< 尼希米記 7 >
1 當城垣修好之後,我安了門扇,遂委派了守門者、歌詠者和肋未人。
Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa.
2 以後,我委派了我的兄弟哈納尼,和堡壘長哈納尼雅,管理耶路撒冷,因為哈納尼雅是一個可信賴、敬畏天主出眾的人。
Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine.
3 我命他們說:「耶路撒冷的門,不到太陽發暖不准開;太陽還未落時,就要關門上閂! 守衛當由耶路撒冷的居民中指派,各按自己的班次,各在自己的屋前守衛。」
Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”
4 那時城市寬闊廣大,但城中居民稀少,房舍還沒有建築。
Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu.
5 我的天主使我立意,召集有權勢的人、官長和民眾,要他們來登記。我發現了一冊初次由充軍歸來的人的族譜,上面有這樣的記載:
Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:
6 以下是由被擄充軍返回本省的子民的人中,當初被巴比倫王拿步高,擄往巴比倫去的人中,回了耶路撒冷和猶大,各本城的人。
Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
7 他們是同則魯巴貝耳、耶叔亞、乃赫米雅、色辣雅、阿米雅、納哈瑪尼、摩爾德開、彼耳商、米斯帕勒特、彼革外、勒洪和巴阿納,一起回來的。以色列民男子的數目如下:
wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana): Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:
11 帕哈特摩阿布的子孫,即耶叔亞和約阿布的子孫,二千八百一十八名;
wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,818
wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98
watu wa Bethlehemu na Netofa 188
watu wa Beth-Azmawethi 42
29 克黎雅特耶阿陵人、革非辣人和貝厄洛特人,共七百四十三名;
watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743
watu wa Betheli na Ai 123
wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 721
39 司祭:有耶達雅的子孫,即耶叔亞的家族,九百七十三名;
Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973
43 肋未人:曷達委雅的後裔,耶叔亞和卡德米耳的子孫,七十四名。
Walawi: wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia) 74
Waimbaji: wazao wa Asafu 148
45 門丁有沙隆的子孫,阿特爾的子孫,塔耳孟的子孫,阿谷布的子孫,哈提達的子孫,勺拜的子孫,共一百三十八名。
Mabawabu wa malango: wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 138
46 獻身者:有漆哈的子孫,哈穌法的子孫,塔巴敖特的子孫,
Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,
wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,
wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,
wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,
wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,
wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,
53 巴刻步克的子孫,哈谷法的子孫,哈爾胡爾的子孫,
wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54 巴茲里特的子孫,默希達的子孫,哈爾沙的子孫,
wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
55 巴爾科斯的子孫,息色辣的子孫,塔瑪赫的子孫,
wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
wazao wa Nesia na Hatifa.
57 撒羅滿的僕役的子孫:有索泰的子孫,索費勒特的子孫,培黎達的子孫,
Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,
wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
59 舍法提雅的子孫,哈提耳的子孫,頗革勒特責巴因的子孫和阿孟的子孫。
wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.
60 所有獻身者的子孫和撒羅滿的僕役的子孫,共計三百九十二名。
Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392
61 以下這些人,是由特耳默拉、特耳哈爾沙、革魯布、阿丹和依默爾上來,而不能說出自己的家族和族系,是否出自以色列的:
Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
62 德拉雅的子孫,托彼雅的子孫,和乃科達的子孫,共計六百四十二人。
wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 642
63 司祭中:有哈巴雅的子孫,哈科茲的子孫和巴爾齊來的子孫。巴爾齊來娶了基肋阿得人巴爾齊來的女兒為妻,也取了他的名字。
Na kutoka miongoni mwa makuhani: wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
64 他們查考登記的族譜,卻沒有找到自己的名字,所以他們由司祭中被革除了。
Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi.
65 省長指令他們,不准他們享用至聖之物,直到有位大司祭,帶著烏陵和突明出來解決。
Kwa hiyo, mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.
Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360;
67 僕婢七千三百三十七人在外;還有歌詠的男女二百五十四名。
tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245.
68 此外,還有駱駝四百三十五匹,驢六千七百二十匹。
Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245
69 有些族長捐獻了一千金「塔理克,」盤子五十個,司祭長衣五百三十件,作為基金。
ngamia 435 na punda 6,720.
70 另一些族長納了二萬金「塔理克,」二千二百銀「米乃,」作為建築的基金。
Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000 za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.
71 其餘名眾捐獻的,共計二萬金「塔理克,」二千銀「米乃,」司祭長衣六十七件。
Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu, na mane 2,200 za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
72 司祭、勒未人、門丁、歌詠者、獻身者和全以色列,各住在本城內。
Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.
Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe. Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,