< 約書亞記 11 >

1 哈祚爾王雅一聽見這事,便派人去見瑪冬王,史默龍王,阿革沙夫王,
Basi ikawa aliposikia haya, Yabini, mfalme wa Hazori, alituma ujumbe kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme Shimroni, na kwa mfalme wa Akshafu.
2 和住在北方山區,基乃勒特南方平原低地,和西方的多爾高原諸王;
Alituma pia ujumbe kwa wafalme walikuwa katika mlima wa kaskazini mwa nchi, katika bonde la Mto Yordani kusini mwa Kinerethi, katika nchi za tambarare, na katika nchi za milima ya Dori kuelekea magharibi.
3 又去見東西各地的客納罕人、阿摩黎人、希威人、培黎齊人,以及住在山區的耶步斯人,和赫爾孟山麓米茲帕地方的赫特人。
Pia, alituma ujumbe kwa Wakanaani walioko mashariki na magharibi, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wayebusi katika nchi za milima, na Wahivi karibu na Mlima Hermoni katika nchi ya Mizipa.
4 他們都帶領自己所有的軍隊和車輛。
Maadui zao wote walitoka pamoja nao, wanajeshi wengi sana, hesabu yao ilikuwa kama mchanga wa pwani. Walikuwa na farasi wengi sana na magari.
5 這些王子都合一起來,來到默龍水邊紮營,要同以色列人交戰。
Wafalme wote hawa walikutana katika muda waliokuwa wameupanga, na walipiga kambi katika maji ya Meromu ili kupigana vita na Israeli.
6 上主對若蘇厄說:「在這些人面前,你不要害怕,因為明天這時,我必要使他們全在以色列人面前被殺;你要砍斷他們的馬蹄筋,火燒他們的車輛。」
Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiogope mbele zao, kwa kuwa muda kama huu kesho ninawatia hao kwa Waisraeli wakiwa wafu. Utaivunja vunja miguu ya farasi zao, na utayachoma moto magari yao.”
7 若蘇厄遂率領自己的軍民突至默龍水旁,向他們進攻。
Yoshua na watu wote wa vita walitoka na mara wakafika katika maji ya Meromu, na wakawashambulia maadui.
8 上主將他們交在以色列人手中,以色列人擊殺他們,往西直追到大漆冬和米斯勒佛特瑪殷,往東直追到米茲帕山谷,將他們殺得沒有剩下一個。
Yahweh akawatia maadui katika mkono wa Israeli, na waliwapiga kwa upanga na wakawafuata mpaka Sidoni, Misrefothi - Maimu, na katika bonde la Mizipa upande wa mashariki. Waliwaua wote hakuna hata mmoja aliyeachwa hai.
9 若蘇厄便照上主指示他的,對待了他們,砍斷了他們的馬碲筋,火燒了他們的車輛。
Yoshua aliwatendea kama vile Yahweh alivyomwambia. Alivunja miguu ya farasi na magari aliyachoma moto.
10 若蘇厄班師回來時,奪取了哈祚爾,用刀斬了哈祚爾王。──原來哈祚爾以前是這些王國的都城。
Kwa wakati huo, Yoshua alirudi na akauteka mji wa Hazori. Alimwua mfalme wake kwa upanga (Hazori ulikuwa ni kichwa cha falme hizi zote).
11 又將城內的一切生靈,用刀殺死,完全予以毀滅,沒有留下一個生靈,以後放火燒了哈祚爾城。
Waliwapiga kwa upanga kila kiumbe chenye uhai kilichokuwa huko, na alivitenga ili viteketezwe, hivyo hapakuwa na kiumbe hai kilichoachwa hai. Na kisha aliuchoma moto Hazori.
12 若蘇厄奪取了那些王子的一切城邑,生摛那些王子,用刀將他們殺死,將城池完全予以毀滅,全照上主的僕人梅瑟所吩咐的。
Yoshua aliiteka miji yote ya wafalme hawa. Aliwateka pia wafalme wake wote na akawapiga wote kwa upanga. Aliwateketeza kabisa kwa upanga, kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyoagiza.
13 至於那些處於土丘上的城市,除哈祚爾外,以色列人都沒有焚毀:若蘇厄只燒了哈祚爾。
Waisraeli hawakuchoma moto mji wowote miongoni mwa miji iliyojengwa juu ya vilima vya vifuasi vya udongo, isipokuwa Hazori, ndio mji pekee ambao Yoshua aliuchoma kwa moto.
14 那些城中所有的財物和牲畜,以色列人都搶了來,歸為己有:所有的人都用刀殺死,完全予以毀滅,沒有留下一個生靈。
Jeshi la Israeli lilichukua nyara kutoka katika miji pamoja na mifugo kwa ajili yao wenyewe. Waliua kila mtu kwa upanga hadi pale walipokufa wote. Hakuna kiumbe hai kilichoachwa hai.
15 上主怎樣吩咐衪的僕人梅瑟,梅瑟也怎樣吩咐了若蘇厄,若蘇厄也就怎樣辦了。凡上主吩咐梅瑟的事,若蘇厄沒有不照辦的。
Kama vile Yahweh alivyomwagiza mtumishi wake Musa, na kwa namna hiyo hiyo, Musa alivyomwagiza Yoshua. Na katika mambo yote ambayo Yahweh alimwamuru Musa kuyafanya, Yoshua hakuacha kufanya hata jambo moja.
16 這樣,若蘇厄佔領了那整個地區:包括山地,整個南方,哥笙全境,平原,阿辣巴原野,以色列山地和附近平原,
Yoshua alitwaa nchi hiyo yote, nchi ya milima, Negevu yote, nchi yote ya Gosheni, nchi ya vilima vidogo, bonde la Mto Yordani, nchi ya milima ya Israeli, na nchi tambarare.
17 由上色依爾去的哈拉克山起,一直到赫爾孟山麓,黎巴嫩山谷間的巴爾加得:各城的王子都被生摛,都被殺死。
Kutoka Mlima Halaki karibu na Edomu, kuelekea kasikazini hadi Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni chini ya Mlima Hermoni, aliwateka wafalme wake wote na kuwaua.
18 若蘇厄同這些王子交戰,時日頗為長久,
Yoshua alipigana vita na wafalme wote kwa muda mrefu.
19 因為除住在基貝紅的希威人外,沒有一座城願與以色列子民媾和,都是以色列人用武力攻取的。
Hakuna hata mji mmoja uliofanya amani na jeshi la Israeli isipokuwa Wahivi walioishi Gibeoni. Israeli ilitwaa miji yote iliyosalia katika vita.
20 原來這是上主的意思,叫他們心硬,來與以色列人交戰,好使他們遭受無情的毀滅,澈底的破壞,正如上主對梅瑟所吩咐的
Kwa kuwa alikuwa ni Yahweh ambaye alikuwa ameifanya kuwa migumu mioyo yao ili wapande na kufanya vita dhidi ya Israeli, ili kwamba aweze kuwaangamiza kabisa, na kutowaonesha huruma, kama alivyomwaagiza Musa.
21 以後若蘇厄出兵,消滅了赫貝龍、德彼爾、阿納布山地、猶大山地和以色列山地所有的阿納克人,毀滅了他們和他們所有的城市。
Kisha Yoshua akaja kwa wakati ule na aliiangamiza Anakimu. Aliyafanya haya katika nchi ya milima, huko Hebroni, Debiri, Anabu, na katika nchi yote ya Yuda, na katika nchi yote ya milima ya Israeli. Yoshua aliwaangamiza kabisa pamoja na miji yao.
22 這樣以色列子民境內,沒有剩下一個阿納克人,只在迦薩、加特和阿布多得還有。
Hakuna hata mmoja wa watu wa Anakimu aliyeachwa katika nchi ya Israeli, isipokuwa huko Gaza, Gathi na Ashidodi.
23 若蘇厄佔領了那整個地區,全如上主對梅瑟所說的;若蘇厄遂將這地區按照以色列支派分給他們作產業。以後國內昇平,再無戰事。
Hivyo Yoshua aliiteka nchi yote, kama vile Yahweh alivyomwambia Musa. Yoshua aliwapa Israeli kama urithi, kila kabila lilipewa sehemu yake. Kisha nchi ikapumzika bila vita.

< 約書亞記 11 >