< 民數記 32 >
1 勒烏本的子孫和加得的子孫,擁有很多的家畜;他們一見雅則爾地方和基肋阿得地方,是適於畜牧的區域,
Sasa wana wa uzao wa Reubeni na wa Gadi walikuwa na idadi kubwa ya wanyama. Waliiona ardhi ya Jazeri na Gileadi, kuwa ni ardhi nzuri kwa mifugo.
2 便前來對梅瑟和厄肋阿匝爾大司祭及會眾的首領說:「
Kwa hiyo wana wa Gadi na wa Reubeni wakaja kumwambia Musa, na Eliazari kuhani, na viongozi wa watu. Wakasema,
3 阿塔洛特、狄朋、雅則爾、尼默辣、赫市朋、厄肋阿肋、色班、乃波和貝紅,
“Hii ndiyo orodha ya maeneo ambayo tumeyatembelea: Diboni, Jazeri, Nimraha, Heshibonni, Ellealehi, Sebamu, Nebo, na Beoni.
4 這些地方是上主為以色列會眾所征服的,是適於畜牧的地方,而你的僕人們正有牛羊。」
Haya ni maeneo ambayo BWANA aliyachukua mbele ya watu wa Israeli, na maeneo mazuri kwa ajili ya mifugo. Sisi watumishi wako tuna mifugo mingi sana.
5 他們又說:「若是我們在你眼中獲得寵幸,希望你將這地方賜給你的僕人們作產業,不必叫我們過約但河。」
Wakasema kuwa, “Kama tutapata kibali mbele ya macho yako, tunaomba ardhi hii tupewe, sisi watumishi wako, kuwa urithi. Usituvushe ng'ambo ya Yorodani.”
6 梅瑟回答加得的子孫和勒烏本的子孫說:「怎麼! 你們的兄弟去打仗,你們卻要住在這裡﹖
Musa akawajibu wale wana wa auzao wa Gadi na Reubeni, “Je, mngependa ndugu zenu waende vitani wakati ninyi mkikaa hapa?
7 為什麼你們要叫以色列的子民喪氣,使他們不敢進入上主賜給他們的土地﹖
Kwa nini kuwafish moyo watu wa Israeli wasivuke kwenda kwenye nchi ambayo BWANA amewapa?
8 當我由卡德士巴爾乃亞派遣你們的祖先去窺探這地時,他們也這樣做過。
Baba zenu walifanya hivyo nilipowatuma kutoka Kadeshi Banea kwenda kuipeleleza ile nchi.
9 他們上到厄市苛耳山谷,窺探了那地方,回來就使以色列子民喪了氣,致使他們再不願進入上主賜給他們的土地。
Walienda mpaka kwenye bonde la Eskoli. Waliiona ile ardhi kisha wakawafisha moyo watu wa Israeli kwa hiyo wakagoma kuingia kwenye nchi ambayo BWANA alikuwa amewapa.
Siku hiyo hasira ya BWANA iliwaka. Akaapa akisema,
11 凡由埃及出來過了二十歲的人,不得看見我誓許給亞巴郎、依撒格和雅各伯的土地,因為他們沒有一心一意地隨從我;
'Kwa hakika hakuna mtu aliyetoka Misri, kuanzia wa umri wa miaka ishirini na zaidi ambao wataiona nchi ambao niliwaapia Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, kwa sababu hawakunifuata mimi kwa ukamilifu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni.
12 只有刻納次人耶孚乃的兒子加肋布和農的兒子若蘇厄除外,因為他們一心一意地隨從了上主。』
Ni Kalebu na Joshua tu ndio walionifuata kwa ukamilifu.'
13 因為上主對以色列發了怒,遂使他們在曠野中漂泊了四十年,直到在上主眼前作惡的那一世代完全死盡。
Kwa hiyo hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israei. Akawafanya wazunguke zunguke jangwani kwa miaka arobaini mpaka kile kizazi kilichofanya maovu mbele za macho yake kilipoteketea.
14 現在,看,你們這些罪人的苗裔,竟起來替代你們先人,再增加上主對以色列的忿怒!
Tazama, mmetokea katika nafasi za baba zenu, kama watu wengine wenye dhambi zaidi, ili kuongeza hasira ya BWANA kwa Israeli.
15 如果你們背離了他,他再把民眾拋在曠野裡;這樣,你們就要使這整個民族毀滅了。」
Kama hamtamfuata, ataiacha Israeli jangwani na mtakuwa mmewateketeza watu hawa wote.
16 他們遂上前來,對他說:「我們願在這裡為我們的牛羊築圈,為我們的家眷建城。
Kwa hiyo wakaja karibu na Musa wakamwambia, “Turuhusu tujenga hapa uzio kwa ajili ya ng'ombe zetu na miji hapa kwa ajili ya familia zetu.
17 但我們必武裝起來,在以色列子民前頭上陣,直到我們領他們進入了自己的地方;至於我們的家眷,為預防本地的居民,應叫他們安居在堅固的城內。
Hata hivyo, sisi wenyewe tutajipanga kijeshi kwenda na jeshi la Israeli mpaka tumewaongoza kupata maeneo yao. Lakini familia zetu zitakuwa kwenye miji ya maboma kwa ssbabu ya watu wengine ambao bado wanaishi katika nchi hii.
18 不到以色列子民各個都佔有了產業,我們決不回家。
Hatutarudi kwenye familia zetu mpaka kila mmoja watu wa Israeli apate urithi wake.
19 我們既然在約但河東得到了產業,在約但河西,就不再同他們分產業了。」
Sisi hatutachukua urithi wa ardhi pamoja nao kule ng'ambo ya Yorodani, kwa sababu urithi wetu uko hapa upande wa mashariki mwa Yorodani.”
20 梅瑟答覆他們說:「若是你們這樣做,若是你們武裝起來,在上主面前作戰;
Kwa hiyo Musa akawajibu, “Kama mtafanya mnachokisema, kama mtajipanga wenyewe mbele za BWANA kwenda vitani,
21 若是你們個個都武裝著在上主面前過約但河,直到他將自己的敵人驅散,
basi kila mmoja wa wanajeshi wenu lazima avuke Yorodani mbele za BWANA, mpaka atakapowafukuza maadui zake kutoka mbele zake
22 直到上主把那地征服以後,你們纔回家,你們對上主,對以色列就算無罪。那麼,這地照上主的允許,歸你們作為產業。
na nchi itawaliwe na Israeli mbele zake. Kisha mtaweza kurudi. Hamtakuwa na hatia mbele za BWANA na mbele ya Israeli. Hii nchi itakuwa miliki yenu mbele za BWANA.
23 但是,如果你們不這樣去做,你們必獲罪於上主,要知道你們必自招罪罰。
Bali kama hamtafnya hivyo, tazama, mtakuwa mmefanya dhambi mbele ya BWANA. Mwe na hakika kuwa dhambi yenu itaonekana
24 你們可為家眷建城,為牛羊築圈;但是你們口頭所許的,卻必要實踐。」
wazi. Jengeni miji kwa ajili ya familia zenu na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; kisha fanyeni kile mlichokisema.”
25 加得的子孫和勒烏本的子孫回答梅瑟說:「你僕人們必照我主所吩咐的去做。
Wale wana wa Gadi na Reubeni wakamwambia Musa, wakisema, “Watumishi wako wtafanya kama vile wewe, bwana wetu, unavyotuamuru.
26 我們的孩童、婦女、牛羊和一切牲畜,都留在這裡,留在基肋阿得的城裡;
Watoto wetu, wake zetu, makundi yetu, na wanyama wetu wote watakaa huko kwenye miji ya Gileadi.
27 至於你的僕人們,凡武裝起來的,都要過河,在上主面前上陣作戰,如我主所吩咐的。」
Hata hivyo, sisi watumishi wako, tutavuka kwenda ng'ambo mbele za BWANA kupigana, kila mtu ambaye yuko tayari kwa vita, kama vile wewe, bwana wetu, unavyosema.”
28 梅瑟遂為他們向大司祭厄肋阿匝爾、農的兒子若蘇厄,以及以色列子民各支派的家長下了指示,
Kwa hiyo Musa akawapa maelekezo yayowahusu kwa Eliazari kuhani, kwa Joshua mwana wa Nuni, na kwa viongozi wa koo kufuata jamaa zao katika makabila ya wana wa Israeli.
29 向他們說:「若是加得子孫和勒烏本子孫,都武裝起來與你們同過約但河,在上主面前作戰,在你們征服那地以後,就把基肋阿得地方給他們作為產業。
Musa akawaambia, “Kama uzao wa Reubeni na Gadi watavuka ng'ambo ya Yorodani pamoja nanyi, kila mwanamume anayetakiwa kuwa vitani mbele za BWANA, na kama nchi mtaitawala mbele zenu, ndipo mtakapowapa eneo la Gileadi kuwa miliki yao.
30 但是,如果他們不武裝起來同你們一起過河,就應在客納罕地與你們同分產業。」
Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa na silaha zao, basi mtawapa urithi wao katika nchi ya Kanaani.”
31 加得子孫和勒烏本子孫回答說:「凡上主關於你僕人所說的,我們必照做。
Kwas hiyo wana wa uzao wa Gadi na wa Reubeni wakamjibu wakisema, Kama vile BWANA alivyosema nasi, sisi watumwa wako, hiki ndicho tutakachokifanya.
32 我們必武裝起來在上主面前過河,往客納罕地去;但約但河東的地方應給我們作產業。」
Tutavuka tukiwa na silaha zetu mbele za BWANA kuingia katika nchi ya Kanaani, lakini urithi wetu utabaki utabaki upande huu wa Yorodani.”
33 梅瑟遂將阿摩黎人王息紅的國土和巴商王敖格的國土,那地域及其境內的城池,以及那地域四周的城池,都給了他們;給了加得的子孫、勒烏本的子孫和若瑟的兒子默納協半支派。
Kwa hiyo uzao wa Gadi na Reubeni, na pia nusu ya kabila la Manase mwana wa Yusufu, Musa akawapa ufalme wa Sihoni, mfalme wa Waamori, na wa Ogi, mafalme wa Bashani, Aliwapa hiyo nchi, na kuwagawia miji yake yote pamoja na mipaka yake, miji yote ya nchi inayowazunguka.
Wale wa uzao wa Gadi wakaijenga Diboni,
Atarothi, Aroeri, Atrothi, Jazeri, Jogbehaha, Bethi Nimraha,
36 貝特尼默辣和貝特哈蘭:這些都是堅固的城邑,並築有羊圈。
na Bethi Harani kuwa miji iliyo na maboma na mazizi ya kondoo wao.
37 勒烏本的子孫重建了赫市朋、厄肋阿肋、克黎雅塔因、
Wale wa uzao wa Reubeni wakaijenga Heshiboni. Elealehi, Kiriathaimu,
38 乃波、巴爾默紅──有些名字已改──和息貝瑪;他們給重建的城邑另取了別名。
Nebo, Baali Meoni - baadaye waliyabadili majina yao, na Sibimaha.
39 默納協的兒子瑪基爾的子孫去了基肋阿得,佔據了那地方,驅逐了那裡的阿摩黎人。
Wale wa uzao wa Machiri mwana wa Manase walienda Gileadi na kuutwaa kutoka kwa Waamori waliokuwa wakiishi humo.
40 梅瑟遂將基肋阿得給了默納協的兒子瑪基爾;他就在那裡住下了。
Kisha Musa akaitoa Gileadi kwa Machiri mwana wa Manase, na watu wake wakaishi humo.
41 默納協的兒子雅依爾去佔據了阿摩黎人的村落遂稱這些村落為哈沃特雅依爾。
Jairi mwana wa Manase alienda kuiteka miji yake na kuiita Havothi Jairi.
42 諾巴黑去佔據了刻納特及其屬鎮,給那地方起了自己的名字,叫諾巴黑。
Nobaha alienda kuitieka Kenathi na vijiji vyake, na akauita kwa jina lake Nobaha.