< 历代志下 17 >

1 亚撒的儿子约沙法接续他作王,奋勇自强,防备以色列人,
Yehoshafati mwana wa Asa akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoshafati akajiimarisha dhidi ya Israeli.
2 安置军兵在犹大一切坚固城里,又安置防兵在犹大地和他父亚撒所得以法莲的城邑中。
Akaweka majeshi katika miji yote Yuda yenye ngome, na akaweka magereza katika nchi ya Yuda na katika miji ya Efraimu, ambayo Asa baba yake alikuwa ameiteka.
3 耶和华与约沙法同在;因为他行他祖大卫初行的道,不寻求巴力,
Yahwe alikuwa pamoja na Yehoshafati kwa sababu alitembea katika njia za kwanza za baba yake Daudi, na hakuwatafuta Mabaali. (Baadhi ya mandiko ya kale hayana “Daudi”, na baadhi ya matoleo ya kisasa yameacha hili jina “Daudi).
4 只寻求他父亲的 神,遵行他的诫命,不效法以色列人的行为。
Badala yake, alimtegemea Mungu wa baba yake, na alitembea katika amri zake, siyo katika tabia ya Israeli.
5 所以耶和华坚定他的国,犹大众人给他进贡;约沙法大有尊荣资财。
Kwa hiyo Yahwe akaimarisha sheria katika mkono wake; Yuda wote wakaleta kodi kwa Yehoshafati. Alikuwa na utajiri na heshima kubwa.
6 他高兴遵行耶和华的道,并且从犹大除掉一切邱坛和木偶。
Moyo wake ulikuwa umejikita katika njia za Yahwe. Pia aliziondoa sehemu za juu na Maashera mbali na Yuda.
7 他作王第三年,就差遣臣子便·亥伊勒、俄巴底、撒迦利雅、拿坦业、米该亚往犹大各城去教训百姓。
Katika mwaka wa tatu wa utawala wake aliwatuma wakuu wake Ben-haili, Obadia, Zekaria, Nethania, na Mikaya, ili wafundishe katika miji ya Yuda.
8 同着他们有利未人示玛雅、尼探雅、西巴第雅、亚撒黑、示米拉末、约拿单、亚多尼雅、多比雅、驼·巴多尼雅,又有祭司以利沙玛、约兰同着他们。
Pamoja nao walikuwepo Walawi: Shemaya, Nethanieli, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, na Tob-adonia, pamoja nao walikuwepo makuhani Elishama na Yehoramu.
9 他们带着耶和华的律法书,走遍犹大各城教训百姓。
Walifundisha katika Yuda, wakiwa na kitabau cha sheria ya Yahwe. Wakaenda karibu miji yote ya Yuda na kufundisha miongoni mwa watu.
10 耶和华使犹大四围的列国都甚恐惧,不敢与约沙法争战。
Hofu ya Yahwe ikashuka juu ya falme zote za nchi, zilizouzunguka Yuda, kwa hiyo hazikufanya vita dhidi ya Yehoshafati.
11 有些非利士人与约沙法送礼物,纳贡银。阿 拉伯人也送他公绵羊七千七百只,公山羊七千七百只。
Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi, fedha kama kodi. Waarabu pia wakamletea makundi, 7, 700 kondoo waume, na mbuzi 7, 770.
12 约沙法日渐强大,在犹大建造营寨和积货城。
Yehoshafati akawa na nguvu sana.
13 他在犹大城邑中有许多工程,又在耶路撒冷有战士,就是大能的勇士。
Akajenga ngome na miji ya maghala katika Yuda. Alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda, na wanajeshsi—imara, wanaume hodari—katika Yerusalemu.
14 他们的数目,按着宗族,记在下面:犹大族的,千夫长押拿为首率领大能的勇士—三十万;
Hapa ni rodha yao, wamepangwa kwa majina ya nyumba za baba zo: Kutoka Yuda, maakida wa maelfu; Adna yule jemedari, na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 300, 000;
15 其次是,千夫长约哈难率领大能的勇士—二十八万;
akifuatiwa na Yehonani jemedari, na pamoja naye wanaume 280, 00;
16 其次是,细基利的儿子亚玛斯雅(他为耶和华牺牲自己)率领大能的勇士—二十万。
akifuatiwa na Amasia mwana wa Zikri, ambaye kwa hiari alijitoa kumtumikia Yahwe; na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 200, 000.
17 便雅悯族,是大能的勇士以利雅大率领拿弓箭和盾牌的—二十万;
Kutoka Benyamini: Eliada mtu jasiri, na pamoja naye watu 200, 000 waliovaa upinde na ngao;
18 其次是,约萨拔率领预备打仗的—十八万。
akifutiwa na Yehozabadi, na pamoja naye askari 180, 000 waliotayari kwa vita.
19 这都是伺候王的,还有王在犹大全地坚固城所安置的不在其内。
Hawa walikuwa ni wale ambao walimtumikia mfalme, miongoni mwao wale ambao mfalme aliwaweka katika miji ya ngome katika Yuda yote.

< 历代志下 17 >