< 士師記 7 >
1 耶魯巴耳即基德紅和所有跟隨他的民眾一早起身,在哈洛得泉安營;米德楊的營幕就在他們北面,在摩勒山腳的平原裏。
Ndipo Yerubaali (yaani Gideoni) akainuka mapema, na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaweka kambi kando ya chemchemi ya Harodi. Kambi ya Midiani ilikuwa kaskazini mwao katika bonde karibu na kilima cha More.
2 上主對基德紅說:「跟隨你的民眾太多,我不能把米德楊交在他們手中,免得以色列對我自誇說:是自己的能力救了自己。
Bwana akamwambia Gideoni, Kuna askari wengi sana kwa mimi kukupa ushindi juu ya Wamidiani, ili Waisraeli wasijisifu juu yangu, wakisema, 'Nguvu zetu zimetuokoa'.
3 現在你要向民眾宣告說:凡害怕恐懼的可以回去,急速離開這裏。」於是民眾中有二萬二千回去,只剩下一萬人。
Basi, tangaza masikioni mwa watu, ukisema, Yeyote anayeogopa, anayetetemeka, arudi na atoke katika mlima Gileadi. 'Basi, watu elfu ishirini na mbili wakaondoka, na elfu kumi wakabaki.
4 上主又對基德紅說:「民眾還是太多;領他們下到水邊去,我要在那裏為你檢驗他們。凡我告訴你說:這人可同你去,他就與你同去;凡我告訴你說:這人不可同你去,他就不可去。」
Bwana akamwambia Gideoni, 'Watu bado ni wengi sana. Wapeleke chini kwenye maji, na nitafanya idadi yao iwe ndogo kwa ajili yako. Kama nikisema, 'Huyu atakwenda pamoja nawe,' atakwenda pamoja nawe; lakini kama nikisema, 'Huyu hawezi kwenda pamoja nawe,' hatakwenda. '
5 他就引民眾下到水邊;上主向基德紅說:「凡用舌頭舔水像狗舔水似的,將他們安置在一處;同樣,凡屈膝跪下飲水的,將他們安置在一處。」
Gideoni akawapeleka watu kwenye maji; Bwana akamwambia, “Ondoa kila mtu atakayelamba maji, kama mbwa alambavyo, kutoka kwa wale wanaopiga magoti na kunywa.”
6 用手捧到嘴邊舔水的共有三百人;其餘民眾都是屈膝跪下喝水。
Wanaume mia tatu walilamba. Wengine wote walipiga magoti kunywa maji.
7 上主對基德紅說:「我要用這三百舔水的人拯救你們,把米德楊交於你手中。讓其餘的民眾各回本地去。」
Bwana akamwambia Gideoni, “Kwa watu hawa mia tatu waliokwisha kulamba maji, nitakuokoa na kukupa ushindi juu ya Wamidiani. Acha kila mtu arudi mahali pake.”
8 基德紅便留下民眾的罐子和號角,打發眾以色列人各回自己的帳幕,只留下三百人。米德楊的營幕就在他們下面的平原裏。基德紅巧取米德楊營
Kwa hiyo wale waliochaguliwa walichukua vifaa vyao na tarumbeta zao. Gideoni akawarudisha watu wote wa Israeli, kila mtu kwenda kwenye hema yake, lakini akawaweka watu mia tatu. Basi kambi ya Midiani ilikuwa chini yake katika bonde.
9 當夜上主對他說:「起來,下去攻營! 我已將敵營交在你的手中了。
Usiku huo huo Bwana akamwambia, “Simama! Kavamie kambi, kwa maana nitakupa ushindi juu yake.
10 如果你一人害怕下去,可帶你的隨從普辣一起下到營幕,
Lakini ikiwa unaogopa kushuka, shka kwenye kambi pamoja na Purh mtumishi wako,
11 聽他們說什麼;以後你的手就會堅強,敢下去攻營了。」於是他和他的隨從普辣便下去,來到營中駐軍的前哨。
na usikilize kile wanachosema, na ujasiri wako utaimarishwa kushambulia kambi.” Basi Gidioni akaenda pamoja na Pura mtumishi wake, mpaka chini kwa walinzi wa kambi.
12 那時米德楊、阿瑪肋克和東方的子民都散佈在平原裏,多如蝗蟲;他們的駱駝不可勝數,多如海邊的沙粒。
Wamidiani, Waamaleki, na watu wote wa mashariki walikaa karibu na bonde, wengi kama wingu la nzige. Ngamia zao walikuwa zaidi ya mawingu; walikuwa zaidi kuliko idadi ya mchanga katika bahari.
13 基德紅來到時,正有一個人給他的同伴講夢說:「我作了一個夢:有一個大麥麵餅滾入米德楊營內,直滾向帳幕,將帳幕撞倒:翻轉朝上。」
Gideoni alipofika huko, mtu alikuwa akimwambia mwenzake ndoto. Mtu huyo akasema, “Angalia! Niliota ndoto, na nikaona mkate wa shayiri umeanguka ndani ya kambi ya Midiani. Ukaja hemani, na kuipiga kwa nguvu sana hata ikaanguka chini ikapinduka na kulala chini. '
14 他的同伴回答說:「這不是別的,這是以色列人約阿士的兒子基德紅的刀劍;天主已把米德楊及其全營交於他手中。」
Mtu mwingine akasema, 'Hii si kitu kingine isipokuwa upanga wa Gideoni (mwana wa Yoashi), Mwisraeli. Mungu amempa ushindi juu ya Midiani na jeshi lake lote. '
15 基德紅一聽見這夢的敘述和解釋,就朝拜天主;然後回到以色列營中說:「起來! 因為上主已將米德楊的營幕交在你們手中了。」
Gideoni aliposikia habari ya ile ndoto na tafsiri yake, akainama chini na kuabudu. Alirudi kwenye kambi ya Israeli na kusema, “Simameni! Bwana ametupa ushindi juu ya jeshi la Midiani.”
16 他於是把三百人分作三隊,把號角和空罐子交在每人手中,把火把放在罐子裏;
Akawagawa watu mia tatu katika makundi matatu, na akawapa tarumbeta zote na mitungi tupu, na taa ndani ya kila mtungi.
17 然後吩咐他們說:「你們看我怎樣行,你們便怎樣行;一到營幕邊上,我怎樣作,你們也要怎樣作。
Akawaambia, 'Niangalieni mimi na kufanya yale ninayoyafanya. Tazama! Ninapofika kwenye mwisho wa kambi, ni lazima mfanye kile ninachofanya.
18 當我與跟隨我的人吹號角時,你們也應該在營幕四周吹號角,並且喊叫;為上主,為基德紅! 」
Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote Mlio pamoja nami, basi mtapiga tarumbeta zenu katika kila upande wa kambi nzima na kupiga kelele, “Kwa Bwana na Gideoni!”
19 在三更之初,當哨兵換防的時候,基德紅領著他那一百人來到營幕邊上,吹起號角來,打破手中的罐子。
Basi Gideoni na watu mia moja waliokuwa pamoja naye walifika mwisho wa kambi, hapo mwanzoni mwa saa ya kati. Wakati Wamidiani walikuwa wakibadilisha walinzi, walipiga tarumbeta na kuvunja mitungi iliyokuwa mikononi mwao.
20 同時三隊一齊吹號角,打破罐子,左手拿著火把,右手拿著號角吹,並喊叫說:「刀劍為上主,為基德紅! 」
Vikosi vitatu vilipiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Walikuwa na taa katika mikono yao ya kushoto na tarumbeta katika mikono yao ya kulia ili kuwapiga. Walipiga kelele, “Upanga wa Bwana na wa Gideoni.”
21 眾人都在營幕四周,各站在自己的地方。那時敵營驚醒,亂喊亂竄。
Kila mtu alisimama mahali pake kando ya kambi na jeshi la Midiani likakimbia. Walipiga kelele na kukimbia
22 當那三百人吹號角的時候,上主使敵營互相撕殺。以後朝著責勒達逃往貝特史大,直到面對塔巴特的阿貝耳默曷拉。米德楊慘敗
Walipopiga tarumbeta mia tatu, Bwana akaweka upanga wa kila mtu wa Midiani dhidi ya wenzake na dhidi ya jeshi lake lote. Jeshi likimbia mpaka Bethshita kuelekea Serera, mpaka mpaka wa Abel Mehola, karibu na Tabathi.
23 那時以色列人從納斐塔里、阿協爾和默納協全地集合,追趕米德楊。
Watu wa Israeli kutoka Naftali, Asheri, na Manase wote waliitwa nje, nao wakawafuata Midiani.
24 基德紅又打發使者到全厄弗辣因山地說:「請下來攻打米德楊人,在他們前佔據約但河的渡口,直到貝特巴辣。」全厄弗辣因人就集合,佔據了約但河的渡口,一直到貝特巴辣。
Gideoni akatuma wajumbe katika nchi zote za mlima wa Efraimu, akisema, “Nenda chini dhidi ya Midiani na umiliki Mto Yordani mpaka Bethbara, ukawazuie.” Basi wanaume wote wa Efraimu walikusanyika pamoja na kuimiliki maji, mpaka Bethbara na Mto Yordani.
25 他們捉住了米德楊的兩個領袖,即敖勒布和則厄布,在敖勒布石上把敖勒布殺死,在則厄布醡酒池裏把則厄布殺死;以後繼續追趕米德楊人,並把敖勒布和則厄布的頭送到約但對岸基德紅跟前。
Wakawatwaa wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu. Wakamwua Orebu kwenye mwamba wa Orebu, nao wakamwua Zeebu katika shinikizo la divai la Zeebu. Wakawafuata Wamidiani, wakamletea Gideoni vichwa vya Orebu na Zeebu, ng'ambo ya pili ya Yordani.