< 何西阿书 12 >

1 以法莲吃风,且追赶东风, 时常增添虚谎和强暴, 与亚述立约,把油送到埃及。
Efraimu hujilisha upepo na kufuata upepo wa mashariki. Yeye daima huzidisha uongo na unyanyasaji. Wanafanya agano na Ashuru na huchukua mafuta ya Misri.
2 耶和华与犹大争辩, 必照雅各所行的惩罚他, 按他所做的报应他。
Bwana pia ana mashtaka dhidi ya Yuda na ataadhibu Yakobo kwa yale aliyoyatenda; atamlipa kwa matendo yake.
3 他在腹中抓住哥哥的脚跟, 壮年的时候与 神较力,
Katika tumbo Yakobo akamshika ndugu yake kisigino, na katika ubinadamu wake alijitahidi kwa Mungu.
4 与天使较力,并且得胜, 哭泣恳求, 在伯特利遇见耶和华。 耶和华—万军之 神在那里晓谕我们以色列人; 耶和华是他可记念的名。
Alishindana na malaika akashinda. Alilia na kuomba kwa neema yake. Alikutana na Mungu huko Betheli; huko Mungu aliongea naye.
5
Huyu ndiye Bwana, Mungu wa majeshi; “Yahweh” ndilo jina lake.
6 所以你当归向你的 神, 谨守仁爱、公平,常常等候你的 神。
Basi tembea kwa Mungu wako. Shika uaminifu na uhuru wa agano, na umsubiri Mungu wako daima.
7 以法莲是商人, 手里有诡诈的天平,爱行欺骗。
Wafanyabiashara wana mizani ya uongo mikononi mwao; wanapenda kudanganya.
8 以法莲说: 我果然成了富足,得了财宝; 我所劳碌得来的, 人必不见有什么不义,可算为罪的。
Efraimu akasema, “Kwa hakika mimi ni tajiri sana; Nimepata utajiri kwa nafsi yangu. Katika kazi yangu yote hawataona uovu wowote ndani yangu, chochote ambacho kitakuwa dhambi.”
9 自从你出埃及地以来, 我就是耶和华—你的 神; 我必使你再住帐棚,如在大会的日子一样。
Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, tangu ulipotoka nchi ya Misri. Nitakufanya uishi tena katika hema, kama siku za karamu iliyowekwa.
10 我已晓谕众先知, 并且加增默示, 借先知设立比喻。
Niliwaambia manabii, na nimewapa maono mengi kwa ajili yenu. Kwa mkono wa manabii nilitoa mifano.
11 基列人没有罪孽吗? 他们全然是虚假的。 人在吉甲献牛犊为祭, 他们的祭坛好像田间犁沟中的乱堆。
Ikiwa kuna uovu huko Gileadi, hakika watu hawafai. Gilgali wanachinja ng'ombe; madhabahu zao zitakuwa kama miundo ya jiwe katika miamba ya mashamba.
12 从前雅各逃到亚兰地, 以色列为得妻服事人, 为得妻与人放羊。
Yakobo akakimbia mpaka nchi ya Aramu; Israeli alifanya kazi ili kupata mke; naye akachunga kundi la kondoo ili kupata mke.
13 耶和华借先知领以色列从埃及上来; 以色列也借先知而得保存。
Bwana akawaleta Israeli kutoka Misri kwa kutumia nabii, naye akawatunza kwa nabii.
14 以法莲大大惹动主怒, 所以他流血的罪必归在他身上。 主必将那因以法莲所受的羞辱归还他。
Efraimu amemkasirisha sana Bwana. Basi Bwana wake ataachia damu yake, naye atamrudishia aibu yake.

< 何西阿书 12 >