< 民數記 35 >

1 上主在耶里哥對面,約但河邊,摩阿布曠野內,訓示梅瑟說:「
BWANA akanena na Musa kwenye nyanda za Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko akasema,
2 你命令以色列子民,應由他們分得的產業內,指定一些城給肋未人居住,將城四周的牧場,也分給肋未人。
“Waamuru watu wa Israeli kutoa sehemu ya urithi wa ardhi yao kwa Walawi. Watawapa miji ya kuishi ndani yake na eneo la malisho kuzunguka miji hiyo.
3 這些城歸他們居住,城郊的牧場為牧放他們所有的牛羊和一切牲畜。
Walawi watakuwa na miji hiyo ya kuishi. Eneo la malisho litakuwa kwa ajili ya ng'ombe zao, kondoo zao, na wanyama wao wote.
4 你們劃給肋未城郊的牧場,應由城牆起,周圍向外伸展至二千肘,
Hayo malisho yatakayozunguka miji hiyo ambayo mtawapa Walawi yataanzia kwenye maboma kwa ukubwa wa “mita 457” kila upande.
5 即由城外向東方量二千肘,向南方量二千肘,向西方量二千肘,向北方量二千肘,城在中央;這些土地為作他們城郊的牧場。
Utapima dhiraa elfu mbili kutoka nje ya mji kuelekea mashariki, na dhiraa elfu mbili kuelekea kusini, na dhiraa elfu mbili kuelekea upande wa magharibi, na dhiraa elfu mbilii kuelekea upandewa kaskazini. Haya yatakuwa maeneo ya malisho yao. Miji itakuwa katikati.
6 分給肋未人的城中,應指定六座為避難城,殺人者可逃入城中。此外還應給他們四十二座城。
Katika hiyo miji sita mtakayowapatia Walawi itatumika kama miji ya ukimbizi. Mtatoa maeneo haya ili kama mtu ameua mtu apate mahali pa kukimbilia. Pia mtatoa miji mingine arobaini na mbli.
7 這樣,劃給肋未人的城,共計四十八座,連城郊的牧場在內。
Jumla ya miji ambyo mtawapa Walawi itakuwa arobaini na nane. Mtawapa hiyo miji pamoja na maeneo yao ya malisho.
8 當你們由以色列子民的產業中,劃分給肋未人城邑時,由大支派應多取,由小支派應少取;每支派應依照自己分得的產業,將城邑劃給肋未人。」
Zile kabila kubwa za watu wa Israeli, kabila ambalo lina ardhi zaidi, watatoa ardhi zaidi. Makabila madogo madogo watatoa miji michache. Kila kabila lazima watoe kwa ajili ya Walawi kwa kufuata mgawo waliopata.”
9 上主訓示梅瑟說:「
Kisha BWANA akanena na Musa akamwambia,
10 你告訴以色列子民說:幾時你們過約但河進入了客納罕地,
“Sema na wana wa Israeli na uwaambie, 'Mtakapovuka Yorodani kuingia Kanaani,
11 應選定幾座城作你們的避難城,凡誤殺人的,可逃到那裡。
Kisha mchague miji itakayotumika kama miji ya ukimbizi kwa, ajili yenu, mahali ambapo mtu aliyeua mtu pasipo kukusudia anaweza kukimbilia.
12 這些城可作為你們脫免復仇者的避難所,好使殺人者不致在未立於會眾前受審判以前,便遭人殺害。
Hii miji itakuwa kwenu miji ya ukimbizi kwa mtu anayetaka kulipa kisasi. ili kwamba mtuhumiwa asije akauawa bila kwanza kusikilizwa na jamii.
13 你們應指定六座城作為你們的避難城。
Mtachagua miji sita kuwa miji ya ukimbizi.
14 在約但河東指定三座,在客納罕地指定三座,作為避難城。
Mtatoa miji mitatu kule ng'ambo ya Yorodani na miji mitatu huko Kanaani. Itakuwa miji ya ukimbizi.
15 這六座城為以色列子民和外方人,以及住在你們中間的人,作為避難所;凡誤殺人的,都可逃到那裡去。
Kwa ajili ya watu wa Israeli, wageni, kwa, yeyote anayeishi kati yenu, hii miji sita itatumika kama miji ya ukimbizi kwa mtu yeyote atakayeua mtu bila kukusudia anaweza kukimbila.
16 人若用鐵器打人,將人打死,他就是兇手,兇手應處死刑。
Lakini kama mtuhumiwa amempiga mtu na chombo cha chuma, na huyo mtu akafa, basi kwa hakika yule mtuhumiwa ni muuaji. Kwa hiyo anatakiwa kuuawa.
17 人若用手中可砸死人的石頭打人,將人砸死;他就是兇手,兇手應處死刑。
Kama yule mtuhumiwa amempiga mtu kwa jiwe mkonono mwake ambalo linaweza kumwua mtu, na kama yule mtu atakufa, basi hakika huyo mtuhumiwa ni mwuaji. Kwa hakika anatakiwa kuuawa.
18 或者人若用手中可打死人的木器打人,將人打死,他就是兇手,兇手應處死刑。
Kama mtuhumiwa amempiga mtu kwa silaha ya mti ambayo inaweza kuua mtu na kama huyo mtu atakufa, basi kwa hakika huyo mtuhumiwa ni mwuaji. kwa hakika huyo anataikwa kuuawa.
19 報血仇的,可將兇手殺死;幾時遇見他,可將他殺死。
Mwenye kulipa kisasi cha damu ndiye atakayemwua mwuaji. atkapokutana naye, anaweza kumwua.
20 人若因懷恨撞倒了人,或故意拋物打人,致使那人死了;
Lakini kama yule mtuhumiwa atamshinda mtu yeyote yule anayemchukia au kama atamtupia kitu, wakati akimvizia, kiasi kwamba huyo mtu akafa,
21 或者因仇恨用手打人,將人打死;打人的應處死刑,因他是兇手;報血仇的人,幾時遇著兇手,可將他殺死。
au kama atampiga ngumi kwa chuki na mtu huyo akafa, ndipo yule mtuhumiwa aliyempiga hakika atauawa. Yeye ni mwuaji. Yule mlipa kisasi cha damu anaweza kumwua muuaji pale atakapokutana naye.
22 但是,若人並無怨仇,偶然撞倒人,或無意中拋物傷人,
Lakini kama mtuhumiwa atampiga mtu ghafla bila kuwa na chuki hapo awali, au kama atamtupia kitu ambacho kitampiga mtu bila kumvizia
23 或因沒有看見,使任何能打死人的石頭落在人身上,致使那人死了,彼此並沒有仇恨,也沒有意思害人,
au kama atatupa jiwe amabalo linaweza kumwua mtu bila kumwona, basi huyo mtu hakua adui yake, hakukusudia kumwumiza huyo mtu. Basi hiki ndicho kitachofanywa kama mtu huyo atakufa.
24 對這樣的案件,應在打死人的和要報血仇者之間進行裁判。
Kwa tatizo la jinsi hiyo, Watu wataamua kati ya mlipa kisasi na mtuhumiwa kwa kufuata taratibu zifuatazo.
25 會眾要把殺人者由報血仇者手內救出,使他回到他曾逃入的避難城內,叫他住在那裡,直到傅過聖油的大司祭去逝。
Watu watamwokoa mtuhumiwa kutoka kwenye nguvu za mlipa kisasi cha damu. Watu watamrudisha mtuhumiwa katika mji wa ukimbizi ambao hapo awali alikimbilia. Ataishi pale mpaka yule kuhani anayetumikia atakapokufa, ambaye alipakwa mafuta matakatifu.
26 但殺人者如果離開他逃入避難城的邊界以外,
Lakini kama yule mtuhumiwa muda fulani ataenda nje ya mipaka ya mji a ukimbizi ambao alikimbilia,
27 報血仇者在避難城邊界以外遇見了他,將死殺人者殺死,他並不犯流向的罪,
na kama yule mlipa kisasi cha damu atamwona nje ya mipaka ya mji wake wa ukimbizi, kama atamwua huyo mtuhumiwa, mlipa kisasi cha damu hatakuwa na hatia ya mauaji hayo.
28 因為那該留在避難城內,直到大司祭去世;大司祭死後,殺人者方可回到屬自己產業的地方:
Hii ni kwa sababu yule mtuhumiwa alitakiwa kubaki katika mji wake wa ukimbizi mpaka kuhani mkuu atakapokufa. Baada ya kifo cha kuhani mkuu, yule mtuhumiwa atarejea kwenye nchi yake ambako kuna mali yake.
29 這是你們世世代代,在你們任何住處,應遵守的法令。
Hizi amri zitakuwa maagizo kwenu kwa kizazi chote mahali kote mnakoishi.
30 凡殺人的案件,應依據幾個證人的口供,才可以處決殺人犯;惟獨一人作證,不足以以人宣判死刑。
Yeyote amwuaye mtu, mwuaji atauawa, kama neno la ushahidi litakavyotolewa. Lakini ushahidi wa mtu mmoja unaweza usitoshe kusababisha mtu kuuawa.
31 對於被判死刑的殺人犯,你們不可取贖命金,,因為他應該死
Pia, msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa mwuaji ambaye ana hatia ya mauti. Kwa hakika lazima auawe.
32 同樣,你們對逃入避難城的人,亦不可取贖金,准他在大司祭死以前回到本鄉居住。
Na msipokee fidia ya mtu aliyekimbilia kwenye miji ya ukimbizi. Msimruhusu kwa namna yeyote kurudi kwenye mali zake mpaka pale kuhani mkuu atakapokufa.
33 你們不可玷污你們所居之地,因為血能玷污地;在那裏流了血,除非那殺人者的血,為那地沒有其他取潔的方法。
Msiiharibu nchi mnayokaa kwa namna hii, kwa kuwa damu ya mwuaji huharibu nchi. Hakuna sadaka ya upatanisho inayoweza kufanywa kwa nchi pale damu inapomwagika juu yake, isipokuwa kwa damu ya mtu aliyeimwaga.
34 你們不可褻瀆你們所居之地,這地也是我居留之地,因為我上主是住在以色列子民中間」。
Kwa hiyo msiinajisi nchi mnayoishi kwa sababu Mimi ninaishi ndani yake. Mimi BWANA huishi kati ya watu wa Israeli.”'

< 民數記 35 >