< 撒迦利亞書 3 >

1 [第四個神視:撒殫控告耶叔亞大司祭]以後上主使我看見大司祭耶叔亞,站在上主的使者面前,同時撒殫站在耶叔亞右邊控告他。
Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki.
2 上主的使者對撒殫說:「惟願上主責斥你,撒殫! 惟願揀選耶路撒冷的上主責斥你。這不是由火中抽出來的一根木柴嗎﹖﹖」
Bwana akamwambia Shetani, “Bwana akukemee Shetani! Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?”
3 那時耶叔亞身穿污穢的衣服,站在使者的面前。
Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika.
4 使者就吩咐那些立在他面前的說:「脫去他身上污穢的衣服! 」以後向他說:「看,我已脫去了你的罪過,給你穿上華麗的禮服。」
Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.” Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.”
5 隨後接著吩咐說:「在他頭上纏上一條潔淨的頭巾! 」他們就在他頭上纏上了一條潔淨的頭巾,給他穿上了潔淨的禮服。那時,上主的使者,站在旁邊。
Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa Bwana akiwa amesimama karibu.
6 上主的使者便勸耶叔亞說:「
Malaika wa Bwana akamwamuru Yoshua:
7 萬軍的上主這樣說:如果你遵行我的道路,謹守我的法令,你便可以管理我的家,看守我的庭院;我必要使你在這些等立者中,自由出入。」
“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.
8 所以,大司祭耶叔亞,你且聽著:你和坐在你面前的同伴都是作預兆的人。攪,我必要使我的僕人「苖芽」生出。
“‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.
9 看,這是我在耶叔亞面前安置的石頭,在這惟一的石頭上有七隻眼睛;看! 我要親自在石上刻上題名──萬軍上主的斷語──並且要在那一天除去地上的罪過。
Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.
10 在那一天──萬軍上主的斷語──你們必要互相邀請自己的鄰里,到葡萄樹和無花果樹下。
“‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

< 撒迦利亞書 3 >