< 約伯記 21 >

1 約伯回答說:
Kisha Ayubu akajibu na kusema,
2 你們且聽一聽我的話! 這也算是你們給我的安慰。
“Sikilizeni hotuba yangu kwa makini, hii na iwe faraja yenu.
3 請讓我發言,我說完後,任你們笑罵。
Nimeteswa, lakini pia nitasema; nikisha kusema, endeleeni kudhihaki.
4 我豈是抱怨人﹖我失了忍耐,難道沒有理由﹖
Lakini kwangu mimi, malalamikio yangu ni kwa mtu? Kwa nini nisiwe mwenye subira?
5 你們注意聽我,必要吃驚,且要用手堵住口。
Nitazameni na mshangae, nanyi wekeni mkono wenu midomoni mwenu.
6 甚至我一回想,我就恐怖,全身戰慄。
Ninapoyafikiria mateso yangu, ninaumizwa, mwili wangu unaogopa.
7 惡人為何享受高壽而勢力強大﹖
Kwa nini waovu wanaendelea kuishi, wanazeeka, na kuwa na uwezo katika madaraka?
8 他們在世時,子孫昌盛,親眼看見子子孫孫。
Wazao wao wanathibitishwa mbele zao, na uzao wao unaimarika machoni pao.
9 他們的住宅平安,無所畏懼,天主的棍杖也不加在他們身上。
Nyumba zao ziko salama mbali na hofu; wala fimbo ya Mungu haiko juu yao.
10 他們的公牛交尾,無不成功;母牛產子,決無流產。
Dume lao la ng'ombe linazalisha; halishindwi kufanya hivyo; ng'ombe wao anazaa na hafishi ndama wake akiwa mchanga.
11 他們使孩子跑出像羊群,子女跳躍如麋鹿。
Wanawapeleka wadogo wao kama kundi la kondoo, na watoto wao hucheza.
12 他們伴著手鼓與豎琴歌唱,隨著笛聲歡呼。
Wanaimba kwa tari na vinubi na hufurahi kwa muziki na zomari.
13 他們幸福地度過天年,平安地降入陰府。 (Sheol h7585)
Wanatumia siku zao katika mafanikio, na wanashuka kuzimu kwa utulivu. (Sheol h7585)
14 但他們曾向天主說:「離開我們! 我們不願知道你的道路。
Wanamwambia Mungu, 'Ondoka kwetu kwani hatutaki ufahamu wowote juu ya njia zako.
15 全能者是誰,竟叫我們事奉他﹖我們祈求他有什麼好處﹖」
Mwenye enzi ni nani, hata tumwabudu? Tutafaidika na nini tukimwabudu? Tutapata faida gani ikiwa tutamwomba?
16 看啊! 他們的幸福,豈不在他們掌握中﹖惡人的思想豈不離他很遠﹖
Tazama, je mafanikio yao hayamo katika mikono yao wenyewe? Sina cha kufanya na ushauri wa waovu.
17 惡人的燈有多少次熄滅過﹖災禍有多少次降在他們身上﹖天主何嘗因忿怒而消滅他們﹖
Mara ngapi taa za waovu huzimwa, au kwamba majanga huja juu yao? Mara ngapi inatokea kwamba Mungu husambaza huzuni kwao kwa hasira?
18 使他們好像被風吹的碎湝﹖好像被暴風捲去的糠秕﹖
Ni mara ngapi inatokea kwamba wanakuwa kama mabua mbele ya upepo au kama makapi yanayopeperushwa na dhoruba?
19 難道天主要向他的兒子討罪債﹖其實應向他本人報復,叫他覺悟!
Mnasema, 'Mungu huweka hatia ya mtu kwa watoto wake kuilipa.' Na alipe yeye mwenyewe, ili kwamba aweze kujua hatia yake mwenyewe.
20 叫他親眼看見自己的毀滅,親自飲下全能者的義怒之杯。
Acha macho yake yaone uangamivu wake mwenyewe, na acha anywe gadhabu ya Mwenyezi.
21 他既逝去,他本人的歲月已絕,他的家庭對他還有什麼相干﹖
Kwani anaangaliaje familia yake mbele yake idadi ya miezi yake inapokwisha.
22 天主既審判天上者,人豈能教給他什麼智識﹖
Je kuna mtu anaweza kumfundisha Mungu maarifa kwa kuwa yeye huwaukumu hata walio juu?
23 有人到死一無所缺,享盡了平安幸福。
Mtu mmoja ufa katika nguvu zake kamili, akiwa na utulivu kabisa na kwa amani.
24 他的腰部充滿脂肪,他的骨髓潤澤豐盈;
Mwili wake hauna uhitaji, na kiini cha mifupa yake ina unyevu na afya njema.
25 但有人卻至死心靈酸苦,一生毫無福樂;
Mtu mwingine ufa kwa uchungu wa nafsi, bila kujifurahisha kwa jambo lolote jema.
26 他們卻一同埋於塵土,為蛆蟲所掩蓋。
Wanazikwa kaburini wote kwa pamoja, funza wanawafunika wote.
27 我確知你們的思想,以及對我所籌劃的陰謀。
Tazama, nayajua mawazo yenu, na jinsi mnavyotaka kunikosesha.
28 你們要問:「霸王的家在那裏﹖惡人住的帳幕在何處﹖」
Kwa kuwa mwasema, 'Iko wapi sasa nyumba ya mwana wa mfalme? Liko wapi kao alipokaa mwovu?'
29 你們怎麼不問過路的人﹖難道你們不承認他們的證據﹖
Je hamjawauliza wasafiri? Hamfahamu wanavyoweza kusema,
30 「惡人在毀滅之日不受害,在憤怒之日會得救。」
kwamba mwovu anaepushwa na siku ya shida, na kwamba anawekwa mbali na siku ya gadhabu?
31 他的動作,誰敢當面指摘﹖他的行為,誰能報復﹖
Ni nani atakaye ituhumu siku ya mwovu mbele yake? Ni nani atakayemwadhibu kwa alichokifanya?
32 他最後被抬入墳墓,且親自守護自己的墓地。
Hata hivyo atapelekwa kaburini; watu wataliona kaburi lake.
33 谷中的土壤,他感覺甘美;眾人都跟他而去,但在他前面的人,更不可勝數。
Udongo wa bondeni utakuwa mtamu kwake; watu wote watamfuata, hata kuwe na watu wengi mbele yake.
34 你們為何說空話來安慰我﹖你們的答話顯然只是欺詐!
Ni jinsi gani basi mtanifariji bila kufikiri, kwa kuwa majibu yenu hayana lolote ila uongo?”

< 約伯記 21 >