< 創世記 16 >

1 亞巴郎的妻子撒辣依,沒有給他生孩子,她有個埃及婢女,名叫哈加爾。
Kisha Sarai mke wa Abram, alikuwa hajamzalia mtoto, lakini alikuwa na mtumishi wa kike, Mmisri ambaye jina lake aliitwa Hajiri.
2 撒辣依就對亞巴郎說:「請看,上主既使我不能生育,你可去親近我的婢女,或許我能由她得到孩子。」亞巴郎就聽了撒辣依的話。
Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, “Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye.” Abram akasikiliza sauti ya Sarai.
3 亞巴郎住在客納罕地十年後,亞巴郎的妻子撒辣依將自己的埃及婢女哈加爾,給了丈夫亞巴郎做妾。
Ilikuwa baada ya Abram kuishi miaka kumi katika nchi ya Kanaani ndipo Sarai, mke wa Abram, alimtoa Hajiri yule mmisri mtumishi wake kwa mume wake awe kama mke wake.
4 亞巴郎自從同哈加爾親近,哈加爾就懷了孕;她見自己懷了孕;就看不起自己的主母。
Kwa hiyo akawa na mahusiano na Hajiri, na akabeba mimba. Na alipoona kuwa amebeba mimba, akamdharau bibi yake.
5 撒辣依對亞巴郎說:「我受羞辱是你的過錯。我將我的婢女放在你懷裏,她一見自己懷了孕,便看不起我。願上主在我與你之間來判斷! 」
Kisha Sarai akamwambia Abram, “Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamuwe kati yangu na wewe.”
6 亞巴郎對撒辣依說:「你的婢女是在你手中;你看怎樣好,就怎樣待她罷! 」於是撒辣依就虐待她,她便由撒辣依面前逃跑了。
Lakini Abram akamwambia Sarai, “Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake.” Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka.
7 上主的使者在曠野的水泉旁,即在往叔爾道上的水泉旁,遇見了她,
Malaika wa Yahwe akamkuta karibu na chemichemi ya maji katika jangwa, chemichemi iliyo katika njia kuelekea Shuri.
8 對她說:「撒辣依的婢女哈加爾! 你從那裏來,要往那裏去﹖」她答說:「我由我主母撒辣依那裏逃出來的。」
Akasema, Hajiri, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi na unakwenda wapi?” Na akasema, ninamtoroka bibi yangu Sarai.”
9 上主的使者對她說:「你要回到你主母那裏,屈服在她手下。」
Malaika wa Yahwe akamwambia, “Rudi kwa bibi yako, na unyenyekee chini ya mamlaka yake.”
10 上主的使者又對她說:「我要使你的後裔繁衍,多得不可勝數。」
Kisha Malaika wa Yahwe akamwambia, “Nitazidisha uzao wako maradufu, kiasi kwamba watakuwa wengi wasioweza kuhesabika.”
11 上主的使者再對她說:「看,你已懷孕,要生個兒子;要給他起名叫依市瑪耳,因為上主俯聽了你的苦訴。
Malaika wa Yahwe pia akamwambia, “Tazama, wewe unamimba, na utazaa mtoto kiume, na utamwita jina lake Ishmaeli, kwasabab Yahwe amesikia mateso yako.
12 他將來為人,像頭野驢;他要反對眾人,眾人也要反對他;他要衝著自己的眾兄弟支搭帳幕。」
Atakuwa punda mwitu wa mtu. Atakuwa adui dhidi ya kila mtu, na kila mtu atakuwa adui yake, na ataishi kando na ndugu zake wote.”
13 哈加爾遂給那對她說話的上主起名叫「你是看顧人的天主,」因為她說:「我不是也看見了那看顧人的天主嗎﹖」
Kisha akamwita jina hili Yahwe aliye zungumza naye, “Wewe ni Mungu unionaye mimi,” kwa kuwa alisema, “je ninaendelea kweli kuona, hata baada ya kuwa ameniona?”
14 為此她給那井起名叫拉海洛依井。這井是在卡德士與貝勒得之間。
Kwa hiyo kisima kiliitwa Beerlahairori; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.
15 哈加爾給亞巴郎生了一個兒子,亞巴郎給哈加爾所生的兒子,起名叫依市瑪耳。
Hajiri akamzalia Abram mwana wa kiume, na Abram akamwita mwanawe, ambaye Hajiri amemzaa jina, Ishmaeli.
16 哈加爾給亞巴郎生依市瑪耳時,亞巴郎已八十六歲。
Abram alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hajiri alipomzaa Ishmaeli kwa Abram.

< 創世記 16 >