< 诗篇 12 >

1 大卫的诗,交与伶长。调用第八。 耶和华啊,求你帮助,因虔诚人断绝了; 世人中间的忠信人没有了。
Msaada, Yahweh, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; nao waaminifu wametokomea.
2 人人向邻舍说谎; 他们说话,是嘴唇油滑,心口不一。
Kila mmoja anasema kwa jirani yake maneno matupu; kila mmoja anaongea kwa midomo yenye sifa za uongo na maneno ya udanganyifu.
3 凡油滑的嘴唇和夸大的舌头, 耶和华必要剪除。
Yahweh, katilia mbali midomo yenye sifa za uongo, kila ulimi unanena kwa nguvu mambo makubwa.
4 他们曾说:我们必能以舌头得胜; 我们的嘴唇是我们自己的, 谁能作我们的主呢?
Hawa ni wale ambao wamesema, “Kwa ndimi zetu tutashinda. Wakati midomo yetu itakapo ongea, ni nani atakaye kuwa mtawala juu yetu?”
5 耶和华说:因为困苦人的冤屈 和贫穷人的叹息, 我现在要起来, 把他安置在他所切慕的稳妥之地。
“Kwa sababu ya vurugu zilizopo kinyume na maskini, na kwa sababu ya kuugua kwao wahitaji, Nitainuka,” asema Yahwe. “Nitawaletea usalama wanao hitaji.”
6 耶和华的言语是纯净的言语, 如同银子在泥炉中炼过七次。
Maneno ya Yahwe ni masafi, kama fedha iliyo safishwa katika tanuru duniani, iliyo ng'arishwa mara saba zaidi.
7 耶和华啊,你必保护他们; 你必保佑他们永远脱离这世代的人。
Wewe ni Yahwe! Unaye watunza. Una wahifadhi wacha Mungu kutoka katika hiki kizazi cha waovu na hata milele.
8 下流人在世人中升高, 就有恶人到处游行。
Waovu hutembea kila pande pale uovu unapoinuliwa kati ya wanadamu.

< 诗篇 12 >