< 約書亞記 15 >

1 猶大支派的子孫按照家族,抽籤分得的土地是在極南部,以厄東邊境為界,南至親曠野。
Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea ukoo kwa ukoo, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini.
2 南方的邊界起自鹽海頂端,即海灣南端,
Mpaka wao wa kusini ulianzia kwenye ghuba iliyoko kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi,
3 沿阿刻辣賓山坡之南,經親曠野,上至卡德士巴爾乃亞之南,再由此經過赫茲龍,上至阿達爾,再繞過卡爾卡,
ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini ukaenda hadi kusini mwa Kadesh-Barnea. Tena ukapitia Hesroni ukapanda hadi Adari na ukapinda hadi Karka.
4 穿過阿茲孟直到埃及小河,而後廷至大海:以上是他們南方的邊界。
Kisha ukaendelea mpaka Azmoni na kuunganika na Kijito cha Misri, na kuishia baharini. Huu ndio mpaka wao wa upande wa kusini.
5 東方的邊界是起自鹽海直到約旦河口;北方的是起自約旦河口的海灣,
Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi ukienea mahali Mto Yordani unapoingilia. Mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia penye ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia,
6 上至貝特曷革拉,經過貝特阿拉巴北部,上至勒烏本人波罕的盤石;
ukapanda hadi Beth-Hogla, na kuendelea kaskazini mwa Beth-Araba hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni.
7 再由此上至德彼爾,沿阿苛爾山谷,往北轉向位於谷南的阿杜明山坡對面的革里羅特,再經默士水泉,直到洛革耳泉。
Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na materemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli.
8 以後再由此由本希農山谷而上,直達耶步斯,即耶路撒冷的南側,再上至俯視本希農山谷西方的山頂,這山位於勒法因平原的北端。
Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai.
9 再由這山頂轉向乃費托亞水泉,直到厄斐龍山,然後轉向巴阿拉,──即克黎雅特耶阿陵。
Kutoka juu ya kilima mpaka ule ukaendelea hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa, ukatokea kwenye miji ya Mlima Efroni na kuteremka kuelekea Baala (yaani Kiriath-Yearimu).
10 再從巴阿拉向西折向肥依爾山,繞過耶阿陵即革撒隆山脊北部,下至貝特舍默士,經過提默納,
Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna.
11 直至厄刻龍山脊北部,再繞過史加龍,經巴阿拉山,直到雅貝乃耳,最後至海為止。
Ukaelekea hadi kwenye mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini.
12 西方的邊界以大海海濱為界:以上是猶大子孫按照家族所分得的地區四周的邊界。
Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu. Hii ndiyo mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao.
13 若蘇厄遵照上主的吩咐,將猶大子孫中的一部分土地,即克黎雅特阿爾巴,分給了耶孚乃的兒子加肋布。阿爾巴是阿納克的祖先,阿爾巴即是赫貝龍。
Kwa kufuata maagizo ya Bwana kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki).
14 加肋布從那裏趕走了阿納克的三個子孫:舍瑟、阿希曼和塔爾耳買;他們是阿納克的後代。
Kutoka Hebroni Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki.
15 加肋布又從那裏上去,攻打了德彼爾固民。──德彼爾以叫克黎雅特色費爾。
Kutoka hapo akaondoka kupigana dhidi ya watu walioishi Debiri (jina la Debiri hapo kwanza uliitwa Kiriath-Seferi).
16 加肋布說:「誰能征服或拿下克黎雅特色費爾,我便將我的女兒阿革撒給他為妻。」
Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayeweza kupigana na kuteka Kiriath-Seferi.”
17 加肋布的弟兄,刻納次的兒子敖特尼奪下了那城,加肋布便將自己的女兒阿革撒給他為妻。
Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, akauteka; hivyo Kalebu akamtoa Aksa binti yake aolewe naye.
18 阿革撒快門的時候,丈夫勸她向她的們父親要求一塊田地。阿革撒一下驢,加肋布便向她說:「妳要﹖」什麼
Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka juu ya punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?”
19 阿革撒答說:「請你給我一件禮物;即要把我安放在南方的旱地,求你也將水泉給我。」她的父親就把上泉和下泉賜給了她。
Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini.
20 以下是猶大支派子孫.按照家族分得的產業:
Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo:
21 猶大支派子孫在乃革布與厄東交界的城市,有卡貝責耳、阿辣得、雅古爾、
Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa: Kabseeli, Ederi, Yaguri,
22 克納狄摩納、阿爾阿辣。
Kina, Dimona, Adada,
23 刻德士、哈祚爾、依特南、
Kedeshi, Hazori, Ithnani,
24 齊弗、特冷、貝阿羅特、
Zifu, Telemu, Bealothi,
25 哈祚爾哈達大、克黎約特赫茲龍──祚爾加達、即哈祚爾、
Hazor-Hadata, Kerioth-Hezroni (yaani Hazori),
26 阿曼、舍瑪、摩拉達、
Amamu, Shema, Molada,
27 哈匝爾加達、赫士孟、貝特培肋特、
Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti,
28 哈匝爾叔阿耳、貝爾舍巴及所屬村鎮、
Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia,
29 巴阿拉、依因、厄曾、
Baala, Iyimu, Esemu,
30 厄耳托拉得、革息耳、曷爾瑪、
Eltoladi, Kesili, Horma,
31 漆刻拉格、瑪德瑪納、桑森納、
Siklagi, Madmana, Sansana,
32 肋巴敖特、史耳新和恩黎孟:共計二十九座城巴和及所屬村鎮。
Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake.
33 在盆地有厄市陶耳、祚辣、阿市納、
Kwenye shefela ya magharibi: Eshtaoli, Sora, Ashna,
34 匝諾亞、恩加寧、塔普亞、厄南、
Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu,
35 雅爾慕特、阿杜藍、索苛、阿則卡、
Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,
36 沙阿辣因、阿狄塔殷、革德辣及革德洛塔殷:共計十四座城和所屬村鎮。
Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.
37 責南、哈達沙、米革達耳加得、
Senani, Hadasha, Migdal-Gadi,
38 狄耳罕、米茲培、約刻特耳、
Dileani, Mispa, Yoktheeli,
39 基士、波茲卡特、厄革隆。
Lakishi, Boskathi, Egloni,
40 加朋、拉赫瑪斯、基特里士、
Kaboni, Lamasi, Kitlishi,
41 革德洛特、貝特達貢、納阿瑪、瑪刻達:共計十六座座城和所屬村鎮。
Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake.
42 里貝納、厄特爾、阿商、
Libna, Etheri, Ashani,
43 依弗達、阿市納、乃漆布、
Yifta, Ashna, Nesibu,
44 刻依拉、阿革齊布、瑪勒沙:共計九座城和所屬村鎮;
Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake.
45 尚有厄刻龍和所屬城鎮。
Ekroni, pamoja na viunga vyake na vijiji vyake;
46 還有從厄刻龍到海,所有靠近阿市多得所屬村鎮。
magharibi ya Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake;
47 阿市多得所屬城鎮,直到埃及小河;並以大海為界
Ashdodi, miji yake na vijiji vyake na Gaza viunga vyake na vijiji vyake, hadi kufikia Kijito cha Misri na Pwani ya Bahari Kuu.
48 在山地有沙米爾,雅提爾、索苛、
Katika nchi ya vilima: Shamiri, Yatiri, Soko,
49 達納、克黎雅特色費爾,即德彼爾、
Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri),
50 阿納布、厄市特摩、阿寧、
Anabu, Eshtemoa, Animu,
51 哥笙、曷隆和基羅:共計十一座城所屬村鎮。
Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake.
52 阿辣布、、杜瑪、厄商、
Arabu, Duma, Ashani,
53 雅農、貝特塔普亞、阿費克、
Yanimu, Beth-Tapua, Afeka,
54 胡默達、克黎雅特阿爾巴,即赫貝龍和漆敖爾:共計九座城所屬村鎮。
Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake.
55 瑪紅、加爾默爾、齊弗、猶他、
Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,
56 依次勒耳、刻約德罕、匝諾亞、
Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,
57 卡因、基貝亞、提默納:共計十座城所屬村鎮。
Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake.
58 哈耳胡耳、貝特族爾、革多爾、
Halhuli, Beth-Suri, Gedori,
59 瑪阿辣特、貝特阿諾特、厄耳特孔:共計六座城所屬村鎮。特科亞、厄弗辣大即白冷、培敖爾、厄堂、谷隆、塔堂、索勒、加倫、加林、貝特爾、瑪納:共計十一座城所屬村鎮。
Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake.
60 尚有克黎雅特巴爾即克黎雅特耶阿陵和阿辣巴兩座城,所屬村鎮。
Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake.
61 在曠野有貝特阿辣巴、
Huko jangwani: Beth-Araba, Midini, Sekaka,
62 尼貝商、監城和恩革狄:共計六座城所屬村鎮。
Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake.
63 至於住在耶路撒冷的耶步斯人,猶大人不能將他們趕走,因此耶步斯人直到今日,仍同猶大人一起住在耶路撒冷。
Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, waliokuwa wakiishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.

< 約書亞記 15 >