< 何西阿書 6 >

1 「來,我們回到上主那裏去,因為衪撕碎了我們,也必要治愈;衪打傷了我們,也必要包紮。
“Njoo, turudi kwa Bwana. Kwa maana ametuvunja vipande vipande, lakini atatuponya; ametujeruhi, lakini atatufunga majeraha yetu.
2 兩天後衪必使田復生,第三天衪必使我們興起,生活在衪的慈顏下。
Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, na tutaishi mbele yake.
3 讓我們認識上主,讓我們努力認識上主! 衪定要像曙光一樣出現,衪要來到我們中間,有如秋雨,有如滋潤田地的春雨。」
Nasi tumjue Bwana; tukaendelee kumjua Bwana. Kuja kwake ni hakika kama asubuhi; atakuja kwetu kama mvua, kama mvua ya vuli ambayo huinyeshea ardhi.”
4 厄弗辣因,我可對你們作什麼﹖因為你們的仁愛有如旱晨的浮雲,有如易於消散的朝露。
Efuraimu, nikufanyie nini? Yuda, nikufanyie nini? Uaminifu wako ni kama wingu la asubuhi, kama umande unaoondoka mapema.
5 因此,我藉先知們砍伐了他們,以我口中的言語殺死戳了他們;我的的裁判出現有如光明:
Kwa hiyo nimewavunja vipande vipande kwa vinywa vya manabii, nimewaua kwa maneno ya kinywa changu. Maagizo yako ni kama nuru inayoangaza.
6 因為我喜歡仁慈勝過祭獻,喜歡人認識天主勝過全燔祭。
Kwa maana natamani uaminifu wala si dhabihu, na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
7 但是他們在阿當就犯了罪,在那裏已背叛了我。
Kama Adamu wamevunja agano; hawakuwa waaminifu kwangu.
8 基肋阿得是座作惡的城池,滿了血跡。
Gileadi ni jiji la wahalifu wenye miguu ya damu.
9 一隊司祭就如埋伏的強盜,在往舍根的路上行兇;的確,他們行了可恥的事
Kama makundi ya wanyang'anyi wanaomngojea mtu, hivyo makuhani hujiunga pamoja kufanya mauaji kwa njia ya Shekemu; wamefanya uhalifu wa aibu.
10 在貝特耳我見了可惡的事:在那裏厄弗辣因行了淫,以色列玷污了自己
Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo baya; Uzinzi wa Efraimu ukopale, na Israeli ametiwa unajisi.
11 當我轉變我百姓的命運時,猶大啊! 為你也注定了一個收割期。
Kwa maana wewe, Yuda, mavuno yameteuliwa, nitakaporudisha urithi wa watu wangu.

< 何西阿書 6 >