3 我必除盡你和你的家,使你的家像尼八的兒子耶羅波安的家一樣。
Tazama, Nitamfagia kabisa Baasha na familia yake na nitaifanya familia yako kama familia ya Yeroboamu mwana wa Nebati.
4 凡屬巴沙的人,死在城中的必被狗吃,死在田野的必被空中的鳥吃。」
Mbwa watamla yeyote ambaye anatoka kwa Baasha wanaofia mjini, na ndege wa angani watamla yeyote anayaefia shambani.”
5 巴沙其餘的事,凡他所行的和他的勇力,都寫在以色列諸王記上。
Lakini kwa mambo mengine yanayohusiana na Baasha, aliyofanya, na uwezo wake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
6 巴沙與他列祖同睡,葬在得撒。他兒子以拉接續他作王。
Baasha akalala na mababu zake na akazikwa Tirza, na Ela mwanae akawa mfalme mahali pake.
7 耶和華的話臨到哈拿尼的兒子先知耶戶,責備巴沙和他的家,因他行耶和華眼中看為惡的一切事,以他手所做的惹耶和華發怒,像耶羅波安的家一樣,又因他殺了耶羅波安的全家。
Kwa kupitia nabii Yehu mwana wa Hanani neno la BWANA likaja kinyume na Baasha na familia yake, wote kwa sababu ya maovu yote aliyofanya machoni pa BWANA, akamghadhabisha kwa kazi ya mikono yake, kama familia ya Yeroboamu, na kwa sababu alikuwa ameiua familia yote ya Yeroboamu.
8 猶大王亞撒二十六年,巴沙的兒子以拉在得撒登基作以色列王共二年。
Katika mwaka wa kumi na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akaanza kutawala juu ya Israeli kule Tirza; akatawala kwa miaka miwili.
9 有管理他一半戰車的臣子心利背叛他。當他在得撒家宰亞雜家裏喝醉的時候,
Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza.
10 心利就進去殺了他,篡了他的位。這是猶大王亞撒二十七年的事。
Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.
11 心利一坐王位就殺了巴沙的全家,連他的親屬、朋友也沒有留下一個男丁。
Zimri alipoaanza kutawala, mara tu baada ya kukaa kwenye kiti cha enzi, akawaua wanafamilia wote wa Baasha. Hakumwacha mtoto hata mmoja wa kiume, hakuna hata wa ndugu yake wala wa rafiki zake.
12 心利這樣滅絕巴沙的全家,正如耶和華藉先知耶戶責備巴沙的話。
Kwa hiyo Zimri aliingamiza familia yote ya Baasha, kama alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA, ambalo lilinenwa kinyume na Baasha na nabii Yehu,
13 這是因巴沙和他兒子以拉的一切罪,就是他們使以色列人陷在罪裏的那罪,以虛無的神惹耶和華-以色列上帝的怒氣。
kwa dhambi zote za Baasha na za Ela mwanae ambazo walizifanya, ambazo kwazo waliisababisha Israeli kufanya dhambi, kiasi c ha kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuzikasilikia sanamu zao.
14 以拉其餘的事,凡他所行的,都寫在以色列諸王記上。
Kwa mambo mengine yanayohusiana na Ela, yote ambayo alifanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
15 猶大王亞撒二十七年,心利在得撒作王七日。那時民正安營圍攻非利士的基比頓。
Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri alitawala kwa siku saba tu kule Tirza. Jeshi likafanya kambi kule Gibethoni, ambao ni mji wa Wafilisti.
16 民在營中聽說心利背叛,又殺了王,故此以色列眾人當日在營中立元帥暗利作以色列王。
Lile jeshi lililokuwa limeweka kambi kule lilisikika lilksema, “Zimri amepanga njama na amemwua mfalme.” Kwa hiyo siku hiyo hapo kambini, Israeli yote ikamtangaza Omri, mkuu wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli.
17 暗利率領以色列眾人,從基比頓上去,圍困得撒。
Omri akapanda kutoka Gibethoni na Israeli yote pamoja naye, nao wakauhusuru Tirza.
18 心利見城破失,就進了王宮的衛所,放火焚燒宮殿,自焚而死。
Kwa hiyoZimri alipoona kuwa mji umetekwa, akaingia kwenye ngome na akaivamia ikulu ya mfalme na kulichoma moto jengo lote pamoja na yeye; kwa hiyo akafa kwa moto.
19 這是因他犯罪,行耶和華眼中看為惡的事,行耶羅波安所行的,犯他使以色列人陷在罪裏的那罪。
Hii ilikuwa ni kwa sababu ya dhambi alizofanya kwa kufanya maovu mbele ya macho ya BWANA, kwa kutembea katika njia ya Yeroboamu na katika dhambi ambazo alifanya, kiasi cha kuifanya Israeli wafanye dhambi.
20 心利其餘的事和他背叛的情形都寫在以色列諸王記上。
Pia kwa mambo mengiine yanayomhusu Zimri, na fitina yake aliyofanya, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
21 那時,以色列民分為兩半:一半隨從基納的兒子提比尼,要立他作王;一半隨從暗利。
Sasa watu wa Israeli walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili. Nusu ya watu walimfuata Tibni mwana wa Ginathi, wakamfanya kuwa mfalme, na Nusu walimfufata Omri.
22 但隨從暗利的民勝過隨從基納的兒子提比尼的民。提比尼死了,暗利就作了王。
Lakini watu waliomfuata Omri walikuwa na nguvu kuliko wale waliomfuata Tibni mwana wa Ginathi. Kwa hiyo Tibni akafa, na Omri akawa mfalme.
23 猶大王亞撒三十一年,暗利登基作以色列王共十二年;在得撒作王六年。
Omri alianza kutawala juu ya Israeli katika mwaka wa thelathini na moja wa Asa mfalme wa Yuda, naye akatawala miaka kumi na miwili. Alitawala akiwa Tirza kwa miaka sita.
24 暗利用二他連得銀子向撒瑪買了撒馬利亞山,在山上造城,就按着山的原主撒瑪的名,給所造的城起名叫撒馬利亞。
Akakinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa kilo 68 za fedha. Akajenga mji juu ya mlima na ule mji akauita Samaria, kwa sababu ya jina la Shemeri, mmiliki wa awali wa kile kilima.
25 暗利行耶和華眼中看為惡的事,比他以前的列王作惡更甚。
Omri akafanya maovu mbele ya BWANA na akafanya yaliyo maovu zaidi kuliko wale waliokuwa kabla yake.
26 因他行了尼八的兒子耶羅波安所行的,犯他使以色列人陷在罪裏的那罪,以虛無的神惹耶和華-以色列上帝的怒氣。
Kwa kuwa alitembea katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake ambazo kwa hizo aliwaongoza Waisraeli kufanya dhambi, ili kumkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli, ili kuwa na hasira juu ya sanamu zao za ubatili.
27 暗利其餘的事和他所顯出的勇力都寫在以色列諸王記上。
Kwa mambo mengine yanayomhusu Omri ambayo alfanya, na nguvu zake alizoonyesha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
28 暗利與他列祖同睡,葬在撒馬利亞。他兒子亞哈接續他作王。
Kwa hiyo Omri akalala na mababu zake na akazikwa Samaria na Ahabu mwanae akawa mfalme mahali pake.
29 猶大王亞撒三十八年,暗利的兒子亞哈登基作了以色列王。暗利的兒子亞哈在撒馬利亞作以色列王二十二年。
Katika mwaka wa thelathiini na nane wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akaanza kutawala juu ya Israeli. Ahabu mwana wa Omri akatawala Israeli kule Samaria kwa miaka ishirini na mbili.
30 暗利的兒子亞哈行耶和華眼中看為惡的事,比他以前的列王更甚,
Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo maovu mbele ya BWANA, zaidi ya wote waliokuwa kabla yake.
31 犯了尼八的兒子耶羅波安所犯的罪;他還以為輕,又娶了西頓王謁巴力的女兒耶洗別為妻,去事奉敬拜巴力,
Ikawa kidogo tu Ahabu ayaendee makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa hiyo akamwoa Yezebeli binti wa Ethibaali, mfalme wa Wasidoni; akaenda akamwabudu baali na akamsujudia.
32 在撒馬利亞建造巴力的廟,在廟裏為巴力築壇。
Akamjengea madhabahu Baali, ambayo alikuwa ameijenga kule Samaria.
33 亞哈又做亞舍拉,他所行的惹耶和華-以色列上帝的怒氣,比他以前的以色列諸王更甚。
Ahabu akatengeneza Ashera. Ahabu akafanya maovu zaidi kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Isareli, akamkasirisha kuliko wafalme wote wa Israeli waliokuwa kabla yake.
34 亞哈在位的時候,有伯特利人希伊勒重修耶利哥城;立根基的時候,喪了長子亞比蘭;安門的時候,喪了幼子西割,正如耶和華藉嫩的兒子約書亞所說的話。
Katika siku zake Hieli Mbetheli aliijenga tena Yeriko. Akaijenga misingi ya mji kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, naye akayajenga malango ya mji kwa kufiwa na mwanae mdogo Segebu, na walifanya hivi kwa sababu walitii neno la BWANA, ambalo alikuwa amelinena kwa kinywa cha Joshua mwana wa Nuni.

< 列王紀上 16 >