< 路加福音 6 >

1 有一個安息日,耶穌經過麥田時,祂的門徒掐著麥穗,用手搓著吃。
Sasa ilitokea kwenye Sabato kwamba Yesu alikuwa akipita katika ya shamba la nafaka na wanafunzi wake walikuwa wakichuma masuke, wakayasuguasugua kati ya mikono yao wakala nafaka.
2 有幾個法利賽人說:「為什麼你們做安息日不准做的呢? 」
Lakini baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Kwa nini mnafanya kitu ambacho si halali kisheria kukifanya siku ya sabato”?
3 耶穌回答說:「你們沒有讀過:達味和同他在一起的人,在飢餓時所做的嗎?
Yesu, akawajibu, akisema, “Hamkuwahi kusoma kile Daudi alifanya alipokuwa na njaa, yeye na wanaume waliokuwa pamoja naye?
4 怎麼進了天主的殿,拿起供餅來吃了,又給了同他在一起的人吃。這餅原不准他人吃,而只准司祭吃。
Alikwenda katika nyumba ya Mungu, na akachukuwa mikate mitakatifu na kuila baadhi, na kuitoa baadhi kwa watu aliokuwa nao kuila, hatakama ilikuwa halali kwa makuhani kuila.”
5 耶穌又向他們說:「人子是安息日的主。」
Kisha akawaambia, “Mwana wa Adamu ni Bwana wa Sabato.”
6 另一個安息日,祂進了會堂施教。在那裡有一個人,他的右手乾枯了。
Ilitokea katika Sabato nyingine kwamba alikwenda ndani ya sinagogi na kuwafundisha watu huko. Palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kulia ulikuwa umepooza.
7 經師和法利賽人窺察祂是否在安息日治病,好尋隙好控告祂。
Waandishi na Mafarisayo walikuwa wanamwangalia kwa makini kuona kama angemponya mtu siku ya Sabato, ili waweze kupata sababu ya kumshtaki kwa kufanya kosa.
8 祂看透了他們的心思,就對那枯了手的人說:「起來,站在中間。」他遂站了起來。
Lakini alijua nini walikuwa wanafikiri na akasema kwa mtu aliyekuwa amepooza mkono, “Amka, simama hapa katikati ya kila mmoja.” Hivyo huyo mtu akanyanyuka na kusimama pale.
9 耶穌對他們說:「我問你們:安息日是許行善呢? 還是許作惡呢? 是救命呢? 還是喪命呢?
Yesu akasema kwao, “Nawauliza ninyi, ni halali siku ya Sabato kufanya mema au kufanya madhara, kuokoa maisha au kuyaharibu?” Kisha aliwaangalia wote na kumwambia yule mtu,
10 祂環視眾人一週,就對那人說:「伸出你的手來! 那人照樣一做,他的手便復了原。
“Nyoosha mkono wako.” Akafanya hivyo, na mkono wake ulikuwa umeponywa.
11 他們竟狂怒填胸,彼此商議,要怎樣來對付耶穌。
Lakini walijawa na hasira, wakaongeleshana wao kwa wao kuhusu nini wanapaswa wafanye kwa Yesu.
12 在這幾天,耶穌出去,上山祈禱。
Ilitokea siku hizo kwamba alikwenda mlimani kuomba. Aliendelea usiku mzima kumuomba Mungu.
13 天一亮,祂把們徒叫來,由他們人揀選了十二人,並稱他們為宗徒:
Ilipokuwa asubuhi, aliwaita wanafunzi wake kwake, na akawachagua kumi na wawili kati yao, ambao pia aliwaita “mitume.”
14 即西滿,耶穌又給他起名叫伯多祿,和他的兄弟安德肋、雅各伯、若望、斐理伯、巴爾多祿茂、
Majina ya wale mitume yalikuwa Simoni (ambaye pia alimwita Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartolomayo,
15 瑪竇、多默、阿耳斐的兒子雅各伯、號稱「熱誠者」的西滿、
Mathayo, Tomaso na Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni, ambaye aliitwa Zelote,
16 雅各伯的兄弟猶達和猶達依斯加略,他成了負賣者。
Yuda mwana Yakobo na Yuda Iskariote, ambaye alikuwa msaliti msaliti.
17 耶穌同他們下山,站在一塊平地上,有祂的一大群們徒和很多從猶太、耶路撒冷及提洛和漆冬海邊來的群眾,
Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.
18 他們來是為聽祂講道,並為治好自己的病症;那些疲邪魔纏擾的人都被治好了
Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia.
19 群眾都設法觸摸祂,因為有一種能力從祂身上出來,治好眾人。
Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote.
20 耶穌舉目望自己的們徒說:「你們貧窮的是有福的,因為天主的國是你們的。
Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu.
21 你們現今飢餓的是有福的,因為你們將得飽飫。你們現今哭泣的是有福的,因為你們將要歡笑。
Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka.
22 幾時,為了人子的緣故,人惱恨你們,並棄絕你們,並以的名字為可惡的,而加以辱罵詛咒,你們才是有福的。
Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu.
23 在那一天,歡喜踴躍吧! 看,你們的賞報在天上是豐厚的,因為他們的祖先也同樣對待了先知。
Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.
24 但是你們富有的是禍的,因為你們已經獲得了你們的安慰。
Lakini ole wenu mlio matajiri! Kwa maana mmekwisha pata faraja yenu.
25 你們現今飽飫的是禍的,因為你們將要飢餓。你們現今歡笑的是禍的,因為你們將要哀慟哭泣。
Ole wenu mlio shiba sasa! Kwa maana mtaona njaa baadaye. Ole wenu mnaocheka sasa! Kwa maana mtaomboleza na kulia baadaye.
26 幾時,眾人都誇讚你們,你們是禍的,因為他們的祖先也同樣對待了假先知。
Ole wenu, mtakaposifiwa na watu wote! Kwa maana baba zao waliwatendea manabii wa uongo vivyohivyo.
27 但是我給你們這些聽眾說:應愛你們的仇人,善待惱恨你們的人;
Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni.
28 應祝福詛咒你們的人,為毀謗你們的人祈禱。
Wabarikini wale wanao walaani ninyi na waombeeni wale wanaowaonea.
29 有人打你的面頰,也把另一面轉給他,有人拿去你的外衣,也不要阻擋他拿你的內衣。
Kwake yeye akupigaye shavu moja, mgeuzie na la pili. Kama mtu akikunyang'anya joho lako usimzuilie na kanzu.
30 凡求你的,就給他;有人拿你的東西,別再索回。
Mpe kila akuombaye. Kama mtu akikunyang'anya kitu ambacho ni mali yako, usimuombe akurudishie.
31 你們願意人怎麼待你們,也要怎麼待人。
Kama mpendavyo watu wawatendee, nanyi watendeeni vivyo hivyo.
32 若你們愛那愛你們的,為你們還算什麼功德? 因為連罪人也愛那愛他們的人。
Kama mkiwapenda watu wawapendao ninyi tu, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwamaana hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
33 你們善待那善待你們的,為你們還算什麼功德? 因為連罪人也這樣做。
Kama mkiwatendea mema wale wanaowatendea ninyi mema, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwa maana hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
34 你們若借給那些有希望償還的,,為你們還算什麼功德? 就是連罪人也借給罪人,為能如數收回。
Kama mkikopesha vitu kwa watu ambao mnategemea watawarudishia, hiyo ni thawabu gani kwenu? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, na hutegemea kupokea kiasi hicho hicho tena.
35 但是,當愛你們的仇人,善待他們;借出,不要再有所希望:如此,你們的賞報必定豐厚,且要成為至高者的子女,因為祂對待忘恩的和惡人,是仁慈的。
Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwasababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu.
36 你們應當慈悲,就像你們的父那樣慈悲。
Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
37 你們不要判斷,你們也就不受判斷;不要定罪,也就不被定罪;你們要赦免,也就蒙赦免。
Msihukumu, nanyi hamta hukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Sameheni wengine, nanyi mtasamehewa.
38 你們給也就給你們;並且還要用好的,連按帶搖,以致外溢的升斗,倒在你們的懷裏,因為你們用什麼升斗量,也用什麼升斗量給你們。
Wapeni wengine, nanyi mtapewa. Kiasi cha ukarimu - kilichoshindiliwa, kusukwasukwa na kumwagika - kitamwagika magotini penu. Kwa sababu kwa kipimo chochote mnachotumia kupimia, kipimo hicho hicho kitatumika kuwapimia ninyi.”
39 祂又向他們講比喻說:「瞎子豈能給瞎子領路? 不是兩人都要跌在坑裏嗎?
Kisha akawaambia mfano pia. “Je mtu aliye kipofu aweza kumwongoza mtu mwingine kipofu? Kama alifanya hivyo, basi wote wangalitumbukia shimoni, je wasingetumbukia?
40 沒有徒弟勝過師父的:凡受過完備教育的,僅相似自己的師父而已。
Mwanafunzi hawi mkubwa kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu akiisha kufundishwa kwa ukamilifu atakuwa kama mwalimu wake.
41 怎麼,你看見你兄弟眼中的木屑,而你眼中的大樑,倒不理會呢?
Na kwa nini basi wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti lililo ndani ya jicho lako huliangalii?
42 你怎能對你的兄弟說:兄弟,讓我取出你眼中的木屑吧! 而你竟看不見你眼中的大樑呢? 假善人啊! 先取出你眼中的大樑,然後才看得清楚,以便取出你兄弟眼中的木屑。
Utawezaje kumwambia ndugu yako, 'Ndugu, naomba nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,' nawe huangalii boriti iliyo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Kwanza itoe boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utaona vizuri kutoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.
43 沒有好樹結壞果子的,也人壞樹結好果子的。
Kwa sababu hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri.
44 每一棵樹,憑它的果子就可認出來。人從荊棘上收不到無花果,從茨藤上也剪不到葡萄。
Kwa sababu kila mti hutambulika kwa matunda yake. Kwa sababu watu hawachumi tini kutoka kwenye miba, wala hawachumi zabibu kutoka kwenye michongoma.
45 善人從自己心中的善庫發出善來,惡人從惡庫中發出惡來,因為心裏充滿什麼,口裏就說什麼。
Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu. Kwa sababu kinywa chake husema yale yaujazayo moyo wake.
46 你們為什麼稱呼我:主啊! 主啊! 而不我所吩咐的呢? 」
Kwanini mnaniita, 'Bwana, Bwana', na bado hamyatendi yale nisemayo?
47 凡到我跟前,聽了我的道理,而實行的,我要給你們指出,他相似什麼人:
Kila mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatendea kazi, nitawaonyesha jinsi alivyo.
48 他相似一個建築房屋的人,掘地深挖,把基礎立在盤石上,洪水瀑發時,大水沖擊那座房屋,而不能搖動它,因為它建築得好。
Anafanana na mtu ajengae nyumba yake, ambaye huchimba chini sana, na kujenga msingi wa nyumba juu ya mwamba imara. Mafuriko yalipokuja, maporomoko ya maji yaliipiga nyumba, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.
49 但那聽了而不實行的,相似在平地上不打基礎,而築房屋的人,洪水一沖擊,那房屋立刻傾倒,且破壞的很慘。」
Lakini yeyote asikiaye neno langu na hakulitii; mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ulipoishukia kwa nguvu, nyumba ile ilitopata maangamizi makubwa.

< 路加福音 6 >