< 創世記 47 >

1 若瑟遂去呈報法郎說:「我父和我兄弟,帶著他們的牛羊和一切所有,從客納罕地來了,現今都在哥笙地方。」
Kisha Yusufu akaingia kwa Farao na kumwambia, “Baba yangu na ndugu zangu, kondoo wao, mbuzi wao, na yote waliyonayo, wamefika kutoka katika nchi ya Kanaani. Tazama, wapo katika nchi ya Gosheni.”
2 若瑟由他兄弟中選了五人,引他們去謁見法郎。
Akawachukua watano katika ndugu zake na kuwatambulisha kwa Farao.
3 法郎問若瑟的兄弟們說:「你們有何職業﹖」他們回答法郎說:「你的僕人們是放羊的人,我們和我們的祖先,都是如此。」
Farao akawambia ndugu zake, “Kazi yenu ni nini?” Wakamwambia Farao, “Watumishi wako ni wafugaji, kama mababu zetu.”
4 繼而又對法郎說:「我們來僑居此地,因為客納罕地饑荒很凶,你僕人們的羊群找不到草地,所以請陛下讓你的僕人們住在哥笙地方。」
Kisha wakamwambia Farao, “Tumekuja kukaa kwa muda katika nchi. Hakuna malisho kwa ajili ya makundi ya watumishi wako, kwa maana njaa ni kali sana katika nchi ya Kanaani. Hivyo, tafadhari waache watumishi wako wakae katika nchi ya Gosheni.”
5 法郎遂面對若瑟說:「你父親和你兄弟既來到了你這裏,
Kisha Farao akamwambia Yusufu, kusema, “Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako.
6 埃及國全在你面前,你可叫你父親和你兄弟住在最好的地方,叫他們住在哥笙地;你若知道他們中有能幹的可派他們管我的牲畜。」
Nchi ya Misri iko mbele yako. Mkalishe baba yako na ndugu zako katika eneo zuri, nchi ya Gosheni. Ikiwa unafahamu watu wenye uwezo miongoni mwao, uwaweke kuwatunza wanyama wangu.”
7 然後若瑟引他父親來謁見法郎;雅各伯向法郎請安。
Kisha Yusufu akamwingiza Yakobo baba yake na kumweka mbele ya Farao. Yakobo akambariki Farao.
8 法郎遂問雅各伯說:「請問高壽﹖」
Farao akamwambia Yakobo, “Umeishi kwa muda gani?”
9 雅各伯回答法郎說:「我寄居人世,已一百三十年;我一生歲月又少又苦,不會達到我祖先寄居人世的年數。」
Yakobo akamwambia Farao, “Miaka ya safari zangu ni mia moja na thelathini. Miaka ya maisha yangu imekuwa mifupi na ya maumivu. Siyo kama miaka ya baba zangu.”
10 雅各伯再向法郎請安,辭別法郎出來了。
Kisha Yakobo akambariki Farao na kuondoka mbele zake.
11 若瑟依照法郎的吩咐,給他父親和兄弟安排了住處,將埃及國辣默色斯境內最好的地方,給了他們作產業。
Kisha Yusufu akamweka baba yake na ndugu zake. Akawapa eneo katika nchi ya Misri, sehemu nzuri sana ya nchi, katika eneo la Ramesesi, kama Farao alivyokuwa ameagiza.
12 若瑟並按照他們的人口,供給他父親和兄弟以及他父親全部家屬的食糧。
Yusufu akamhudumia baba yake kwa chakula, ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake, kulingana na hesabu ya wahitaji wao.
13 那時因為饑荒十分嚴重,各地絕糧,連埃及國和客納罕地也因饑荒缺了糧。
Basi hakukuwa na chakula katika nchi yote; kwani njaa ilikuwa kali sana. Nchi ya Misri na nchi ya Kanaani ikaharibika kwa sababu ya njaa.
14 若瑟因售糧與民眾,將埃及國和客納罕地內所有的一切銀錢,都聚斂了來,將這些銀錢盡歸入法郎王室。
Yusufu akakusanya pesa yote iliyokuwa katika nchi ya Misri na nchi ya Kanaani, kwa kuwauzia wakaaji wake chakula. Kisha Yusufu akaleta ile pesa katika kasri la Farao.
15 當埃及國和客納罕地的銀錢都用盡了,埃及人前來見若瑟說:「銀錢已用完了,請給我們糧食,免得我們死在你面前! 」
Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha, Wamisri wote wakaja kwa Yusufu wakisema, “Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?”
16 若瑟回答說:「如果沒有銀錢,可將你們的家畜送來;我將糧食給你們,交換你們的家畜。」
Yusufu akasema, “Ikiwa pesa yenu imekwisha, leteni wanyama wenu nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu.”
17 他們遂將家畜送來,交給若瑟;若瑟便以糧食換取了他們的馬、牛、羊、驢;那一年人們就以所有的家畜,換糧食生活。
Hivyo wakaleta wanyama wao kwa Yusufu. Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi, kondoo, mbuzi na kwa punda. Akawalisha kwa mkate kwa kubadilisha na wanyama wao mwaka ule.
18 這一年過後,第二年他們又來見他說:「我們實不瞞我主,銀錢都用盡了,畜養的家畜也全歸了我主,在我主面前什麼也沒有了,只剩下了我們自身和我們的田地。
Mwaka ule ulipokwisha, wakaja kwake mwaka uliofuata na kumwambia, “Hatutaficha kwa bwana wangu kwamba pesa yetu yote imekwisha, na wanyama ni wa bwana wangu. Hakuna kilichobaki mbele za bwana wangu, isipokuwa miili yetu na nchi yetu.
19 為什麼要我們死在你面前﹖讓田地荒蕪呢﹖你用糧食收買我們和我們的田地罷! 好叫我們的田地都歸法郎作主。請給我們穀種,好叫我們生活,不致於死,田地也不致於荒蕪。」
Kwa nini tufe mbele za macho yake, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu badala ya chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumishi wa Farao. Tupe mbegu ili kwamba tuishi na tusife, na kwamba nchi isiwe tupu bila watu.
20 埃及人為饑荒所迫,人人出賣了自己的農田;若瑟遂為法郎購得了埃及所有的田地,田地遂盡歸法郎所有。
Hivyo Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri. Kwani kila Mmisri akauza shamba lake, kwa sababu njaa ilikuwa kali sana. Kwa njia hii, nchi ikawa mali ya Farao.
21 並使埃及境內的人民,從這邊直到那邊,都成了農奴;
Na watu, akawafanya kuwa watumwa kutoka mpaka mmoja wa Misri hata mkapa mwingine.
22 只有司祭的田地他沒有買得,因為司祭有得自法郎的常糧,可藉法郎賜與他們的常糧生活,所以沒有賣他們的田地。
Ilikuwa ni nchi ya makuhani pekee ambayo Yusufu hakuinunua, kwa maana makuhani walikuwa wakipewa posho. Walikula katika sehemu aliyowapa Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.
23 那時若瑟對人民說:「今天我將你們和你們的田地,都已買下歸於法郎,這裏有你們的穀種,你們拿去播種;
Kisha Yusufu akawambia watu, “Tazama, nimewanunua ninyi na nchi yenu leo kwa ajili ya Farao. Basi mbegu hii hapa kwa ajili yenu, nanyi mtapanda katika nchi.
24 到了收穫的時候,五分之一應歸法郎,其餘四分歸你們自己,作為田地的穀種,作為你們和你們的家屬以及幼兒的食糧。」
Wakati wa mavuno, mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu, kwa mbegu za shamba na kwa chakula cha nyumba zenu na watoto wenu.”
25 他們答說:「你救了我們的性命! 唯願我們在我主前蒙恩,我們情願給法郎為奴! 」
Wakasema, “Umeokoa maisha yetu. Na tupate kibali machoni pako. Tutakuwa watumishi wa Farao.”
26 由此若瑟為埃及的田地立了法例,至今有效:五分之一應歸法郎;只有司祭的田地例外,不歸法郎。
Hivyo Yusufu akaifanya kuwa sheria inayofanya kazi hata leo katika nchi ya Misri, kwamba moja ya tano ni ya Farao. Eneo la makuhani peke yake ndo halikufanywa kuwa la Farao.
27 以色列人住在埃及國哥笙地方,那裏置業繁殖,人數大為增加。
Hivyo Israeli akaishi katika nchi ya Misri, katika eneo la Gosheni. Watu wake wakapata umiliki pale. Walikuwa wenye kuzaa na kuongezeka sana.
28 雅各伯在埃及國又活了十七年;雅各伯的一生歲月共計一百四十七年。
Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, kwa hiyo miaka ya maisha ya Yakobo ilikuwa miaka mia moja arobaini na saba.
29 以色列自知死期已近,便叫了他兒子若瑟來,對他說:「如果我在你眼內得寵,請將你的手放在我的胯下許下,以恩情和忠實對待我,不要將我埋在埃及。
Wakati wa kufa kwake Yakobo ulipokaribia, alimwita Yusufu mwanaye na kumwambia, “Ikiwa nimepata kibali mbele zako, weka mkono wako chini ya paja langu, na unitendee kwa uaminifu na kweli. Tafadhari usinizike Misri.
30 我與我的祖先同眠了,你應將我帶出埃及,葬在他們的墓地裏。」若瑟答說:「我必照你的話去行。」
Nitakapolala na baba zangu, utanitoa Misri na kunizika katika eneo la kuzikia la baba zangu.” Yusufu akasema, “Nitafanya kama ulivyosema.”
31 雅各伯接著說:「你對我發誓。」若瑟遂對他發了誓;以色列便靠著床頭屈身下拜。
Israeli akasema, “Niapie,” na Yusufu akamwapia. Kisha Israeli akainama chini mbele ya kitanda chake.

< 創世記 47 >