< 以弗所書 1 >

1 因天主的旨意,做耶穌基督宗徒的保祿,致書給那些在 [厄弗所的 ] 聖徒和信仰基督耶穌的人。
Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kwa waliotengwa kwa ajili ya Mungu walioko Efeso na ambao ni waaminifu katika Kristo Yesu.
2 願恩寵與平安,由我們的天主和主耶穌基督,賜與你們!
Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
3 願我們的主耶穌基督的天主和父受讚美!祂在天上,在基督內,以各種屬神的祝福,祝福了我們,
Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa. Ni yeye aliyetubariki kwa kila baraka za kiroho, katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo.
4 因為祂於創世以前,在基督內己揀選了我們,為使我們在祂面前,成為聖潔無瑕疵的;
Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituchagua sisi ambao tunaamini katika Kristo. Alituchagua sisi ili tuweze kuwa watakatifu na tusiolaumika mbele yake.
5 又由於愛,按照自己旨的決定,預定了我們藉著耶穌基督獲得義子的名分,而歸於祂,
Katika pendo Mungu alituchagua mwanzo kwa kututwaa kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Alifanya hivi kwa sababu alipendezwa kufanya kile alichotamani.
6 為頌揚祂恩寵的光榮,這恩寵是祂在自己的愛子內賜與我們的;
Matokeo yake ni kwamba Mungu anatukuzwa kwa neema ya utukufu wake. Hiki ndicho alichotupatia bure kwa njia ya mpendwa wake.
7 我們就是全憑天主豐厚的恩寵,在祂的愛子內,藉祂愛子的血,獲得了救贖,罪過的赦免。
Kwa kuwa katika mpendwa wake, tunaukombozi kupitia damu yake, msamaha wa dhambi. Tunalo hili kwa sababu ya utajiri wa neema yake.
8 的確,天主豐厚地把這恩寵傾注在我們身上,賜與我們各種智慧和明達,
Alifanya neema hii kuwa nyingi kwa ajili yetu katika hekima na ufahamu.
9 為使我們知道,祂旨意的奧祕,是全照祂在愛子內所定的計畫;
Mungu alifanya ijulikane kwetu ile kweli iliyofichika ya mpango, kutokana na hamu iliyodhihirishwa ndani ya Kristo.
10 就是依照祂的措施,當時期一滿,就使天上和地上的萬有,總歸於基督元苜。
Wakati nyakati zimetimia kwa utimilifu wa mpango wake, Mungu ataviweka pamoja kila kitu cha mbinguni na cha juu ya nchi ndani ya Kristo.
11 我們也是在基督內得作天主的產業,因為我們是由那位按照自己旨意的計畫施行萬事者,早預定了的,
Katika Kristo tulikuwa tumechaguliwa na kukusudiwa kabla ya wakati. Hii ilikuwa ni kutokana na mpango wa anayefanya vitu vyote kwa kusudi la mapenzi yake.
12 為使我們這些首先在默西亞內懷著希望的人,頌揚祂的光榮;
Mungu alifanya hivyo ili kwamba tuweze kuwapo kwa sifa ya utukufu wake. Tulikuwa wa kwanza kuwa na ujasiri ndani ya Kristo.
13 在基督內,你們一聽到了真理的話,即你們得救的福音,便信從了,且在祂內受了恩許聖神的印證;
Ilikuwa kwa njia ya Kristo kwamba mlisikia neno la kweli, injili ya wokovu wenu kwa njia ya Kristo. Ilikuwa katika yeye pia kwamba mmeamini na kutiwa mhuri na Roho Mtakatifu aliye ahidiwa.
14 這聖神就是我們得嗣業的保證,為使天主所置為嗣業的子民,蒙受完全的救贖,為頌揚祂的光榮。
Roho ndiyo dhamana ya urithi wetu mpaka umiliki utakapopatikana. Hii ilikuwa ni kwa sifa ya utukufu wake.
15 因此,我一聽見你們對主耶穌的信德和對眾聖徒的愛德,
Kwa sababu hii, tangu wakati niliposikia kuhusu imani yenu ndani ya Bwana Yesu na kuhusu pendo lenu kwa wale wote ambao wametengwa kwa ajili yake.
16 便不斷為你們感謝天主,在我的祈禱中紀念你們,
Sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu na kuwataja katika maombi yangu.
17 為使我們的主耶穌基督的天主,即那光榮的父,把智慧和啟示的神恩,賜與你們,好使你們認識祂;
Ninaomba kwamba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, baba wa utukufu, atawapeni roho ya hekima, mafunuo ya ufahamu wake.
18 並光照你們心靈的眼目,為叫你們認清祂的寵召什麼希望,在聖徒中祂嗣業的光榮,是怎樣豐厚;
Ninaomba kwamba macho yenu ya moyoni yatiwe nuru kwa ninyi kujua ni upi ujasiri wa kuitwa kwenu. Naomba kwamba mjue utajiri wa utukufu wa urithi wake miongoni mwa wale waliotengwa kwa ajili yake.
19 祂對我們虔信的人,所施展的強有力而見效的德能是怎樣的偉大。
Naomba kwamba ujue ukuu uzidio wa nguvu yake ndani yetu ambao tunaamini. Huu ukuu ni kutokana na kufanya kazi katika nguvu zake.
20 正如祂已將這德能施展在基督身上,使祂從死者中復活,叫祂在天上坐在自己右邊,
Hii ni nguvu iliyofanya kazi ndani ya Kristo wakati Mungu alipomfufua kutoka kwa wafu na kumketisha katika mkono wake wa kuume katika mahali pa mbingu.
21 超乎一切率領者、掌權者、異能者、宰制者,以及一切現世及來世的可稱呼的名號以上; (aiōn g165)
Alimketisha Kristo juu mbali na utawala, mamlaka, nguvu, enzi, na kila jina litajwalo. Alimketisha Yesu si tu kwa wakati huu lakini kwa wakati ujao pia. (aiōn g165)
22 又將萬有置於祂的腳下,使祂教會內作至上的元首,
Mungu amevitiisha vitu vyote chini ya miguu ya Kristo. Amemfanya yeye kichwa juu ya vitu vyote katika kanisa.
23 這教會就是基督的身體,就是在一切內充滿一切者的圓滿。
Ni kanisa kwamba ndilo mwili wake, ukamilifu wake ambaye hujaza vitu vyote katika njia zote.

< 以弗所書 1 >