< 詩篇 140 >

1 上主,求您救拔我脫離兇惡的人; 上主,求您保護我脫離強暴的人!
Yahwe, uniokoe dhidi ya waovu; unikinge dhidi ya watu wenye vurugu.
2 他們心中策劃惡謀,他們終日挑撥爭鬥;
Wao wanapanga uovu mioyoni mwao; wanasababisha mapigano kila siku.
3 他們磨快自己的舌尖,有如蛇蝮,他們的雙脣的下面,含有蛇毒。 (休止)
Ndimi zao zinajeruhi kama nyoka; sumu ya fira imo midomoni mwao. (Selah)
4 上主,求您拯救我脫離兇惡的人;上主,求您保護我擺脫強暴的人,因他們企圖要我腳步滑倒。
Ee Yahwe, unilinde dhidi ya mikono ya waovu; unikinge na vurugu za watu wanaopanga kuniangusha.
5 驕傲人給我暗暗設網羅,張起繩索作為圈套,設下陷井等我路過。 (休止)
Wenye majivuno wameweka mtego kwa ajili yangu; wameeneza nyavu; wameweka kitanzi kwa ajili yangu. (Selah)
6 我求上主說:您是我的天主;上主,求您聽我哀禱的苦訴!
Nilimwambia Yahwe, “Wewe ni Mungu wangu; usikie kilio changu unihurumie.”
7 上主天主,您是我有力的救助,在作戰時,請您掩護我的頭顱。
Ee Yahwe, Bwana wangu, wewe ni mwenye nguvu uwezaye kuniokoa; hunifunika ngao kichwa changu siku ya vita.
8 上主,求您不要順隨惡人的奢欲;上主,請不要完成他們的計謀。 (休止)
Ee Yahwe, usiyatimize matakwa ya waovu; usiruhusu njama zao kufanikiwa. (Selah)
9 願那些顯露頭而圍困我的人,出於他們口脣的詛咒,反歸己身。
Wale wanao nizunguka huinua vichwa vyao; madhara ya midomo yao wenyewe na yawafunike.
10 願火降落在他們的身上,將他們拋入深坑免再高昂。
Makaa ya moto na yawaangukie; uwatupe motoni, kwenye shimo refu, wasiweze kuinuka tena.
11 搬弄是非的人,不得在世久存,災禍會突然使強暴的人被擒。
Watu wenye ndimi na wasifanywe salama juu ya nchi; na uovu umuwinde kumpiga mtu mwenye vurugu mpaka afe.
12 我確知上主必為受壓迫的人伸冤,也必為貧窮的人主持正義的判斷。
Ninajua kuwa Yahwe atahukumu kwa haki walioteswa, na kuwa atawapa haki wahitaji.
13 義人必定將您的聖名頌讚,善人必定居住在您的面前。
Hakika watu wenye haki watalishukuru jina lako; watu wanyoofu wataishi uweponi mwako.

< 詩篇 140 >