< 耶利米書 46 >
Hili ni neno la Yahwe lililomjia Yeremia nabii juu ya mataifa.
2 關於埃及:對於埃及王法郎乃苛,於猶大王約史的兒子約雅金第四年,在幼發拉的河附近的加克米士,被巴比倫王拿步高擊敗的軍隊:
Juu ya Misri; “Hili ni juu ya jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri aliyekuwako Karkemishi kando ya mto Frati. Hili ni jeshi alilolishinda Nebukadneza mfalme wa Babeli likishindwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:
Wekeni tayari ngao ndogo na kubwa, na msonge vitani.
4 騎士,你們應裝備戰馬,快騎上,戴上盔,磨快槍,披甲出陣!
Watieni farasi lijamu na hatamu, na mpande juu yao, ninyi wapanda farasi. Jiwekeni mahali penu, mkiwa mmevaa helmeti vichwani mwenu. Inoweni mishale yenu na kuvaa silaha zenu.
5 怎麼﹖我看見他們驚惶潰退,他們的勇士遭受襲擊,急速奔逃,不敢回顧,竟然恐怖四起﹖──上主的斷語。
Ninaona nini hapa? Wana woga na wanakimbia, maana askari wao wameshindwa. Wanakimbia kwa usalama na hawaangalii nyuma. Kitisho kipo mahali pote - hili ni tamko la Yahwe -
6 敏捷的不能逃脫,英勇的不能自救,在靠近幼發拉的河的北岸,瓦解覆滅!
wepesi hawawezi kukimbia, na askari hawezi kukwepa. Wana jikwaa kaskazini na kuanguaka kando ya mto Frati.
Ni nani hawa wainukao kama Nile, ambao maji yao yanaruka juu na chini kama mito?
8 埃及如尼羅,水波起伏如河流,湧上來說:「我湧上來淹沒大地,掃滅城市和城中的居民。
Misri huinuka kama mto Nile, na maji yake yanaumuka juu na chini kama mito. Anasema, 'nitapanda juu; nitaifunika nchi. Nitaiharibu miji na watu wake.
9 戰馬上前,戰車急馳,戰士出陣,持盾的雇士人和普特人,張弓的路丁人!
Inukeni, farasi. Mwe na hasira, ninyi vibandawazi. Askari na waende, Kushi na Putu, watu walio na ujuzi wa ngao, na Ludimu, watu wenye ujuzi wa kupiga pinde zao.
10 這一天正是我主萬軍的上主,報復自己仇敵的復仇日,刀劍必要吞噬、飽嘗、痛飲他們的鮮血;在靠近幼發拉的河北岸,我主萬軍的上主必要執行一場大屠殺。
Siku hiyo itakuwa siku ya kisasi kwa Bwana Yahwe wa majeshi, naye atajilipizia kisasa juu ya adui zake. Upanga utararua na kujirishisha. Utakula na kujishibisha kwa damu yao. Kwa maana kutakuwa na sadaka kwa Bwana Yahwe wa majeshi katika nchi ya kaskazini kando ya mto Frati.
11 埃及的處女! 你儘管上基肋阿得去拾取香草,只是徒然增添藥材;你已無法治療!
Panda Gileadi ujipatie dawa, binti wa Misri uliyebikra. Haifai kwamba unaweka dawa nyingi juu yako. Hakuna uponyaji kwako.
12 萬民聞知了你的羞辱,大地充滿了你的哀哭;噫! 勇士衝向勇士,雙方同時倒仆。
Mataifa wamesikia kuaibika kwako. Nchi imejawa na maombolezo yako, maana askari anajikwaa juu ya askari; na wote wawili uanguka pamoja.”
13 上主論及巴比倫王拿步高前來攻擊埃及地,對耶肋米亞先知說的話:
Hili ndilo neno Yahwe alilomwambia nabii Yeremia wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipokuja na kushambulia nchi ya Misri:
14 你們在埃及宣傳,在米革多耳傳報,在諾夫及塔黑培乃斯傳布說:你起來準備! 刀劍已在你四周撕殺。
Toa taarifa kwa Misri na isikiwe katika Migdoli na Memfisi. Wamesema katika Tapenesi, wekeni kituo na mwe imara, kwa maana upanga unakula wote kati yenu.
15 怎麼,阿丕斯逃跑了,你的牛神也站立不住﹖原來上主已將牠推倒。
Kwa nini Apisi mungu wenu amekimbia? Kwa nini ng'ombe dume mungu wenu hakuweza kusimama? Yahwe amemwangusha chini.
16 你的混合部隊已離心潰退,各向自己的同僚說:起來,回到我們的民族,我們的生身地去,遠避吞殺的刀劍!
Ameongeza idadi ya waliojikwaa. Kila askari anaanguka kinyume cha anayefuata. Wanasema, “Inuka. Haya twende nyumbani. Haya na turudi kwa watu wetu, katika nchi yetu ya asili. Na tuuache upanga huu unaotuuwa.”
17 人應給埃及王法郎起個綽號,叫「時機過後的叫囂。」
Walitangaza pale, “Farao mfalme wa Misri ni kelele tu, ameuacha wasaa wake mbali.”
18 我永在──那稱謂萬軍上主的君王的斷語──有一位必要前來,勢如群山中的大博爾,又如海濱的加爾默耳。
Kama niishivyo - hili ni tamko la mfalme - Yahwe wa majeshi kwa jina, kuna mtu atakuja aliye kama Mlima Tabori na Mlima Karmeli kando ya bahari.
19 寄居在埃及的女兒! 請你自備流徙的行裝,因為諾夫將要變為荒野,被火焚燒,再沒有人居住。
Wekeni masanduku yenu kuyachukua uhamishoni, binti mwishio Misri. Kwani Memfisi haitafaa, magofu. Hakuna atakayeishi huko.
20 埃及是一頭美麗的小母牛,但是有一隻牛蠅從北方向她撲來。
Misri ni mtamba mzuri sana, lakini mdudu aumaye anakuja kutoka kaskazini. Anakuja.
21 她的傭兵在她內雖像肥胖的牛犢,也一同轉身逃遁,不能抵抗,因為他們遭殃的日子,受罰的時期,已來到他們身上。
Askari wake wakukodiwa ni kama dume la ng'ombe lililonona kati yake. lakini wao pia watageuka na kukimbia. Hawatasimama pamoja, kwani siku yao ya madhara inakuja kunyume chao, wakatik wa kuadhibiwa kwao.
22 她發聲嘶嘶好像蛇行,因為敵人正在率軍前進,好像伐木的樵夫,帶著斧鉞向她衝來:
Misri anatoa sauti kama ya nyoka na kuondoka kwa kutambaa. maana adui yake anajiandaa kinyume chake. Wanamkabili kama mkata miti aliye na shoka.
23 砍伐她的森林──上主的斷語──雖然它稠密得不可侵入,因為他們多於蝗蟲,不可勝數。
Wataangusha misitu - japokuwa ni mingi sana - hili ni tamko la Yahwe. Kwa maana adui watakuwa wengi kuliko nzige, wasiohesabika.
Binti Misri ataaibishwa. Atawekwa mkononi mwa watu kutoka kaskazini.”
25 萬軍的上主,以色列的天主說:「看,我必懲罰諾地的阿孟,法郎和埃及,埃及的神祇和君王,以及信賴法郎的人,
Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema, “Tazama, niko karibu kumwadhibu Amoni wa Thebesi, Farao, Misri na miungu yake, Farao mfalme wake, na wote wanaomtumaini.
26 將他們交在圖謀他們性命的巴比倫王拿步高和他臣僕的手中;但是以後,埃及仍如昔日有人居住──上主的斷語。
Nitawaweka katika mkono wa wanaoyaona maisha yao, na katika mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli na watumishi wake. Kisha baada ya haya Misri itakaliwa kama mwanzo - asema Yahwe.”
27 至於你,我的僕人雅各伯,你不用害怕;以色列,你不必驚慌;因為,看,我必從遠方救出你來;從充軍之地,救出你的後裔;雅各伯必將歸來,居享安寧,無所恐懼。
Lakini, wewe Yakobo mtumishi wangu, usihofu. Usifadhaike, Israeli, maana tazama, nitakurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya mateka. Kisha Yakobo atarudi, tafuta amani, na kuwa salama, na hapatakuwa na wa kumwogofya.
28 雅各伯,我的僕人! 你不用害怕──上主的斷語──有我與你同在;誠然,對我使你流徙所至的各民族,我要加以毀滅;但是你,我必不毀滅,只依照正義懲罰你,不讓你全然免罰。
Wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope - asema Yahwe - kwa maana nipo nawe, hivyo nitaleta maangamizi makamilifu dhidi ya mataifa yote nilikokupeleka. Lakini sitakuharibu kabisa. Hata hivyo nitakuadhibu kwa haki na hakika sitakuacha bila adhabu.”