< 詩篇 7 >
1 【苦中投奔於主】 達味有感於本雅明族人的話,向上主唱流離之歌。 上主,我的天主!我一心投奔你;求你助我逃脫一切追逐我的人,求你救拔我;
Yahweh Mungu wangu, kwako napata kimbilio! Uninusuru na hao wote wanikimbizao, na uniokoe.
Vinginevyo, watanipura kama simba, na kunitawanya viapande vipande na asiwepo mtu wa kuweza kunirudisha katika usalama.
3 上主!如果我真做了這事,我主!在我手中就真有罪!
Yawheh Mungu wangu, Sijawahi kufanya kile maadui zangu wanacho sema nilifanya; sina hatia katika mikono yangu.
Sijawahi kumkosea mtu yeyote aliye na amani na mimi, au kumdhuru kipumbavu yeyote aliye kinyume na mimi.
5 就讓敵人追逐我,擒獲我,把我的性命踐踏在污地,將我的光榮歸諸於泥灰。
Ikiwa sisemi ukweli basi umruhusu adui yangu kuyaingilia maisha yangu na kuyaharibu; na umuache aukanyage mwili wangu ulio hai kwenye aridhi na kuuacha umelala kwa aibu mavumbini. (Selah)
6 上主,求你震怒奮起,前來克制我仇的暴慢。我的天主,求你醒起助我,施行你定的斷案。
Inuka, Yahweh, katika hasira yako; simama kinyume na hasira kali ya adui zangu; amka kwa ajili yangu na ubebe amri zako ambazo wewe umeamuru kwa ajili yao.
Mataifa yote yamekuzunguka; uwatawale kutoka mbinguni.
8 上主,萬民的審判者! 上主,請照我的正義,請按我的無罪,護衛我的權利。
Yahweh, uwahukumu mataifa; uwaonyeshe kuwa sina hatia, Yahweh, kwa sababu mimi ni mwenye haki na sina hatia, Ewe uliye juu.
9 公義的天主! 惟你洞察肺腑和人心,願惡人的毒害停止,求你堅固義人!
Matendo ya waovu na yafike mwisho, bali uanzishe watu wenye haki, Mungu mwenye haki, wewe ambaye unapima mioyo na fahamu.
Ngao yangu inatoka kwa Mungu, yule anaye okoa moyo wa mwenye haki.
Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu anaye chukizwa na waovu kila siku.
Ikiwa kuna mtu hatubu, Mungu atanoa upanga wake na ata andaa upinde wake kwa ajili ya vita.
13 那只是為自己預備死亡的武器,為自己製造帶火的箭矢。
Ana jiandaa kutumia siraha kupambana naye; anatengeneza mishale yake kuwa ya moto.
Fikiria kuhusu huyo ambaye ana ujauzito wa maovu, mwenye mimba ya mipango ya uharibifu, anaye zaa sumu ya uharibifu.
Yeye huchimba shimo na kuliacha wazi kisha baadaye hudumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.
16 他的兇惡必反轉到自己頭上,他的橫暴必降落在自己的頂上。
Mipango yake mwenyewe ya uharibifu hugeukia kichwa chake mwenyewe, kwa kuwa vurugu zake mwenyewe humshukia kichwani pake.
Kwa haki yako Mungu nitakushukuru; nitaimba sifa kwa Mungu aliye juu.