< 民數記 33 >
1 以下是以色列子民在梅瑟和亞郎指揮下,分隊出離埃及國後所行的路程。
Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni.
2 梅瑟記錄了他們遵上主的命啟營的出發點。以下是他們依次出發的行程:
Kwa agizo la Bwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:
3 他們於正月十五日由辣默色斯起程,即在逾越節第二日,以色列子民大膽地、當著眾埃及人的面出走了,
Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote,
4 其時埃及人正在埋葬上主在他們中所擊殺的一切長子;上主也懲罰了他們的神祇。
waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Bwana alikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwa Bwana alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.
Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.
Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
7 由厄堂起程,轉向巴耳責豐的丕哈希洛特,在米革多耳對面紮營。
Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
8 由丕哈希洛特起程,由海中經過進入曠野,在厄堂曠野中行了三天的路,然後在瑪辣紮營。
Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.
9 由瑪辣起程,來到厄林。在厄林有十二水泉和七十株棕櫚樹,就在那裡紮營。
Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.
Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.
Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.
Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.
Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.
14 由阿路士起程,在勒非丁紮營;民眾在這裡沒有水喝。
Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.
Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.
Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.
Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.
Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.
Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.
Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.
Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.
Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.
Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.
Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.
Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.
Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.
Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.
Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.
Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.
Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.
Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.
Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.
Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.
Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.
Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.
36 由厄茲雍革貝爾起程,在親曠野,即卡德士紮營。
Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.
37 由卡德士起程,在位於厄東地邊界上的曷爾山下紮營。
Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu.
38 亞郎大司祭依上主的命,上了曷爾山,死在那裡,時在以色列子民出埃及國後四十年五月初一日。
Kwa amri ya Bwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri.
Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.
40 其時住在客納罕南部的客納罕人王阿辣得聽說以色列子民來了。
Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.
Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.
Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.
Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.
44 由敖波特起程,在位於摩阿布邊境的依因阿巴陵紮營。
Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.
Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.
Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.
47 由阿耳孟狄貝拉塔因起程,在乃波前面的阿巴陵山地內紮營。
Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.
48 由阿巴陵山地起程,在耶里哥對面,約但河邊,摩阿布曠野紮營;
Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.
49 他們在摩阿布曠野裡,沿著約但河邊紮營,由貝特耶史摩特直到阿貝耳史廷。
Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.
50 在耶里哥對面,約但河邊,摩阿布曠野內,上主訓示梅瑟說:「
Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko, Bwana akamwambia Mose,
51 你告訴以色列子民說:你們幾時過了約但,進入客納罕地,
“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani,
52 應由你們面前驅逐當地所有的居民,應毀壞他們的一切偶像,應打碎他們的一切鑄像,應鏟除他們的一切丘壇。
wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada.
53 你們要佔領那地方,住在那裡,因為我已將那裡給了你們叫你們佔有。
Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki.
54 你們要按支派抽籤分配那地方:人數多的多給,人數少的少給。誰的籤落在那裡,那裡就屬於他。你們依照宗祖支派分配你們的產業。
Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.
55 但如果你們不把當地的居民由你們面前驅逐,那留下的居民,必要成為你們的眼中刺,腰間針,在你們住的地方內迫害你們;
“‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.
56 並且我打算了怎樣對待他們,也要怎樣對待你們。」
Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’”