< 出埃及記 18 >

1 梅瑟的岳父,米德楊的司祭耶特洛,聽說天主為梅瑟和自己的百姓以色列所行的一切,聽說上主將以色列人領出了埃及,
Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wake Musa, alisikia yote Mungu aliyo fanya kwa Musa na kwa Israeli watu wake. Alisikia Yahweh ametoa Israeli kutoka Misri.
2 梅瑟的岳父耶特洛便帶回梅瑟送回去的妻子漆頗辣和
Yethro, baba mkwe wake Musa, akamchukuwa Zipora, mke wa Musa, baada ya kumpeleka nyumbani,
3 他兩個兒子:─一個名叫革爾雄,因為梅瑟說:「我在外方作了旅客;」
na wana wake wawili; jina mmoja lilikuwa Gershomu, kwa kuwa Musa alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.”
4 一個名叫厄里厄則爾,意謂:「我父親的天主是我的救援,救我脫離了法朗的刀劍。」─
Jina la mwingine lilikuwa Eliezeri, kwa kuwa Musa alisema, “Mungu wa babu yangu alikuwa msaada wangu. Aliniokoa na mkono wa Farao.”
5 梅瑟的岳父耶特洛同梅瑟的兒子和妻子來到了梅瑟那裏,來到曠野,近天主的山,梅瑟安營的地方,
Yethro, baba mkwe wake Musa, alikuja na watoto wake Musa na mke wake Musa nyikani alipo eka kambi katika mlima wa Mungu.
6 便叫人告訴梅瑟說:「看,你的岳父耶特洛來見你,你的妻子和兩個兒子也一同來了。」
Alimwambia Musa, “Mimi, baba mkwe wako Yethro, nina kuja kwako na mke wako na wanao wawili.”
7 梅瑟就出來迎接他的岳父,向他下拜,口親他,彼此問安,隨後進了營幕。
Musa alitoka kwenda kukutana na baba mkwe wake, akamwinamia, na kumbusu. Wakajuliana hali na wakaingia ndani ya hema.
8 梅瑟給他岳父講述了上主為以色列的原故,對法朗和埃及人所行的一切,以及路上遭遇的一切困難,上主怎樣整救了他們。
Musa akamwambia baba mkwe wake yale yote Yahweh aliyo ya fanya kwa Farao na Wamisri kwa ajili ya Waisraeli, magumu yote yaliyo watoke njianim na jinsi Yahweh alivyo waokoa.
9 耶特洛聽了上主賜給以色列的各種恩惠,從埃及人手中整救了他們,很是高興。
Yethro akafurahia yale mema yote Yahweh aliyo watendea Israeli, kwa hilo amewaokoa na mkono wa Wamisri.
10 耶特洛說:「上主應受讚頌,他從埃及人和法朗手中拯救了你們,由埃! 人手中救出了這百姓。
Yethro akasema, “Yahweh atukuzwe, kwa kuwa amekuokoa na mkono wa Wamisri na mkono wa Faraom na kuwatoa watu kwenye mkono wa Wamisri.
11 現今我知道「雅威」是眾神中最大的,因為他由那些傲慢對待以色列人的埃及手中,救出這百姓。」
Sasa najua Yahweh ni mkuu kuliko miungu yote, kwasababu Wamisri walipo watenda Waisraeli kwa kiburi, Mungu aliwaokoa watu wake.”
12 梅瑟的岳父耶特洛向天主獻了全燔祭和犧牲,亞郎和以色列眾長老都來到天主前,同梅瑟的岳父聚餐。耶特洛的建議
Yethro, baba mkwe wake Musa, akaleta sadaka ya kuteketeza na dhabihu kwa Mungu. Aruni na wazee wote wa Israeli wakaja kula chakula mbele za Yahweh na baba mkwe wake Musa.
13 次日,梅瑟坐著審判百姓的案件,百姓從早晨到晚上站在梅瑟前。
Siku iliyofuata Musa aliketi kuwa hukumu watu. Watu walisimama kumzunguka Musa kwanzia asubui hadi jioni.
14 梅瑟的岳父看見他對百姓所行的種種,就說:「你對百姓所作的是什麼事﹖為什麼你獨自一人管理,叫眾百姓從早晨到晚上站在你前﹖」
Baba mkwe wake Musa alipo ona yale yote aliyo yafanya kwa watu, alisema, “Ni nini unachofanya na watu? Kwanini unaketi peke yako na watu wote wamesimama kukuzunguka asubui hadi jioni?”
15 梅瑟回答他岳父說:「因為百姓到我跟前詢問天主。
Musa akamwambia baba mkwe wake, “Watu wanakuja kuniuliza muongozo wa Mungu.
16 他們有訴訟的事,就來到我跟前,我便在兩造之間施行審判,講明天主的典章和法律。」
Wanapo kuwa na malumbano, wanakuja kwangu. Ninaamua kati ya mtu mmoja na mwingine, na nina wafundisha maagizo na sheria.”
17 梅瑟的岳父對他說:「你這樣作不對。
Baba mkwe wake Musa alimwambia, “Unachofanya sicho kizuri sana.
18 不但使你自己疲乏,而且也使你同你一起的百姓疲勞不堪,因為這事超過你的力量,你獨自一人是不能勝任的。
Hakika utajichosha, wewe na watu waliyopo na wewe. Huu mzigo ni mzito sana kwako. Hauwezi kufanya peke yako.
19 現在你聽我的話,我給你出一個主意。願天主與你同在! 你在天主前代表這個百姓,將他們的案件呈到天主前;
Nisikilize. Nitakupa ushauri, na Mungu ata kuwa na wewe, kwasababu wewe nimwakilishi wa watu kwa Mungu, na una leta malumbano yao kwake.
20 也將典章和法律教訓他們,告訴他們應走的正路,應行的事項。
Lazima uwafundishe maagizo yake na sheria. Lazima uwafundishe njia yakutembea na kazi ya kufanya.
21 你要從百姓中挑選有才能,敬畏天主,忠實可靠,捨己無私的人,派他們作千夫長、百夫長,五十夫長、十夫長,
Mbali zaidi, lazima uchague wanaume wenye uwezo kutoka watu wote, wanaume wanao muheshimu Mungu, wanaume wa kweli wanao chukuia mapato ya ufisadi. Lazima uwaeke juu ya watu, kuwa viongozi wa maelfu, mamia, hamsini, na makumi.
22 叫他們隨時審斷百姓的案件。若有任何重大案件,呈交你處理;其餘一切小案件,可由他們自己處理;叫他們與你分擔,你就輕鬆多了。
Watawa hukumu watu na kesi za kawaida, lakini kesi ngumu wataleta kwako. Kwa kesi ndogo, wanaweza kuhukumu wenyewe. Kwa hivyo itakuwa rahisi kwako, na watabeba mzigo na wewe.
23 你若這樣作,─天主也這樣命你─你就抵受得住,眾百姓也能平安,各歸其所。」
Ukifanya hivi, na kama Mungu akikuamuru kufanya al kadhalika, basi utaweza kuvumilia, na watu wote watarudi nyumbani wameridhika.”
24 梅瑟聽從了他岳父的話,也都照他說的行了。
Hivyo Musa akasikiliza maneno ya baba mkwe wake na akafanya yale yote aliyo yasema.
25 梅瑟從全以色列人選拔了有才能的人,立他們作百姓的頭目,作千夫長、百夫長、五十夫長和十夫長,
Musa alichagua wanaume wenye uwezo kutoka Israeli na kuwa fanya vichwa juu ya watu, viongozi wahusika wa maelfu, mamia, hamsini, na makumi.
26 叫它們隨時審斷百姓的案件;重大的案件,呈交梅瑟處理;一切小案件,由他們自己處理。
Waliwa hukumu watu katika hali za kawaida. Kesi ngumu walimletea Musa, lakini wao wenyewe wali hukumu kesi ndogo.
27 以後梅瑟送他岳父回了本地。
Kisha Musa akamwacha baba mkwe wake kuondoka, na Yethro akarudi kwenye nchi yake.

< 出埃及記 18 >