< 哥林多前書 15 >

1 弟兄們,我如今把先前所傳給你們的福音告訴你們知道;這福音你們也領受了,又靠着站立得住,
Sasa ninawakumbusha, akina kaka na akina dada, juu ya injili niliyowahubiria, ambayo mliipokea na kusimama kwayo.
2 並且你們若不是徒然相信,能以持守我所傳給你們的,就必因這福音得救。
Ni katika injili hii mmeokolewa, kama mkilishika imara neno nililowahubiri ninyi, isipokuwa mliamini bure.
3 我當日所領受又傳給你們的:第一,就是基督照聖經所說,為我們的罪死了,
Kama kwanza nilivyo ipokea kwa umuhimu niliileta kwenu kama ilivyo: kwamba kutokana na maandiko, Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu,
4 而且埋葬了;又照聖經所說,第三天復活了,
kutokana na maandiko alizikwa, na kwamba alifufuka siku ya tatu.
5 並且顯給磯法看,然後顯給十二使徒看;
Na kwamba alimtokea Kefa, kisha kwa wale kumi na wawili.
6 後來一時顯給五百多弟兄看,其中一大半到如今還在,卻也有已經睡了的。
Kisha aliwatokea kwa wakati mmoja akina kaka na akina dada zaidi ya mia tano. Wengi wao bado wako hai, lakini baadhi yao wamelala usingizi.
7 以後顯給雅各看,再顯給眾使徒看,
Kisha alimtokea Yakobo, kisha mitume wote.
8 末了也顯給我看;我如同未到產期而生的人一般。
Mwisho wa yote, alinitokea mimi, kama vile kwa mtoto aliye zaliwa katika wakati usio sahihi.
9 我原是使徒中最小的,不配稱為使徒,因為我從前逼迫上帝的教會。
Kwa kuwa mimi ni mdogo kati ya mitume. Sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu.
10 然而,我今日成了何等人,是蒙上帝的恩才成的,並且他所賜我的恩不是徒然的。我比眾使徒格外勞苦;這原不是我,乃是上帝的恩與我同在。
Lakini kwa neema ya Mungu nipo kama nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya bidii kuliko wote. Lakini haikuwa mimi, bali neema ya Mungu iliyo ndani yangu.
11 不拘是我,是眾使徒,我們如此傳,你們也如此信了。
Kwa hiyo kama ni mimi au wao, tuna hubiri hivyo na tunaamini hivyo.
12 既傳基督是從死裏復活了,怎麼在你們中間有人說沒有死人復活的事呢?
Sasa kama Kristo alihubiriwa kama aliyefufuka kwa wafu, iweje baadhi yenu mseme hakuna ufufuo wa wafu?
13 若沒有死人復活的事,基督也就沒有復活了。
Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo pia hakufufuka.
14 若基督沒有復活,我們所傳的便是枉然,你們所信的也是枉然;
Na kama Kristo hakufufuka, hivyo mahubiri yetu ni bure, na imani yenu ni bure.
15 並且明顯我們是為上帝妄作見證的,因我們見證上帝是叫基督復活了。若死人真不復活,上帝也就沒有叫基督復活了。
Na tumepatikana kuwa mashahidi wa uongo kumuhusu Mungu, kwa sababu tulimshushuhudia Mungu kinyume, kusema alimfufua Kristo, wakati hakumfufua.
16 因為死人若不復活,基督也就沒有復活了。
Kama ikiwa wafu hawafufuliwi, Yesu pia hakufufuliwa.
17 基督若沒有復活,你們的信便是徒然,你們仍在罪裏。
Na kama Kristo hakufufuliwa, imani yenu ni bure na bado mko kwenye dhambi zenu.
18 就是在基督裏睡了的人也滅亡了。
Hivyo hata wale waliokufa katika Kristo pia wameangamia.
19 我們若靠基督只在今生有指望,就算比眾人更可憐。
Ikiwa kwa maisha haya peke yake tunaujasiri kwa wakati ujao ndani ya Kristo, watu wote, sisi niwakuhurumiwa zaidi ya watu wote.
20 但基督已經從死裏復活,成為睡了之人初熟的果子。
Lakini sasa Kristo amefufuka kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wale waliokufa.
21 死既是因一人而來,死人復活也是因一人而來。
Kwa kuwa kifo kilikuja kupitia mwanadamu, pia kupitia mwanadamu ufufuo wa wafu.
22 在亞當裏眾人都死了;照樣,在基督裏眾人也都要復活。
Kwa kuwa kama katika Adam wote wanakufa, hivyo pia katika Kristo wote watafanywa hai.
23 但各人是按着自己的次序復活:初熟的果子是基督;以後,在他來的時候,是那些屬基督的。
Lakini kila moja katika mpango wake: Kristo, matunda ya kwanza, na kisha wale walio wa Kristo watafanywa hai wakati wa kuja kwake.
24 再後,末期到了,那時基督既將一切執政的、掌權的、有能的都毀滅了,就把國交與父上帝。
Ndipo utakuwa mwisho, pale Kristo atakapo kabidhi ufalme kwa Mungu Baba. Hii ni pale atakapo komesha utawala wote na mamlaka yote na nguvu.
25 因為基督必要作王,等上帝把一切仇敵都放在他的腳下。
Kwa kuwa lazima atawale mpaka atakapoweka maadui zake wote chini ya nyayo zake.
26 儘末了所毀滅的仇敵就是死。
Adui wa mwisho kuharibiwa ni kifo.
27 因為經上說:「上帝叫萬物都服在他的腳下。」既說萬物都服了他,明顯那叫萬物服他的,不在其內了。
Kwa kuwa “ameweka kila kitu chini ya nyayo zake.” Lakini inaposema “ameweka kila kitu,” ni wazi kwamba hii haihusishi wale walioweka kila kitu chini yake mwenyewe.
28 萬物既服了他,那時子也要自己服那叫萬物服他的,叫上帝在萬物之上,為萬物之主。
Wakati vitu vyote vimewekwa chini yake, kisha Mwana mwenyewe atawekwa chini kwake Yeye ambaye aliviweka vitu vyote chini yake. Hii itatokea ili kwamba Mungu Baba awe yote katika vyote.
29 不然,那些為死人受洗的,將來怎樣呢?若死人總不復活,因何為他們受洗呢?
Au pia watafanya nini wale waliobatizwa kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kabisa, kwa nini tena wanabatizwa kwa ajili yao?
30 我們又因何時刻冒險呢?
Na kwa nini tuko katika hatari kila saa?
31 弟兄們,我在我主基督耶穌裏,指着你們所誇的口極力地說,我是天天冒死。
Kaka na dada zangu, kupitia kujisifu kwangu katika ninyi, ambayo ninayo katika Kristo Yesu Bwana wetu, natangaza hivi: nakufa kila siku.
32 我若當日像尋常人,在以弗所同野獸戰鬥,那於我有甚麼益處呢?若死人不復活, 我們就吃吃喝喝吧! 因為明天要死了。
Inanifaidia nini, katika mtazamo wa wanadamu, kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, kama wafu hawafufuliwi? “Acha basi tule na kunywa, kwa kuwa kesho tunakufa.”
33 你們不要自欺;濫交是敗壞善行。
Msidanganywe: “Makundi mabaya huharibu tabia njema.
34 你們要醒悟為善,不要犯罪,因為有人不認識上帝。我說這話是要叫你們羞愧。
“Muwe na kiasi! muishi katika haki! msiendelee kutenda dhambi. Kwa kuwa baadhi yenu hamna maarifa ya Mungu. Nasema hivi kwa aibu yenu.
35 或有人問:「死人怎樣復活,帶着甚麼身體來呢?」
Lakini mtu mwingine atasema, “Jinsi gani wafu wanafufuliwa? Nao watakuja na aina gani ya mwili?”
36 無知的人哪,你所種的,若不死就不能生。
Wewe ni mjinga sana! Kile ulichopanda hakiwezi kuanza kukua isipokuwa kimekufa.
37 並且你所種的不是那將來的形體,不過是子粒,即如麥子,或是別樣的穀。
Na kile unachopanda sio mwili ambao utakuwa, bali ni mbegu iliyochipua. Inaweza kuwa ngano au kitu kingine.
38 但上帝隨自己的意思給他一個形體,並叫各等子粒各有自己的形體。
Lakini Mungu ataipa mwili kama apendavyo, na katika kila mbengu mwili wake mwenyewe.
39 凡肉體各有不同:人是一樣,獸又是一樣,鳥又是一樣,魚又是一樣。
Miili yote haifanani. Isipokuwa, kuna mwili mmoja wa wanadamu, na mwili mwingine wa wanyama, na wili mwingine wa ndege, na mwingine kwa ajili ya samaki.
40 有天上的形體,也有地上的形體;但天上形體的榮光是一樣,地上形體的榮光又是一樣。
Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani. Lakini utukufu wa miili ya mbinguni ni aina moja na utukufu wa duniani ni mwingine.
41 日有日的榮光,月有月的榮光,星有星的榮光;這星和那星的榮光也有分別。
Kuna utukufu mmoja wa jua, na utukufu mwingine wa mwezi, na utukufu mwingine wa nyota. Kwa kuwa nyota moja inatofautiana na nyota nyingine katika utukufu.
42 死人復活也是這樣:所種的是必朽壞的,復活的是不朽壞的;
Hivyo ndivyo ulivyo pia ufufuo wa wafu. Kinacho pandwa kinaharibika, na kinacho ota hakiharibiki.
43 所種的是羞辱的,復活的是榮耀的;所種的是軟弱的,復活的是強壯的;
Kimepandwa katika matumizi ya kawaida, kinaoteshwa katika utukufu. Kimepandwa katika udhaifu, kinaoteshwa katika nguvu.
44 所種的是血氣的身體,復活的是靈性的身體。若有血氣的身體,也必有靈性的身體。
Kimepandwa katika mwili wa asili, kinaoteshwa katika mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, kuna mwili wa kiroho pia.
45 經上也是這樣記着說:「首先的人亞當成了有靈的活人」;末後的亞當成了叫人活的靈。
Hivyo pia imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika roho inayo ishi.” Adamu wa mwisho alifanyika roho itoayo uhai.
46 但屬靈的不在先,屬血氣的在先,以後才有屬靈的。
Lakini wa kiroho hakuja kwanza bali wa asili, na kisha wa kiroho.
47 頭一個人是出於地,乃屬土;第二個人是出於天。
Mtu wa kwanza ni wa dunia, alitengenezwa kwa mavumbi. Mtu wa pili anatoka mbinguni.
48 那屬土的怎樣,凡屬土的也就怎樣;屬天的怎樣,凡屬天的也就怎樣。
Kama vile yule aliyetengenezwa kwa mavumbi, hivyo pia wale waliotengenezwa kwa mavumbi. Kama vile mtu wa mbinguni alivyo, hivyo pia wale wa mbinguni.
49 我們既有屬土的形狀,將來也必有屬天的形狀。
Kama ambavyo tumebeba mfano wa mtu wa mavumbi, tutabeba pia mfano wa mtu wa mbinguni.
50 弟兄們,我告訴你們說,血肉之體不能承受上帝的國,必朽壞的不能承受不朽壞的。
Sasa nawaambia, kaka na dada zangu, kwamba mwili na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu. Wala wakuharibika kurithi wakutoharibika.
51 我如今把一件奧祕的事告訴你們:我們不是都要睡覺,乃是都要改變,
Tazama! Nawaambia ninyi siri ya kweli: Hatutakufa wote, bali wote tutabadilishwa.
52 就在一霎時,眨眼之間,號筒末次吹響的時候。因號筒要響,死人要復活成為不朽壞的,我們也要改變。
Tutabadilishwa katika wakati, katika kufumba na kufumbua kwa jicho, katika tarumbeta ya mwisho. Kwa kuwa tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa na hali ya kutoharibika, na tutabadilishwa.
53 這必朽壞的總要變成不朽壞的,這必死的總要變成不死的。
Kwani huu wa kuharibika lazima uvae wa kutoharibika, na huu wa kufa lazima uvae wa kutokufa.
54 這必朽壞的既變成不朽壞的,這必死的既變成不死的,那時經上所記「死被得勝吞滅」的話就應驗了。
Lakini wakati huu wa kuharibika ukivikwa wa kutokuharibika, na huu wa kufa ukivaa wa kutokufa, ndipo utakuja msemo ambao umeandikwa, “Kifo kimemezwa katika ushindi.”
55 死啊!你得勝的權勢在哪裏? 死啊!你的毒鉤在哪裏? (Hadēs g86)
“Kifo, ushindi wako uko wapi? Kifo, uko wapi uchungu wako?” (Hadēs g86)
56 死的毒鉤就是罪,罪的權勢就是律法。
Uchungu wa kifo ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni sheria.
57 感謝上帝,使我們藉着我們的主耶穌基督得勝。
Lakini shukurani kwa Mungu, atupaye sisi ushindi kupitia Bwana wetu Yesu Kristo!
58 所以,我親愛的弟兄們,你們務要堅固,不可搖動,常常竭力多做主工;因為知道,你們的勞苦在主裏面不是徒然的。
Kwa hiyo, wapendwa kaka na dada zangu, iweni imara na msitikisike. Daima itendeni kazi ya Bwana, kwa sababu mnajua kuwa kazi yenu katika Bwana siyo bure.

< 哥林多前書 15 >