< 撒迦利亚书 13 >
1 “那日,必给大卫家和耶路撒冷的居民开一个泉源,洗除罪恶与污秽。”
“Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.
2 万军之耶和华说:“那日,我必从地上除灭偶像的名,不再被人记念;也必使这地不再有假先知与污秽的灵。
“Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi.
3 若再有人说预言,生他的父母必对他说:‘你不得存活,因为你托耶和华的名说假预言。’生他的父母在他说预言的时候,要将他刺透。
Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la Bwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.
4 那日,凡作先知说预言的必因他所论的异象羞愧,不再穿毛衣哄骗人。
“Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu.
5 他必说:‘我不是先知,我是耕地的;我从幼年作人的奴仆。’
Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’
6 必有人问他说:‘你两臂中间是什么伤呢?’他必回答说:‘这是我在亲友家中所受的伤。’”
Ikiwa mtu atamuuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’
7 万军之耶和华说: 刀剑哪,应当兴起, 攻击我的牧人和我的同伴。 击打牧人,羊就分散; 我必反手加在微小者的身上。
“Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu, dhidi ya mtu aliye karibu nami!” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika, nami nitageuza mkono wangu dhidi ya walio wadogo,
8 耶和华说:这全地的人, 三分之二必剪除而死, 三分之一仍必存留。
katika nchi yote,” asema Bwana, “theluthi mbili watapigwa na kuangamia; hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.
9 我要使这三分之一经火, 熬炼他们,如熬炼银子; 试炼他们,如试炼金子。 他们必求告我的名, 我必应允他们。 我要说:这是我的子民。 他们也要说:耶和华是我们的 神。
Hii theluthi moja nitaileta katika moto; nitawasafisha kama fedha isafishwavyo na kuwajaribu kama dhahabu. Wataliitia Jina langu nami nitawajibu; nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’ nao watasema, ‘Bwana ni Mungu wetu.’”