< 利未記 15 >

1 上主訓示梅瑟和亞郎說:」
Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,
2 你們告訴以色列子民說:幾時一個男人身患淋病,淋病使他不潔。
“Waambie watu wa Israeli, na sema kwao, 'Wakati mtu yeyote kisonono kimemwathiri mwili wake unatoa ugiligili, anakuwa najisi.
3 淋病使人不潔的光景是這樣:不論他身體常流淋液,或有時止住,他總是不潔的。
Unajisi wake unatokana na athari ya kisonono. Iwe mwili wake unatoa ugiligili au umekoma, huo ni unajisi.”
4 凡有淋病的人睡過的床,即染上不潔;凡他坐過之物,即染上不潔。
Kitanda chochote anachokilalia kitakuwa najisi, na kila kitu ambacho anakaa juu yake kitakuwa najisi.
5 凡人摸了他的床,這人應洗滌自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的;
Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na awe amenajisika mpaka jioni.
6 誰坐了淋病人坐過之物,該洗自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的;
Yeyote anayekaa katika kitu chochote ambacho mtu ambaye ameathiriwa na kisonono alikaa, mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
7 誰摸了淋病人的身體,應洗滌自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的。
Na yeyote anayegusa mwili wa ambaye ameathirika na kisonono lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na awe najisi hadi jioni.
8 若有淋病的人,在潔淨人身上吐了唾沫,這人就應洗滌自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的。
Kama mtu ambaye anaona majimaji kama hayo kwa mtu fulani ambaye ametakasika, ndipo mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na atakuwa najisi hata jioni.
9 凡有淋病的人坐過的鞍子,即染上不潔。
Tandiko lolote ambalo ambaye anamajimaji ya kisonono atalikalia litakuwa najisi.
10 誰摸了他身下的任何東西,直到晚上是不潔的;誰攜帶了這些東西,該洗滌自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的。
Yeyote anayegusa kitu chochote kilichokuwa chini ya mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni, na yeyote anayebeba vitu hivyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji; atanajisika mpaka jioni.
11 若有淋病的人,沒有用水洗手接觸了人,這人就應洗滌自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的。
Ambaye anamajimaji kama hayo akimgusa kabla kwanza ya kuosha kwa maji safi mikono yake, mtu aliyeguswa lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
12 凡有淋病的人摸過的陶器,都應打破,任何木具,都應用水洗淨。
Chungu chochote cha udongo ambacho ambaye anamajimaji kama hayo akigusa lazima kivunjwe, na kila chombo cha mti lazima kioshwe na maji safi.
13 幾時有淋病的人治好不流了,他應計算七天為取潔期,洗滌自己的衣服,用活水洗身,然後就潔淨了。
Wakati mwenye kisonono anapotakaswa katika kisonono chake, ndipo lazima ahesabu kwaajili yake siku saba kwaajili ya kutakasika kwake; ndipo afue nguo na aoshe mwili wake kwenye maji yatiririkayo. Ndipo atakuwa safi.
14 到第八天,應拿兩隻斑鳩或兩隻雛鴿,來到上主面前,再會幕門口,交給司祭。
Katika siku ya nane lazima achukue njiwa wawili au kinda mbili za njiwa na aje mbele za Yahwe pakuingilia kwenye hema ya mkutano; pale lazima atoe hao ndege kwa kuhani.
15 司祭應奉獻一隻作贖罪祭,另一隻作全番祭。這樣司祭就替他在上主面前,為他的淋病行了贖罪禮。
Lazima kuhani awatoe, moja kama sadaka ya dhambi na nyingine kama ya kuteketezwa, na kuhani lazima afanye upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe kwaajili ya kisonono chake.
16 人若遺精,應用水洗淨全身,直到晚上是不潔的。
Kama mtu yeyote ametokwa na shahawa, ndipo lazima aoge mwili wake wote katika maji; atanajisika mpaka jioni.
17 凡沾有精異得衣服或皮物,應用水洗淨,直到晚上是不潔的。
Kila vazi au ngozi ambayo juu yake kuna shahawa lazama paoshwe kwa maji; itakuwa najisi mpaka jioni.
18 男女同房媾精,兩人都應用水洗澡,直到晚上是不潔的。
Na kama mwanamke na mwanaume watalala pamoja na kunakutokwa kwa shahawa kwenda kwa mwanamke, lazima wote wawili waoge katika maji; watakuwa najisi mpaka jioni.
19 女人幾時行經,有血由她體內流出,她的不潔期應為七天;誰接觸了她,直到晚上是不潔的。
Mwanamke anapokuwa kwenye hedhi, ataendelea kunajisika kwa siku saba, na yeyote anayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
20 她不潔期內,凡她臥過之處,都染上不潔,凡她坐過之處,也染上不潔;
Chochote anacholala juu yake wakati wa hedhi kitakuwa najisi; kila kitu ambacho anakalia kitakuwa pia najisi.
21 凡摸過她床榻的,應洗滌自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的;
Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
22 凡摸過她坐過之物,應洗滌自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的;
Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.
23 誰若摸了她床上,或她坐過之物上的東西,直到晚上是不潔的;
Iwe juu ya kitanda au kitu chochote juu ya popote atakapokaa, kama akikigusa, mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
24 若男人與她同房,也沾染上她的不潔,七天之久,是不潔的;凡他臥過的床,也染上不潔。
Kama mwanaume yeyote akilala naye, na unajisi wa mwanamke ukamgusa, atakuwa amenajisika siku saba. Kila kitanda ambacho anakilalia mwanaume huyo kitanajisika.
25 女人若在經期外,多日流血;或者,她流血超過了她月經的日期,在流不潔之物的整個時期內,她如在經期內一樣不潔。
Kama mwanamke ametokwa damu kwa siku nyingi ambayo siyo kipindi cha hedhi yake, au ikitoka zaidi ya kipindi chake cha hedhi, wakati wote wa siku za kunajisika, atakuwa kama alikuwa kwenye siku zake za hedhi. Yeye ni najisi.
26 凡她流血期內所臥過的床,就如在經期臥過的床依樣染上不潔;凡她坐過之物,就如她經期內所坐過之物一樣,染上不潔。
Kila kitanda anachokilalia wakati wote wa kutokwa damu itakuwa kwake sawa tu kama kitanda anacholalia wakati wa hedhi, na kila kitu ambacho anakalia kitakuwa najisi, kama tu unajisi wa hedhi yake.
27 誰若摸了,就染上不潔,應洗滌自己的衣服,用水洗澡,直到晚上是不潔的。
Na yeyote anayegusa kitu kati ya vitu hivyo atakuwa najisi; lazima yeye afue nguo zake na aoge mwenyewe kwenye maji, na atakuwa amenajisika mpaka jioni.
28 幾時她治好不流了,她應計算七天,為取潔期。
Lakini kama mwanamke ametakasika katika kutokwa na damu, ndipo atahesabu kwaajili yake siku saba, baada ya hizo atakuwa safi.
29 到第八天,應拿兩隻斑鳩或兩隻雛鴿,來到會幕門口交給司祭;
Katika siku ya nane atachukua kwake njiwa wawili au kinda wawili wa njiwa na atawaleta kwa kuhani pakuingilia hema ya mkutano.
30 司祭應奉獻一隻作贖罪祭,另一隻作全番祭:這樣司祭就替她在上主面前,為她所流的不潔之物行了贖罪禮。
Huyo kuhani atatoa ndege mmoja kama sadaka ya dhambi na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa, na atafanya upatanisho kwaajili ya huyo mbele ya Yahwe kwaajili unajisi wa mwanamke atokwaye damu.
31 你們應叫以色列子民戒避他們的不潔,免得他們因不潔,玷沾汙了我在他們不中的住所,而遭受死亡。
Hivi ndivyo lazima uwatenge watu wa Israeli katika unajisi wao, hivyo hawatakufa tokana na unajisi wao, kwa kuchafua hema langu, ambapo naishi kati yao.
32 這是有關因淋病,或遺精沾染不潔的人,
Huu ndio utaratibu kwa kila ambaye anakisonono, kwaajili kila mwanaume ambaye shahawa yake inatoka na inamfanya kuwa najisi,
33 和行經的婦女,即有關任何遺漏的男女,以及與不潔的女人同房的男人的法律。」
kwaajili ya mwanamke ambaye yuko katika kipindi cha hedhi, kwaajili ya yeyote aliye na kisonono, awe mwanaume au mwanamke, na kwaajili ya yeyote anayelala na mwanamke najisi.

< 利未記 15 >