< 俄巴底亞書 1 >
1 亞北底亞神視]吾主上主關於厄東這樣說:我從上主聽到了一個消息,有一位傳令員已被派往萬民那裏說:「起來! 我們起來向她進攻! 」
Maono ya Obadia. Bwana MUNGU asema hivi juu ya Edomu Tumesikia habari kutoka kwa Bwana, na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, akisema, Inukeni! Tuinuke dhidi yake kwa vita!”
Tazama, nitawafanya wadogo kati ya mataifa, mutadharauliwa sana.
3 你心中的驕傲欺騙了你:你住在磐石裂縫中,安居高處,心中說:「誰能我跌在地上﹖」
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya wewe, wewe ambaye unishi katika makaburi ya miamba, katika nyumba yako ya juu; asemaye moyoni mwako, 'Ni nani atakayenishusha mimi chini?'
4 既使你高棲如鷹,既便你將巢穴安置星辰上,我也要從那裏把你推下──上主的斷語──
Ingawa unasimama juu kama tai na ingawa kiota chako huwekwa kati ya nyota, nitakushusha chini kutoka huko, asema Yahweh.
5 如果盜賊,或夜間的強盜來到你那裏,他們豈不要偷個夠嗎﹖如果收葡萄的來到你那裏,豈不只給氮留下些殘粒嗎﹖你將來也是如此荒涼!
Kama wezi walikuja kwako, ikiwa wanyang'anyi wangekujilia usiku (jinsi ungekatilwa mbali!), Wasingeweza kuiba vya kuwatosha? Ikiwa wakusanya zabibu wangekujilia, wasingeacha mavuno?
6 厄撒烏怎樣被人搜過了,她的寶藏怎樣被人探索了!
Jinsi Esau amekwisha kupigwa, na hazina zake zilizofichwa zimewekwa nje!
7 與你聯盟的人,愚弄了你,將你驅至邊境;與你友好的人,克服了你;與你共食人,給你暗設了陷阱,而你竟一點也沒有理會。
Watu wote wa ushirikiano wako watakupeleka katika njiani ya hadi mpakani. Watu waliokuwa na amani pamoja nawe wamekudanganya, na kukushinda. Wale wanaokula mkate wako wameweka mtego chini yako. Hakuna uelewa ndani yake.
8 在那一天──上主的斷語──我豈能不撲滅厄東的智者,掃除厄撒烏山上的明哲﹖
Je! Sikuweza siku hiyo, asema Bwana, kuwaangamiza watu wenye hekima kutoka Edomu na kuelewa kutoka mlima wa Esau?
9 特曼,你的勇士必驚惶失措,至使厄撒烏山上的人盡遭滅亡。你既然好殺,
Mashujaa wako watafadhaika, Temani, ili kila mtu akatiliwe mbali kutoka mlima wa Esau kwa kuuawa.
10 傷害了你的兄弟雅各伯,你必蒙受羞辱,永遭滅亡:
Kwa sababu ya ukatili uliofanywa kwa ndugu yako Yakobo, utafunikwa na aibu, nawe utakatiliwa mbali milele.
11 因為當外邦人擄掠他財寶的那一天,蠻族來到了他的城門下,對耶路撒冷拈鬮時,你也置身其間,好像他們中的一個。
Siku ile ulikuwa umesimama, siku wageni walichukua mali zake, na waliokuwa wageni katika malango yake, na kupiga kura kwa Yerusalemu, wewe ulikuwa kama mmoja wao.
12 你兄弟遭難的日子,你不應旁觀;猶大子民滅亡的那天,你也不應引以為樂;在患難的日子上,你也不應大言不慚。
Lakini usifurahi siku ya ndugu yako, siku ya msiba wake, wala usifurahi juu ya watu wa Yuda siku ya uharibifu wao; msijisifu siku ya dhiki yao.
13 在我的的百姓遭的時日,你不應闖進他們的門;在他遭難的時日,你更不應伸手劫掠他的財物。
Usiingie mlango wa watu wangu siku ya msiba wao; usifurahi juu ya taabu yao siku ya msiba wao, wala msipotee utajiri wao siku ya uharibifu wao.
14 你不應站在交叉路口,截殺他的難民;在患難之日,你不應交出他的劫後餘生。
Usisimama kwenye njia panda, ili kuwakatilia mbali wakimbizi wake na usiwatoe waathirika wake katika siku ya dhiki.
15 因為上主的日子已臨近萬民,人必按你所作的,照樣對待你;你的行為必歸於你的頭上。
Kwa maana siku ya Bwana iko karibu na mataifa yote. Kama ulivyofanya, itafanyika kwako; matendo yako yatarudi juu ya kichwa chako mwenyewe.
16 正如你們曾在我的聖山上痛飲過,萬民也要不斷痛飲:他們要痛飲,要飲醉,而終歸消滅。
Kwa vile mlivyokunywa katika mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote yatakavyo kunywa daima. Watakunywa na kumeza na itakuwa kana kwamba hawakuwepo kabisa.
17 在熙雍山上必有救援,熙雍將是神聖的;並且雅各伯家要侵佔那侵佔過他們的人。
Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwa na wale waliookoka na watakuwa watakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki miliki zao.
18 雅各伯家將成為火,若瑟家將成為火焰,厄撒烏家卻要成為草楷;雅各伯家和若瑟家要焚燒吞滅他們;厄撒烏家必沒有一個餘生,因為上主說了。
Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu ni mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaunguza, na kuwateketeza. Hakutakuwa na waathirika kwa nyumba ya Esau, kwa kuwa Bwana amesema.
19 他們要佔領南方,厄撒烏的山頂與培肋舍特的平原,要佔領厄弗辣因地和撒馬黎雅地以及阿孟子民的基肋阿得。
Wote kutoka Negebu watamiliki mlima wa Esau na wale wa Shepela watamiliki nchi ya Wafilisti. Wao wataimiliki nchi ya Efraimu na nchi ya Samaria; na Benyamini atamiliki Gileadi.
20 這支充軍在外的叵子民的軍旅,要佔領客納罕人的土地,直到匝爾法特;流亡在色法辣特的耶路撒冷人,要佔領南方的城邑。
Wahamiaji wa jeshi hili la watu wa Israeli watamiliki ardhi ya Kanaani mpaka Sarepta. Wahamiaji wa Yerusalemu, waliopo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu.
21 那時,獲救者必上熙雍山,統治厄撒烏王;王權必歸於上主。
Waokoaji watakwenda hadi juu ya Mlima Sayuni kutawala nchi ya vilima ya Esau, na ufalme utakuwa wa Bwana.