< 約書亞記 17 >

1 默納協是若瑟的長子,他的支派抽籤分得了一份土地。默納協的長子,基肋阿得的父親瑪基爾,因為是個戰士,分得了基肋阿得和巴商。
Na huu ndio mgao wa nchi kwa ajili ya kabila la Manase (aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Yusufu), ambayo ilikuwa kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, ambaye alikuwa ni baba wa Gilieadi. Watoto wa Makiri walipewa nchi ya Gileadi na Bashani, kwasababu Makiri alikuwa ni mtu wa vita.
2 默納協的其餘子孫,赫肋克的子孫,阿斯黎耳的子孫,舍根的子孫,赫斐爾的子孫,舍米達的子孫:這些人按照家族,都是若瑟之子默納協後代的男丁。
Nchi iliyobaki iligawiwa kwa kabila la Manase, walipewa kwa koo zao, ambazo ni Abi Ezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi, na Shemida. Hawa walikuwa ni watoto wa kiume wa Manase mwana wa Yusufu, waliwakilishwa na koo zao.
3 但是默納協的玄孫,瑪基爾的曾孫,基肋阿得的鯀子,赫斐爾的兒子,責羅斐哈得沒有兒子,只有女兒,他的女兒名叫瑪赫拉、米耳加和提爾匝。
Basi Zelofehadi mwana wa Heferi mwana wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase hakuwa na watoto wa kiume, bali alikuwa na watoto wa kike tu. Na majina ya binti zake yalikuwa Mahila, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.
4 她們來到司祭厄肋阿責爾和農的兒子若蘇厄、並首領們面前說:「上主曾吩咐過梅瑟,在我們弟兄們中,也分給我們一份產業。」若蘇厄遂照上主所吩咐的,使她們在伯叔中間,也分得了一份產業。
Walimwendea Eliazeri kuhani, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi na wakasema, “Yahweh alimwagiza Musa atupatie urithi wetu pamoja na kaka zetu.” Hivyo, kwa kuzingatia agizo la Yahweh, aliwapa wanawake hao urithi miongoni mwa ndugu za baba yao.
5 這樣,除約旦河東的基肋阿得和巴商二地外,尚有十分歸屬於默納協,
Manase alipewa sehemu kumi za nchi katika Gileadi na Bashani, ambayo iko upande mwingine wa Yordani,
6 因為默納協的孫女,在默納協的孫子中也獲得產業;不過基肋阿得屬於默納協其餘的子孫。
kwasababu ya binti za Manase walipokea urithi pamona na watoto wake wa kiume. Nchi ya Gileadi iligawanywa kwa kabila la Manase lililosalia.
7 默納協的地界,是從阿協爾起,到舍根對面的米革默塔特,再折向南,直達雅史布和恩塔普亞。
Eneo la Manase lilianzia Asheri hadi Mikimethathi, ambayo iko mashariki mwa Shekemu. Kisha mpaka ulienda upande wa kusini kwa wale walioishi karibu na chemichemi ya Tapua.
8 普亞地歸默納協,但默納協邊界上的特普亞城,卻屬厄弗辣因子孫。
( Nchi ya Tapua ilikuwa ni miliki ya Manase, lakini mji wa Tapua katika mpaka wa Manase ilikuwa ni mali ya kabila la Efraimu.)
9 邊界由此向下伸至卡納谷;谷南的成市屬厄弗辣因,是厄弗辣因在默納協城市所有的城市。默納協的境界是由谷北,直到大海。
Kisha mpaka ulishuka kuelekea kijito cha Kana. Miji hii kusini mwa kijito miongoni mwa miji ya Manase ilikuwa ni mali ya Efraimu. Mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa kijito, na ulikomea katika
10 南面屬厄弗辣因,北面屬默納協,以海為界;北接阿協爾,東部鄰依撒加爾。
bahari. Na nchi iliyokuwa upande wa kusini ilikuwa ni ya Efraimu, na nchi iliyo upande wa Kasikazini ilikuwa ni ya Manase; bahari ilikuwa ndoi mpaka. Kwa upande wa kaskazini ulifika hata Asheri, na upande wa mashariki, Isakari.
11 默納協在依撒加爾和阿協爾境內,有貝特商和所屬村鎮;依貝肋罕和所屬村鎮,多爾居民和所屬村鎮,還有恩多爾居民和所屬村鎮,塔納客居民和所屬村鎮,默基多居民和所屬村鎮,共三區。
Pia katika Isakari na katika Asheri, Manase alimiliki Bethi Shani na vijiji vyake, Ibleamu na vijiji vyake, wenyeji wa Dori na vijiji vyake, wenyeji wa Endori na vijiji vyake, wenyeji wa Taanaki na vijiji vyake, na wenyeji wa Megido na vijiji vyake (na mji wa tatu ni Nafethi).
12 但是默納協子孫未能將這些城中的土人趕走,客納罕人仍然居住在這地區內。
Lakini kabila la Manase halikuweza kuimiliki miji hiyo, kwa kuwa Wakanaani waliendelea kuishi katika nchi hii.
13 當以色列子民強冊盛以後,迫使客納罕人做苦工,卻沒有將他們完全趕走。
Hata wakati watu wa Israeli walipopata nguvu zaidi, hawakuwafukuzia mbali kabisa Wakanaani, bali waliwafanya kuwa watumwa.
14 若瑟的子孫對若蘇厄說:「上主這樣祝福我們,我們又是人數最多的一族,你為什麼只叫我們抽一籤,分一份土地作產業呢﹖
Kisha wazawa wa Yusufu wakamwambia Yoshua, wakisema, “Kwanini umetupa mgao mmoja wa nchi na sehemu moja kwa ajili ya urithi, kwa kuwa tuko wengi, na kwa muda wote Yahweh umetubaliriki?
15 若蘇厄對他們說:「如果你們人數眾多,厄弗辣因為你們太癥狹小,可甘培黎齊人和勒法因人的地方去,砍伐森林中的樹木。」
Yoshua akawaambia, “Kama ninyi ni watu wengi katika hesabu, pandeni ninyi wenyewe katika msitu na kuisafisha nchi kwa ajili yenu wenyewe katika nchi ya Waperizi na ya Refaimu. Fanyeni hivi kwa kuwa nchi ya milima ya Efraimu ni ndogo kwenu.”
16 若瑟的子孫回答說:「這山區為我們仍不夠,何況住在盆地,即住在貝特商和所屬村鎮,以及住在依次勒耳盆地的一切客納罕人,都擁有鐵車。」
Wazawa wa Yusufu wakasema, “Nchi ya milima haitutoshi. Lakini Wakanaani wote wanaoishi katika bonde wana magari ya chuma, wote walio katikaBethi Shani na vijiji vyake, na wale walio katika bonde la Yezreeli.”
17 若蘇厄對若瑟家,即對厄弗辣因和默納協人說:「你們人數眾多,勢力強大,不能只抽一籤,
Kisha Yoshua akawaambi nyumba ya Yusufu, ambao ni Efraimu na Manase, “Ninyi ni watu mlio wengi katika hesabu, na mna nguvu kubwa. Hamtakiwi kuwa na sehemu moja ya nchi mliogawiwa.
18 因此,山地也應歸於你們;那裏雖是森林,盡可砍伐,開闢的土地自然歸於你們。客納罕人雖然擁有鐵車,勢力強大,但你們必能將他們趕走。」
Nchi ya milima itakuwa yenu pia. Ingawa ni msitu, mtaufyeka na kuimiliki hata mipaka yake ya mbali. Mtawafukuzia mbali Wakanaani, ingawa wanayo magari ya chuma na ingawa pia wanazo nguvu.”

< 約書亞記 17 >