< 詩篇 77 >
1 阿撒夫的詩歌,交與樂官耶杜通。 我呼號,我的呼聲上達天主前,我向天主高呼,求他俯聽矜憐。
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu. Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie.
2 我在患難之日,尋求上主,雖整夜伸手,亦不覺辛苦,我的心靈且不接受安撫。
Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana, usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka na nafsi yangu ilikataa kufarijika.
3 我一懷念天主,即咨嗟哀歎,我一沉思考慮,即心灰意懶。
Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni; nikatafakari, roho yangu ikadhoofika.
4 您使我的眼睛徹夜不眠,我實煩燥難安,苦不堪言。
Ulizuia macho yangu kufumba; nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema.
Nilitafakari juu ya siku zilizopita, miaka mingi iliyopita,
nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku. Moyo wangu ulitafakari na roho yangu ikauliza:
“Je, Bwana atakataa milele? Je, hatatenda mema tena?
Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele? Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?
Je, Mungu amesahau kuwa na huruma? Je, katika hasira amezuia huruma yake?”
10 因此我說:這是我的苦難:至高者的右手已經改變。
Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.”
11 我現今追念上主的作為,回想您往昔所行的奇蹟;
Nitayakumbuka matendo ya Bwana; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.
12 沉思您的一切所作所為,更要默想您的一切異事。
Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu.
13 天主,您的行徑完全在於聖化,何神像我們的天主如此偉大?
Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?
14 只有您是施行奇蹟的天主!在萬民中彰顯了您的威武。
Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.
15 您以臂力拯救了您的人民,就是雅各伯和若瑟的子孫。
Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu.
16 大水一旦看見您,天主,大水一見您就都恐怖,連深淵汪洋也都顫抖。
Maji yalikuona, Ee Mungu, maji yalikuona yakakimbia, vilindi vilitetemeka.
Mawingu yalimwaga maji, mbingu zikatoa ngurumo kwa radi, mishale yako ikametameta huku na huko.
18 您的雷霆在旋風中發響,閃電也將整個世界照亮,大地驚慌失措而又搖盪。
Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli, umeme wako wa radi ukaangaza dunia, nchi ikatetemeka na kutikisika.
19 您的道路雖然經過海底,您的途徑雖然穿越大水,卻沒有顯露出您的足跡。
Njia yako ilipita baharini, mapito yako kwenye maji makuu, ingawa nyayo zako hazikuonekana.
20 您曾藉著梅瑟和亞郎的手掌,領導您的子民有如領導群羊。
Uliongoza watu wako kama kundi kwa mkono wa Mose na Aroni.