< 約伯記 1 >
1 從前在胡茲地方,有一個人名叫約伯,為人十全十美,生性正直,敬畏天主,遠離邪惡。
Kulikuwa na mtu katika nchi ya Usi jina lake Ayubu; na Ayubu alikuwa mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na
uovu. Wakazaliwa kwake watoto saba wa kiume na mabinti watatu.
3 家畜有七千隻羊,三千駱駝,五百對牛,五百母驢,且有很多僕人。此人是當時東方人民中最偉大的人物。
Alimiliki kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia moja za maksai, na punda mia tano na idadi kubwa ya watumishi. Mtu huyu alikuwa mtu mkuu wa watu wote wa mashariki.
4 他的每個兒子,按日輪流在家中設宴,且派人邀請他們的三個姊妹來一同宴飲。
Kwa siku yake kila mtoto wa kiume, hufanya karamu katika nyumba yake. Wakatuma na kuwaita dada zao watatu waje kula na kunywa pamoja nao.
5 及至宴飲的日子輪流一週,約伯總是派人召集他們來聖潔他們,清早起來照子女的數目,獻上全燔祭品說:「恐怕我的兒子犯了罪,心中詛咒了天主。」約伯常常如此行事。
Baada ya siku za karamu zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao na kuwatakasa. Aliamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa kila mtoto wake, kwa kusema, “Yawezekana kwamba wanangu wamefanya dhambi na kumkufuru Mungu mioyoni mwao.” Siku zote Ayubu alifanya hivi.
6 有一天,天主的眾子都來侍立在上主面前,撒殫也夾在他們當中。
Kisha ilikuwa siku ambayo watoto wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA. Shetani pia akaenda pamoja nao.
7 上主問撒殫說:「你從那裏來﹖」撒殫回答上主說:「我走遍了世界,周遊了各地回來。」
BWANA akamuuliza Shetani, “Umetoka wapi wewe?” Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, “Natoka kuzunguka zunguka duniani, kutembea huku na huko humo.”
8 上主對撒殫說:「你曾留心注意到我的僕人約伯沒有﹖因為世上沒有一個像他那樣十全十美,生性正直,敬畏天主,遠避邪惡的人。」
BWANA akamuuliza Shetani, “Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hakuna mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mwenye haki na mkamilifu, mmoja aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu.”
9 撒殫回答上主說:「約伯那裏是無緣無故敬畏天主的呢﹖
Kisha Shetani akamjibu BWANA na kusema, “Je Ayubu amcha Mungu bila sababu?
10 你不是四面保護他、他的家庭和他所有的一切麼﹖並且凡是他親手做的,你都祝福了;你使他的牲畜在地上繁殖增多。
Wewe hukumwekea kinga pande zote, kuzunguka nyumba yake, na kuzunguka vitu vyote alivyo navyo kutoka kila upande? Wewe umebariki kazi za mikono yake, na mifugo yake imeongezeka katika nchi.
11 但是你若伸手打擊他所有的一切,他必定當面詛咒你。」
Lakini sasa nyosha mkono wako na uguse yote hayo aliyonayo, na uone kama hatakufuru mbele ya uso wako.”
12 上主對撒殫說:「看,他所有的一切,都隨你處理,只是不要伸手加害他的身體。」撒殫遂離開天主走了。
BWANA akamwambia Shetani, “Tazama, hayo yote aliyonayo yamo mkononi mwako. Isipokuwa juu yake yeye mwenyewe usinyoshe mkono wako.” Kisha Shetani akatoka mbele za BWANA.
13 有一天,他的兒子同他的女兒,正在長兄家裏歡宴飲酒的時候,
Ilitokea siku moja, wana wake wa kiume na binti zake walipokuwa wakila na kunywa mvinyo nyumbani mwa ndugu yao mkubwa.
14 有個帶信的人跑來向約伯說:「牛正在耕田,母驢在一旁吃草的時候,
Mjumbe akamfikia Ayubu na kusema, “Hao maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakichunga karibu nao.
15 舍巴人突然闖來將牲口搶了去,用刀將那些僕人殺了,只有我一人逃脫,來向你報告。」
Waseba wakawaangukia na kutoweka nao. Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.”
16 這人還在報告時,另一個人跑來說:「天主的火由天降下,將羊群和僕人都燒死了,只有我一人逃脫,來向你報告。」
Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, “Moto wa Mungu umeanguka toka mbinguni na kuwateketeza kondoo na watumishi. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.”
17 這人還在報告時,另一個人跑來說:「加色丁人分成三隊闖入駱駝群,將駱駝搶走了,用刀將僕人殺了,只有我一人逃脫,來向你報告。」
Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, “Wakaldayo walifanya vikundi vitatu, wakawashambulia ngamia, na kuondoka nao. Kwa wale watumishi, wamewaua kwa makali ya upanga. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.”
18 這人還在報告時,另一個人跑來說:「你的兒女正在長兄家宴飲的時候,
Wakati alipokuwa akiendelea kusema, akatokea mwingine pia na kusema, “Wana wako wa kiume na binti zako walikuwa wakila na kunywa mvinyo nyumbani mwa ndugu yao mkubwa.
19 忽然從曠野那邊吹來一陣颶風,颳倒了房屋的四角,壓死了你的孩子,只有我一人幸免,來向你報告。」
Upepo wenye nguvu ulitokea jangwani na ukapiga pembe nne za nyumba. Ikawaangukia vijana hao, na wakafa wote. Mimi pekee nimeokoka kukuletea habari.
20 約伯就起來,撕裂了自己的外氅,剃去頭髮,俯伏在地叩拜,
Kisha Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, akanyoa kichwa chake, akaanguka chini kifudifudi na kumwabudu Mungu.
21 說「我赤身脫離母胎,也要赤身歸去;上主賜的,上主收回。願上主的名受到讚美! 」
Akasema, “Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu ni uchi, nami nitakuwa uchi wakati nitakaporudi huko. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa. Jina la BWANA libarikiwe.”
22 就這一切事而論,約伯並沒有犯罪,也沒有說抱怨天主的話。
Katika mambo hayo yote, Ayubu hakutenda dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa uovu.