< 利未記 18 >

1 上主訓示梅瑟說:」
Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
2 你告訴以色列子民說:我是上主你們的天主。
“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
3 你們不要仿效你們註過的埃及地的習慣,也不要仿效我正要領你們去的客納罕地的習慣,不要隨從他們的風俗;
Msitende mambo ambayo watu wa Misri huyatenda, mahali mlikokuwa mkiishi awali. Na ni lazima msitende mambo yale wanayoyatenda watu wa Kanaani, nchi ambayo ninawapeleka nyinyi. Msifuate desturi zao.
4 應執行我的規定,遵守我的法令,依照遵行:我,上主是你們的天主。
Sheria zangu ndizo mtakazozitenda, na amri zangu ndizo mtakazozishika, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
5 你們應遵守我的法令和規定;遵守的人必因此獲得生命:我是上主。婚姻的阻礙
Kwa hiyo ni lazima mzitunze hukumu zangu na sheria zangu. Ikiwa mtu amezitii, ataishi kwa sababu ya hizo. Mimi Ndimi Yahweh.
6 你們中任何人不可親近血親,去揭漏她的下體:我是上主。
Pasiwepo kwenu atakayelala na yeyote aliye na uhusiano wa karibu naye. Mimi ndimi Yahweh.
7 你不可揭露你父親得下體和你母親的下體:她是你的母親,不可揭露她的下體。
Usimfedheheshe baba yako kwa kulala na mama yako. Yeye ni mama yako! Haikupasi kumfedhehesha yeye.
8 你父親妻子的下體,你不可揭露,那是你父親的下體。
Usilale na yeyote wa wake za baba yako; Usimfedheheshe namna hiyo baba yako.
9 你姊妹的下體,不論他是你父親的女兒,或你母親的女兒,或在家生的,或在外生的,你不可揭露她們的下體。
Usilale na yeyote aliye mmoja miongoni mwa dada zako, ama ni binti ya baba yako au ni binti ya mama yako, ama aliyelelewa nyumbani mwenu au mbali nawe. Usilale na dada zako.
10 你兒子的女兒,或你女兒的女兒的下體,你不可揭露,因為她們的下體是你們的下體。
Usilale na binti ya mwanao, au binti ya binti yako. Hiyo ingekuwa aibu yako mwenyewe.
11 你不可揭露你父親妻子的女兒的下體,因為她是你父親所生,是你得姊妹,你不可揭露她的下體。
Usilale na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa kwa baba yako, yeye ni dada yako, na usilale naye.
12 你父親姊妹的下體,你不可揭露,因為她是你父親的骨肉。
Usilale na dada ya baba yako. Yeye ni ndugu wa karibu kwa baba yako.
13 你母親姊妹的下體,你不可揭露,因為她是你母親的骨肉。
Usilale na dada ya mama yako. Yeye ni ndugu wa mama yako.
14 你父親兄弟的下體,你不可揭露,也不可親近他的妻子;她是你的叔伯母。
Usimfedheheshe ndug wa baba yako kwa kulala na mke wake. Usimkaribie kwa kusudi hilo; yeye ni shangazi yako.
15 你兒媳的下體,你不可揭露。她是你兒子的妻子,你不可揭露她的下體。
Usilale na binti- mkwe wako, Yeye ni mke wa mwanao; usilale naye.
16 你兄弟妻子的下體,你不可揭露;那是你兄弟的下體。
Usilale na mke wa kaka yako; usije ukamfedhesha yeye katika njia hii.
17 你不可揭露了一女人的下體又揭露她女兒;不可娶她兒子的女兒,或她女兒的女兒,揭露她的下體,她們都是她的血親:這是醜行。
Usilale na mwanamke kisha na binti yake, au binti wa mwanawe au binti wa binti yake. Hao ni ndugu zake wa karibu, na kulala nao lingekuwa ni uovu.
18 你不可娶一女人又娶他的姊妹,做她的情敵,在她活著的時候,揭露她姊妹的下體。[違犯貞潔的惡行]
Usimwoe dada ya mke wako kuwa mke wako wa pili na kulala naye wakati bado mke wako wa kwanza angali hai.
19 女人在月經不潔期中,你不可接近,揭露她的下體。
Usilale na mwanamke wakati wake wa hedhi.
20 你近人的妻子你不可與她同寢,為她所沾污。
Yeye ni najisi kwa wakati huo. Usilale na mke wa jilani yako na kujichafua mwenyewe kwake katika njia hii.
21 你不可使你任何一個子女經火祭獻給摩肋客,亦不可褻瀆你天主的名:我是上主。
Msiwatoe watoto wenu ili kuwapitisha kwenye moto, ili kwamba muwatoe sadaka kwa Moleki, kwa sababu msije mkalinajisi jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Yahweh.
22 你不可與男人同寢,如同與女人同寢一樣:這是醜惡行為。
Usilale na mwanaume mwingine kama ulalavyo na mwanamke. Jambo hili lingekuwa uovu.
23 你不可與任何獸類同寢,為牠所淫污,女人亦不可委身與走獸,同牠交合:這是逆性邪惡。
Usilale na myama yeyote na kujitia unajisi kwake. Haimpasi mwanamke kufikiria kulala na mnyama ye yote. Huo ungekuwa upotovu.
24 你們不可以任何這樣的事玷污自己,因為這些民足以這一些事玷污了自己,我正要由你們面前將他們驅逐;
Msijichafue wenyewe katika njia hizi, kwa kuwa katika njia hizi mataifa yamechafuliwa, mataifa ambayo Nitayafukuza yatoke kwa ajili yenu.
25 甚至連這地也玷汙了,所以我必追究這地上的罪惡,使這地吐棄地上的居民。
Ni kwa sababu nchi imenajisiwa, hivyo niliiadhibu dhambi yao, nayo nchi ikawatapika wakazi wake
26 至於你們,應遵守我的法令和規定;不論是本地人,或是寄居在你們中間的外方人,這樣醜惡的事,一件也不許做,
Kwa hiyo, yawapasa kuzishika amri zangu na maagiza yangu, na msifanye aina yoyote ya mambo haya ya machukizo, wala Mwisraeli mzaliwa au Mgeni aishie miongoni mwenu.
27 因為在你們以前住在這地上的人,做過這一切醜惡的事,玷污了這地方。
Kwa kuwa ni uovu huu ambao watu wametenda, wale ambao waliishi hapa kabla yenu, na sasa nchi imenajisiwa.
28 希望這地不要因你們而再受到玷汙,將你們吐棄,如同吐棄了你們之前的民族。
Kwa hiyo, muwe waangalifu ili kwamba nchi isiwatapike nyinyi baada ya kuwa mmeinajisi, kama ilivyowatapika wale watu waliokuwako kabla yenu.
29 因為,凡做任何一件這樣醜惡的事,這樣的人,都應由民間剷除。
Yeyote anayefanya mambo haya ya kuchukiza, watu wafanyao mambo hayo ya kuchukiza lazima watakatiliwa mbali kutoka miongoni mwa watu wao.
30 所以你們應遵守我的禁令,不可仿效你們以前的人所有的醜惡風俗,免得因此受到玷汙:我,上主是你們的天主。
Kw a hiyo inawapasa kuzishika amri zangu na sitende mojawapo ya desturi hizi zenyekuchukiza ambazo zilitendwa hapo kabla yenu, ili msijinajisi wenyewe kwa hizo. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.

< 利未記 18 >