< 启示录 18 >
1 此后,我看见另有一位有大权柄的天使从天降下,地就因他的荣耀发光。
Baada ya vitu hivi nilimwona malaika mwingine akishuka chini kutoka mbinguni. Yeye alikuwa na mamlaka kuu, na nchi iliangazwa kwa utukufu wake.
2 他大声喊着说: 巴比伦大城倾倒了!倾倒了! 成了鬼魔的住处 和各样污秽之灵的巢穴, 并各样污秽可憎之雀鸟的巢穴。
Alilia kwa sauti kuu, akisema, “Umeanguka, umeanguka, ule mji mkuu Babeli! Umekuwa sehemu yakaapo mapepo, na sehemu ikaapo kila roho chafu, na sehemu akaapo kila mchafu na ndege achukizaye.
3 因为列国都被她邪淫大怒的酒倾倒了。 地上的君王与她行淫; 地上的客商因她奢华太过就发了财。
Kwa kuwa mataifa yote yamekunywa mvinyo ya tamaa ya uasherati wake ambayo humletea ghadhabu. Wafalme wa nchi wamezini naye. Wafanyabiashara wa nchi wamekuwa matajiri kwa nguvu ya maisha yake ya anasa.”
4 我又听见从天上有声音说: 我的民哪,你们要从那城出来, 免得与她一同有罪,受她所受的灾殃;
Kisha nilisikia sauti nyingine kutoka mbinguni iikisema, “Tokeni kwake watu wangu, ili msije mkashiriki katika dhambi zake, na ili msije mkapokea mapigo yake yoyote.
5 因她的罪恶滔天; 她的不义, 神已经想起来了。
Dhambi zake zimerundikana juu kama mbingu, na Mungu ameyakumbuka matendo yake maovu.
6 她怎样待人,也要怎样待她, 按她所行的加倍地报应她; 用她调酒的杯加倍地调给她喝。
Mlipeni kama alivyowalipa wengine, na mkamlipe mara mbili kwa jinsi alivyotenda; katika kikombe alichokichanganya, mchanganyishieni mara mbili kwa ajili yake.
7 她怎样荣耀自己,怎样奢华, 也当叫她照样痛苦悲哀, 因她心里说: 我坐了皇后的位, 并不是寡妇, 决不至于悲哀。
Kama alivyojitukuza yeye mwenyewe, na aliishi kwa anasa, mpeni mateso mengi na huzuni. Kwa kuwa husema moyoni mwake, 'Nimekaa kama malkia; wala siyo mjane, na wala sitaona maombolezo.'
8 所以在一天之内, 她的灾殃要一齐来到, 就是死亡、悲哀、饥荒。 她又要被火烧尽了, 因为审判她的主 神大有能力。
Kwa hiyo ndani ya siku moja mapigo yake yatamlemea: kifo, maombolezo, na njaa. Atateketezwa kwa moto, kwa kuwa Bwana Mungu ni mwenye nguvu, na ni mhukumu wake.”
9 地上的君王,素来与她行淫、一同奢华的,看见烧她的烟,就必为她哭泣哀号。
Wafalme wa nchi waliozini na kuchanganyikiwa pamoja naye watalia na kumwombolezea watakapouona moshi wa kuungua kwake.
10 因怕她的痛苦,就远远地站着说:哀哉!哀哉! 巴比伦大城,坚固的城啊, 一时之间你的刑罚就来到了。
Watasimama mbali naye, kwa hofu ya maumivu yake wakisema, “Ole, ole kwa mji mkuu, Babeli, mji wenye nguvu! Kwa saa moja hukumu yako imekuja.”
11 地上的客商也都为她哭泣悲哀,因为没有人再买他们的货物了;
Wafanyabiashara wa nchi lieni na kuomboleza kwa ajili yake, kwa kuwa hakuna hata mmoja anunuaye bidhaa zake tena -
12 这货物就是金、银、宝石、珍珠、细麻布、紫色料、绸子、朱红色料、各样香木、各样象牙的器皿、各样极宝贵的木头,和铜、铁、汉白玉的器皿,
bidhaa za dhahabu, fedha, mawe ya thamani, lulu, kitani nzuri, zambarau, hariri, nyekundu, aina zote za miti ya harufu nzuri, kila chombo cha pembe za ndovu, kila chombo kilichotengenezwa kwa miti ya thamani, shaba, chuma, jiwe,
13 并肉桂、豆蔻、香料、香膏、乳香、酒、油、细面、麦子、牛、羊、车、马,和奴仆、人口。
mdalasini, viungo, uvumba, manemane, ubani, mvinyo, mafuta, unga mzuri, ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, na watumwa, na roho za watu.
14 巴比伦哪,你所贪爱的果子离开了你; 你一切的珍馐美味 和华美的物件也从你中间毁灭, 决不能再见了。
Matunda uliyoyatamani kwa nguvu zako yameondoka kutoka kwako. Anasa zako zote na mapambo yametoweka, hayatapatikana tena.
15 贩卖这些货物、借着她发了财的客商,因怕她的痛苦,就远远地站着哭泣悲哀,说:
Wafanyabiashara wa vitu hivi waliopata utajiri kwa mapenzi yake watasimama mbali kutoka kwake kwa sababu ya hofu ya maumivu yake, wakilia na sauti ya maombolezo.
16 哀哉!哀哉!这大城啊, 素常穿着细麻、 紫色、朱红色的衣服, 又用金子、宝石,和珍珠为妆饰。
Wakisema, “Ole, ole mji ule mkuu uliovikwa kitani nzuri, zambarau, na nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na vito vya thamani na lulu!”
17 一时之间,这么大的富厚就归于无有了。 凡船主和坐船往各处去的,并众水手,连所有靠海为业的,都远远地站着,
Ndani ya saa moja utajiri wote huo ulitoweka. Kila nahodha wa meli, kila baharia, na wote wanamaji, na wote wafanyao kazi baharini, walisimama mbali.
18 看见烧她的烟,就喊着说:“有何城能比这大城呢?”
Walilia walipouona moshi wa kuungua kwake. Walisema, “Ni mji gani unafanana na mji huu mkubwa?”
19 他们又把尘土撒在头上,哭泣悲哀,喊着说: 哀哉!哀哉!这大城啊。 凡有船在海中的,都因她的珍宝成了富足! 她在一时之间就成了荒场!
Walitupa mavumbi juu ya vichwa vyao, na walilia, wakitokwa machozi na kuomboleza, “Ole, ole mji mkubwa mahali wote waliokuwa na meli zao baharini walikuwa matajiri kutokana na mali zake. Ndani ya saa moja umeangamizwa.”
20 天哪,众圣徒、众使徒、众先知啊, 你们都要因她欢喜, 因为 神已经在她身上伸了你们的冤。
“Furahini juu yake, mbingu, ninyi waumini, mitume, na manabii, kwa maana Mungu ameleta hukumu yenu juu yake!”
21 有一位大力的天使举起一块石头,好像大磨石,扔在海里,说: 巴比伦大城也必这样猛力地被扔下去, 决不能再见了。
Malaika mwenye nguvu aliinua jiwe kama jiwe kuu la kusagia na alilitupa baharini, akisema, “Kwa njia hii, Babeli, ule mji mkuu, utatupwa chini kwa ukatili na hautaonekana tena.
22 弹琴、作乐、吹笛、吹号的声音, 在你中间决不能再听见; 各行手艺人在你中间决不能再遇见; 推磨的声音在你中间决不能再听见;
Sauti ya vinanda, wanamuziki, wacheza filimbi, na tarumbeta hawatasikika tena kwenu. Wala fundi wa aina yoyote hataonekana kwenu. Wala sauti ya kinu haitasikika tena kwenu.
23 灯光在你中间决不能再照耀; 新郎和新妇的声音,在你中间决不能再听见。 你的客商原来是地上的尊贵人; 万国也被你的邪术迷惑了。
Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako. Sauti ya bwana harusi na bibi harusi hazitasikiwa tena ndani yako, maana wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, na wa mataifa, wamedanganywa kwa uchawi wako.
24 先知和圣徒,并地上一切被杀之人的血,都在这城里看见了。
Ndani yake damu ya manabii na waamini ilionekana, na damu ya wote waliouawa juu ya nchi.”