< 士師記 8 >
1 那時厄弗辣因人對基德紅說:「你去攻打米德楊時,沒有召叫我們,你為什麼這樣對待我們﹖」他們激烈的與他爭吵。
Watu wa Efraimu wakamwambia Gideoni, “Ni nini hiki umetutenda? Haukuita wakati ulipokwenda kupigana na Midiani.” Wakamwambia kwa nguvu.
2 他回答他們說:「我所行的怎能比得上你們呢﹖厄弗辣因所拾的不比阿彼厄則爾所收的葡萄更好嗎﹖
Akawaambia, “Nimefanya nini sasa kulinganisha na mlichofanya ninyi? Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri?
3 天主將米德楊的首領敖勒布和則厄布交在你們手中,我所能行的怎能與你們相比﹖」為了他這番話,他們對他的怒氣,就平息了。基德紅乘勝追趕米德楊王
Mungu amewapa ushindi juu ya wakuu wa Midiani-Orebu na Zeeb! Mimi nimefanya nini ukilinganisha na ninyi?” Hasira yao ikashuka chini aliposema hili.
4 基德紅來到約但河,就渡過河;他與跟隨他的三百人,雖然都疲倦,仍繼續追趕。
Gideoni alikuja Yordani na akavuka juu yake, yeye na watu mia tatu waliokuwa pamoja naye. Walikuwa wamechoka, lakini bado waliendelea kufuatilia.
5 他向穌苛特人說:「請你們給跟隨我的人幾個餅吃,因為他們疲倦了,我還願意追趕米德楊的兩個王子則巴黑和匝耳慕納。」
Akawaambia watu wa Sukothi, “Tafadhali wape mikate kwa watu wanaonifuata, kwa kuwa wamechoka, nami niwafuatilia Zeba na Salmuna, wafalme wa Midiani.
6 穌苛特人的頭目回答說:「難道則巴黑和匝耳慕納的手已在你的掌握中,我們就該把餅送給你的軍隊嗎﹖」
Na wakuu wakasema, “Je, mikono ya Zeba na Salmuna sasa ipo mikononi mwako? Kwa nini tulipe jeshi lako mikate?”
7 基德紅說:「好罷! 幾時上主把則巴黑和匝耳慕納交在我手中,我必要用茨條和荊棘鞭撻你們的身體。」
Gideoni akasema, “Bwana akitupa ushindi juu ya Zeba na Salmunna, nitainyunyiza ngozi yenu kwa miiba ya jangwani na michongoma.
8 以後由那裏上去,到了培奴耳,也向他們說了同樣的話;培奴耳人回答他也像穌苛特人一樣。
Akatoka huko, akaenda Penieli, akawaambia watu maneno hayo hayo; lakini watu wa Penieli wakamjibu kama watu wa Sukothi walivyojibu.
9 他也對培奴耳人說:「當我平安回來時,我必拆毀這座碉堡。」
Akawaambia pia watu wa Penieli, akasema, “Nitakapokuja kwa amani, nitauangusha mnara huu.”
10 那時則巴黑和匝耳慕納正在卡爾科爾,他們的軍隊約有一萬五千人,這是全部東方子民所剩的軍隊,因為已有十二萬持刀的被擊弊斃了。
Sasa Zeba na Salmuna walikuwa huko Karkori pamoja na jeshi lao, karibu na watu elfu kumi na tano, wote waliosalia nje ya jeshi lote la watu wa Mashariki, kwa kuwa walianguka watu 120, 000 waliofundishwa kupigana na upanga.
11 基德紅從諾巴黑和約革治哈東面,順著住帳棚人的路上去,當敵人自以為安全的時候,襲擊了軍營,
Gideoni akapanda barabara iliyochukuliwa na wakaazi wa hema, Noba na Yogbena. Akalishinda jeshi la adui, kwa sababu hawakuwa wanatarajia shambulio.
12 則巴黑和匝耳慕納落荒而逃,基德紅在後面追趕,捉住了那兩個米德楊王子則巴黑和匝耳慕納,並使全軍覆沒。
Zeba na Salmuna walikimbia, na Gideoni alipowafuata, akawatwaa wafalme wawili wa Midiani-Zeba na Salmunna- na kulifanya jeshi lote kuwa na hofu.
13 約阿士的兒子基德紅,從戰場沿赫勒斯斜坡回來,
Gideoni, mwana wa Yoashi, alirudi kutoka kwenye vita kwenda kupitia Heresi.
14 捉住了穌苛特的少年人,查問他。這少年人就給他寫下穌苛特的首領和長老的名字,共七十七人。
Akamkimbilia kijana mmoja wa watu wa Sukothi na kutafuta ushauri kutoka kwake. Kijana huyo alimwelezea viongozi wa Sukothi na wazee wake, watu sabini na saba.
15 基德紅遂往穌苛特人那裏去說:「看! 這是則巴黑和匝耳慕納,你們為了他們曾譏笑我說:難道則巴黑和匝耳慕納的手已在你掌握中,我們就該把餅送給你疲倦的人嗎﹖」
Gideoni akaja kwa watu wa Sukothi, akasema, “Tazameni Zeba na Salmuna, ambao mlinidhihaki kwa ajili yao, nikasema, 'Je! mmemshinda Zeba na Salmuna? Hatujui kwamba tunapaswa kulipa jeshi lako mkate.”
16 他於是捉住那城的長老,用曠野裏的茨條和荊棘懲罰了蘇苛特居民。
Gideoni akawachukua wazee wa mji, naye akawaadhibu watu wa Sukothi pamoja na miiba ya jangwa na michongoma.
17 以後又把培奴耳的碉堡拆毀,殺戮了城內的居民。
Akaangusha mnara wa Penieli na kuwaua watu wa mji huo.
18 然後詢問則巴黑和匝耳慕納說:「你們在大博爾山上殺戮的那些人是怎樣的人呢﹖」他們答說:「他們像你們一樣,個個都像君王的兒子。」
Gideoni akamwambia Zeba na Salmuna, “Ni watu wa aina gani mliwauawa Tabori?” Wakajibu, “Kama wewe ulivyo, ndivyo walivyokuwa. Kila mmoja wao alionekana kama mwana wa mfalme.”
19 基德紅說:「他們是我的兄弟,是我母親的兒子:上主永在:如果你保留了他們不死,我也就不殺你們。」
Gideoni akasema, 'Wao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu. Kama Bwana anaishivyo, kama mngewaacha hai, nisingewauwa.”
20 他遂對自己的長子耶特爾說:「起來,殺死他們! 」但是這孩童害怕,拔不出刀來,因為年紀還小。
Akamwambia Yetheri (mzaliwa wake wa kwanza), “Simama uwaue!” Lakini kijana huyo hakutoa upanga wake kwa kuwa aliogopa, kwa sababu alikuwa bado kijana mdogo.
21 因此,則巴黑和匝耳慕納說:「你親自起來殺死我們罷! 因為人怎樣,他的力量也怎樣。」基德紅就起來殺了則巴黑和匝耳慕納,拿去他們駱駝頸上的月牙環。基德紅辭王位及其末年
Ndipo Zeba na Salmuna wakasema, simama mwenyewe, utuue! Kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Gideoni akasimama na kumwua Zeba na Salmuna. Pia aliondoa mapambo yaliyokuwa juu ya shingo za ngamia zao.
22 事後,以色列人便對基德紅說:「你既然從米德楊手中拯救了我們,請你和你的子孫作我們的君王! 」
Ndipo wana wa Israeli wakamwambia Gideoni, “Ututawale, wewe, mtoto wako, na mjukuu wako; kwa sababu umetuokoa mikononi mwa Midiani.”
23 基德紅回答他們說:「我不作你的君王,我的子孫也不作你們的君王,唯有上主是你們的君王。」
Gideoni akawaambia, “Mimi sitatawala juu yenu, wala mtoto wangu hatatawala juu yenu. Bwana atatawala juu yenu.”
24 基德紅又向他們說:「我只向你們要求一件事:請將每人掠奪的金環給我。」原來依市瑪耳人都有金環。
Gideoni akawaambia, “Nina haja yangu niitakayo kwenu kwamba kila mmoja wenu atanipe pete kutoka kwenye nyara zake.” (Wamidiani walikuwa na pete za dhahabu kwa sababu walikuwa Waishmaeli.)
25 他們答說:「我們情願給你。」於是舖開一件外衣,每人把所掠奪的金環擲在上面。
Wakamjibu, “Tunafurahi kukupa.” Wakatandika vazi na kila mtu akatupa pete kutoka kwenye nyara zake.
26 他所要的金環共有一千七百「協刻耳」重;此外尚有月牙環、耳環和米德楊王所穿的紫紅衣,及他們駱駝頸上的項鏈。
Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilikuwa shekeli 1, 700 za dhahabu. Nyara hizi zilikuwa ni pamoja na mapambo ya makoja, vidani, nguo ya rangi ya zambarau waliyovaa na wafalme wa Midiani, na zaidi ya minyororo iliyokuwa karibu na shingo za ngamia zao.
27 基德紅用這些金子造了一個「厄弗得」便成了基德紅及其家族的羅網。
Gideoni akafanya efodi kutoka katika pete na kuiweka katika mji wake, huko Ofra, na Israeli wote wakaiandama kwa ukahaba na kuabudu. Ilikuwa mtego kwa Gideoni na kwa wale walio nyumbani kwake.
28 米德楊在以色列子民前面屈服,再沒有抬起頭來。基德紅在世時,境內平安了四十年。
Kwa hiyo Midiani ilishindwa mbele ya watu wa Israeli na hawakuinua vichwa vyao tena. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini siku za Gideoni.
Yerubaali, mwana wa Yoashi, akaenda akakaa nyumbani kwake.
30 基德紅有七十個兒子,都是他親生的,因為他有很多妻子。
Gideoni alikuwa na wana sabini, waliokuwa uzao wake, kwa kuwa alikuwa na wake wengi.
31 他在舍根的妾也給他生了一個兒子,給他起名叫阿彼默肋客。
Mwanamke wake, aliyekuwa Shekemu, akamzaa pia mwana, na Gideoni akampa jina lake Abimeleki.
32 約阿士的兒子基德紅壽終正寢,埋在阿彼厄則爾的敖弗辣,他父親約阿士的墳墓裏。
Gideoni, mwana wa Yoashi, akafa katika uzee mzuri, akazikwa huko Ofra katika kaburi la baba yake Joashi, wa jamaa ya Abiyezeri.
33 基德紅死後,以色列子民又去跟從巴耳諸神行邪淫,立巴耳貝黎特當做他們的天主。
Ikawa, Gideoni alipokufa, watu wa Israeli wakageuka tena na kujifanyia ukahaba wenyewe kwa kuabudu Mabaali. Wamlifanya Baali Berith kuwa mungu wao.
34 以色列子民忘記了上主他們的天主,曾從四周所有的敵人手中救了他們,
Watu wa Israeli hawakukumbuka kumtukuza Bwana, Mungu wao, aliyewaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao kila upande.
35 也沒有恩待耶魯巴耳即基德紅的家,以報答他施於以色列的恩惠。
Hawakuweka ahadi zao kwa nyumba ya Yerubaali (yaani Gidioni), kwa ajili ya mema yote aliyoyafanya katika Israeli.