< 以賽亞書 51 >
1 你們追求正義,尋覓上主的人,請聽我說:你們又細察那巖石,你們是從那上邊鑿下來的;要細察那石穴,你們是從那裏挖出來的。
Nisikilizeni mimi, enyi mtendao haki, enyi mtafutaye Yahwe: Tazama katika mwamba uliouchonga nakuchimba kutoka pale ulipopakata.
2 你們要細察你們的父親亞巴郎和產生你們的撒辣,因為當我召叫他時,只有他一人,但我祝福了他,使他繁盛。
Mtazameni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa ninyi; maan alipokuwa na upweke yeye mwenyewe, Nilimuita yeye. Nikambariki yeye na kumfanya yeye kuwa wengi.
3 的確,上主必要憐憫熙雍,憐憫她所有的廢墟,使她的荒野成為伊甸,使她的沙漠變為上主的樂園,其中必有歡樂和愉快,歌頌和絃樂之聲。
Ndio, Yahwe ataifariji Sayuni; Ataifariji miji yake yote iliyo na ukiwa; jangwa lake atalifanya kama Edeni, na jangwa lililo wazi pembeni ya bonde la mto Yordani kama bustani ya Yahwe; Furaha na shangwe vitakuwa kwake, shukrani, na sauti ya kuimba.
4 萬民啊!請傾聽我;萬邦啊!請側耳聽我:法律將由我而出,我的正義要作為萬民的光明。
''Kuwa makini kwangu, watu wangu; na nisikilizeni mimi, watu wangu! Maana nitatoa amri, na nitaifanya haki yangu kuwa sheria ya mataifa.
5 我的正義要迅速降臨,我的救恩業已出現,我的手臂要掌管萬民;諸島嶼都仰望我,依賴我的手臂。
Haki yangu ipo karibu; wokovu wangu utaenda nje, na mikono yangu itahihukumu mataifa; Pwani itanisubiri mimi; maana wanashauku ya kuhusubiria mkono wangu.
6 你們仰觀諸天,俯察大地:縱然諸天將如煙雲消散,大地要像衣服破舊,地上的居民要如蚊子死去,然而我的救恩永遠常存,我的正義決不廢除。
Nyanyueni macho yanu juu angani, na tazama nchi chini, maana mbingu zitatoweka mbali kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, na wenyeji wake watakufa kama inzi. Lakini wokovu wangu utaendelea daima, na haki yangu haitaacha kutenda kazi.
7 你們認識正義,心懷法律的人民,請聽我說:不要怕人家的侮辱,對他們的嘲笑也不必驚恐;
Nisikizeni mimi, enyi mnaotambua ukweli, enyi watu wangu mliobeba sheria yangu katika mioyo yenu: Msiogope matusi ya watu, wala kukatishwa tamaa na unyanyasaji wao.
8 因為他們必如衣服一樣,為蠹蟲所吃掉;如羊毛一樣,為衣魚所吃掉;然而我的正義永遠常存,我的救恩直到萬世。
Maana Nonda watawala wao kama vazi, na minyoo itawala wao kama sufu; lakini haki yangu itakwa daima, na wokovu wangu katika vizazi vyote.''
9 上主的手臂!醒來,醒來!施展威能罷!醒來有如在古時古代一樣。不是你斬了辣哈布,刺殺了巨龍嗎﹖
Amka, amka, jivishe wewe mwenyewe kwa nguvu, mkono wa Yahwe. Amka kama siku za zamani, kizazi cha nyaktii za kale, Je sio wewe uliyeangamiza mnyama wa baharini, na uliyemchoma joka?
10 不是你令海令大洋的水涸竭了嗎﹖不是你使海底變為大路,叫蒙救的人走過嗎﹖
Je haukukausha bahari, maji ya kina kirefu, na kufanya kina cha bahari kuwa nija ya ukombozi kupita?
11 上主所解救的人必要歸來,快樂地來到熙雍,永久的歡樂將臨於他們頭上;他們將享盡歡欣與快樂,憂愁與悲哀必將遠遁。
Fidia ya Yahwe itarudi na kwenda Sayuni kwa kilio cha furaha na furaha ya milele itakuwa katika vichwa vyao, na huzuni na kuomboleza vitatoweka mbali.
12 是我,是我親自安慰了你,你怎麼還怕那有死的人,怕那命如草芥的人子呢﹖
''Mimi, mimi ndiye niwapae faraja. Kwa nini uwaogope watu, ambao wanakufa, watatoto wa wanadamu, waliofanywa kama majani?
13 你怎麼竟忘記了那創造你,展開諸天,奠定大地的上主,而終日不斷對那壓迫你,決意要消滅你的人的狂怒恐怖呢﹖如今壓迫你者的狂怒在那裏呢﹖
Kwa nini umemsahau Yahwe Muumba, yeye azinyooshayembingu na kuweka misingi ya nchi? Nyie ambao mna hofu za mara kwa mara kila siku kwa sababu ya hasira ya moto ya wanyanyasaji anapo fanya maamuzi ya kuangamiza. Iko wapi hasira ya wanyanyasaji?
14 囚禁的人即將釋放,不致死於深坑,他的口糧也不會缺乏。
Yeye aliyeinama chini, Yahwe atafanya haraka kumuachia; hatakufa wala kwenda chini katika shimo, wala hatakosa mkate.
15 我是上主你的天主,即那攪動海洋使浪濤澎湃的,他的名字是「萬軍的上主。」
Maana Yahwe Mungu wenu, anaye ifanya bahari itembee, hivyo mawimbi yake yavume kwa kishindo- Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
16 是我把我的話放在你的口中,將你掩護在我的手蔭之下;是我展開了諸天,奠定了大地,並給熙雍說:「你是我的百姓。」
Niweka maneno yangu mdomoni mwako, na nimekufunika wewe kwa kivuli cha mkono wangu, ili niweze kupanda mbingu, kuweka misingi ya nchi, na kutamkia Sayuni, 'ninyi ni watu wangu.''
17 起來,起來!耶路撒冷!立起來!你這由上主手中飲了他震怒之杯,啜盡了那麻醉爵中渣滓的!
Amka, amka, simama juu, Yerusalemu, ewe unyweae katika kikombe cha hasira ya Yahwe kutoka mkononi mwako; umekunjwa katika kikombe, kikombe cha mateso, na umekunjwa na kumaliza.
18 她所生的兒子中沒有一個來引領她的,她養大的兒子中沒有一個來扶持她手的。
Hakuna hata mmoja miongoni mwa watoto aliyewazaa wa kumuongoza yeye; hakuna hata mmoja miongoni mwa wote aliyewalea wa kumshika mkono wake.
19 這兩件事臨到了你身上,有誰哀憐你呢﹖就是荒涼與滅亡,饑饉與兵燹,有誰安慰你呢﹖
Shida hizi mbili ziliwatokea ninyi- ni nani atahuzunika pamja nanyi? - ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga. Ni nani atakayekufariji wewe?
20 你的兒子昏迷不醒,躺在街頭,像陷入羅網的羚羊;他們還飽嘗了上主的憤怒,受盡了你的天主的恐嚇。
Watoto wako walizimia; walilala kila kona ya mtaa, kama swala kwenye mtego; Wamejawa na hasira ya Yahwe, Laana ya Mungu wako.
21 為此,你這受苦難的,非因酒而醉倒的,請聽這事!
Lakini sasa sikiliza hili, ewe uliodhulumiwa na kulewa, lakini sio kwa mvinyo:
22 你的主宰上主,為自己的人民辯護的天主,這樣說:「看!我已從你手中取回了那麻醉的杯,我憤怒的爵,你必不再喝,
Bwana wenu Yahwe Mungu, anayewasihi watu wake, asema hivi, ''Tazama, Nimechukua kikombe cha ukubwa mkononi mwako- ukubwa wa kikombe cha hasira yangu - ili usiweze kunjwa tena.
23 我將此杯放在壓迫你者的手中,就是曾對你說:「躺下來!讓我們走過去!」你便使你的背脊作為平地,作為街道,任他們走過去的那些人。
Nitakuweka kwenye mikono ya watesaji, wale waliokuambia wewe, Lala chini, ili tutembee juu yako'; wameufanya mgongo wako kama uwanjwa na kama wao wa.''