< 約伯記 8 >
Kisha Bildadi Mshuhi akajibu:
2 這些話你要講到幾時﹖你口中的話像狂風要到何時﹖
“Hata lini wewe utasema mambo kama haya? Maneno yako ni kama upepo mkuu.
Je, Mungu hupotosha hukumu? Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?
4 若你的子女得罪了他,他必將他們交於罪過的權勢下。
Watoto wako walipomtenda dhambi, aliwapa adhabu ya dhambi yao.
Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi,
6 你若純潔正直,他必親來守護你,恢復你正義的居所。
ikiwa wewe ni safi na mnyofu, hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, na kukurudisha katika mahali pako pa haki.
Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo, lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.
“Ukaulize vizazi vilivyotangulia na uone baba zao walijifunza nini,
9 因為我們由昨日纔有,本來一無所知;我們在世上的日月,好似影子。
kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote, nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.
Je, hawatakufundisha na kukueleza? Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?
11 蒲草不在池沼內,怎能長大﹖蘆葦沒有水,怎會長起﹖
Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope? Matete yaweza kustawi bila maji?
Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa, hunyauka haraka kuliko majani mengine.
13 凡忘記天主的,他的末路也是這樣:惡人的希望必化為泡影。
Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.
Lile analolitumainia huvunjika upesi; lile analolitegemea ni utando wa buibui.
15 他倚恃自己的家,但它卻站立不住;他要依附自己的住所,住所卻不能久存。
Huutegemea utando wake, lakini hausimami; huungʼangʼania, lakini haudumu.
Yeye ni kama mti ulionyeshewa vizuri wakati wa jua, ukieneza machipukizi yake bustanini;
huifunganisha mizizi yake kwenye lundo la mawe, na kutafuta nafasi katikati ya mawe.
18 若有人從原處把它拔除,那地必否認說:「我未曾見過它。」
Unapongʼolewa kutoka mahali pake, ndipo mahali pale huukana na kusema, ‘Mimi kamwe sikukuona.’
Hakika uhai wake hunyauka, na kutoka udongoni mimea mingine huota.
20 天主決不棄捨完善的人,也決不支持惡人的勢力。
“Hakika Mungu hamkatai mtu asiye na hatia, wala kuitia nguvu mikono ya mtenda mabaya.
21 你的口角必再洋溢著喜悅,你的唇邊必再充滿歡笑。
Bado atakijaza kinywa chako na kicheko, na midomo yako na kelele za shangwe.
Adui zako watavikwa aibu, nazo hema za waovu hazitakuwepo tena.”