< 以弗所書 6 >

1 你們作子女的,要在主內聽從你們的父母,因為這是理所當然的。『
Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.
2 孝敬你的父親和母親──這是附有恩許的第一條誡命──
“Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),
3 為使你得到幸福,並在地上延年益壽。』
“ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu juu ya nchi.”
4 你們作父母的,不要惹你們的子女發怒;但要用主的規範和訓誡,教養他們。
Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika maonyo na maagizo ya Bwana.
5 你們作奴僕的,要戰戰兢兢,以誠實的心,隨從你們肉身的主人,如同隨同基督一樣。
Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo.
6 不要只在人眼前服事,好像單討人的喜歡,而要像基督的僕人,從心裏遵行天主的旨意;
Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu,
7 甘心服事,好像服事主,而非服事人,
watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu,
8 因為你們知道:每一個人,或為奴的,或自主的,不論行了什麼善事,都要按他所行的領取主的賞報。
mnapaswa kujua kwamba katika kila tendo jema mtu analofanya, atapokea zawadi kutoka kwa Bwana, ikiwa ni mtumwa au mtu huru.
9 至於你們作主人的,要同樣對待奴僕,戒用恐嚇,因為你們知道,他們和你們在天上有同一個主,而且祂是不看情面的。
Na ninyi mabwana fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu. Msiwatishe mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni. Mkijua kuwa hakuna upendeleo ndani yake.
10 此外,你們務要在主內,藉祂的能力作堅強的人。
Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.
11 要穿上天主的全副武裝,為能抵抗魔鬼的陰謀,
Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani.
12 因為我們戰鬥不是對抗血和肉,而是對抗率領者,對抗掌權者,對抗這黑暗世界的霸主,對抗天界裏邪惡的鬼神。 (aiōn g165)
kwa kuwa vita yetu si ya damu na nyama, bali ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala wa ulimwengu wa uovu na giza, dhidi ya pepo katika sehemu za mbingu. (aiōn g165)
13 為此,你們應拿起天主的全副武裝,為使你們在邪惡的日子能夠抵得住,並在獲得全勝之後,仍屹立不動。
Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kusimama imara dhidi ya uovu katika kipindi hiki kiovu. Baada ya kumaliza kila kitu, mtasimama imara.
14 所以要站穩! 用真理作帶,束起你們的腰,穿上正義作甲,
Hatimaye simameni imara. Fanyeni hivi baada ya kuwa mmefunga mkanda katika kweli na haki kifuani.
15 以和平的福音作準備走路的鞋,穿在腳上;
Fanyini hivi mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu wa kutangaza injili ya amani.
16 上此外,還要拿起信德作盾牌,使你們能以此撲滅惡者的一切火箭;
Katika kila hali mkichukua ngao ya imani, ambayo itakuwezesha kuizima mishale ya yule mwovu.
17 並戴上救恩當盔,拿著聖神作利劍,即天主的話,
Vaeni kofia ya wokovu na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu.
18 時時靠著聖神,以各種祈求和哀禱祈禱;且要醒寤不倦,為眾聖徒祈求,
pamoja na maombi na dua. Ombeni kwa Roho kila wakati. Kwa mtazamo huu iweni waangalifu kila wakati kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waamini wote.
19 也為我祈求,使我在開口的時候,賜我能說相稱的話,能放心大膽地傳揚福音的奧祕──
Ombeni kwa ajili yangu, ili nipewe ujumbe ninapofungua mdomo wangu. Ombeni kwamba nieleweshe kwa ujasiri kweli iliyofichika ihusuyo injili.
20 為這福音我竟作了帶鎖鍊的使者──使我能放心大膽,我應該宣講的去宣講。
Ni kwa ajili ya injili mimi ni balozi niliyefungwa minyororo, ili kwamba ndani mwao niseme kwa ujasiri kama ninavyowiwa kusema.
21 今我有可愛的弟兄,且忠於主的服務者提希苛給你們報告一切,好使你們知道我的事和我現在做什麼。
Lakini ninyi pia mjue mambo yangu na jinsi ninavyoendelea, Tikiko ndugu yangu kipenzi na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawajulisha kila kitu.
22 我特意打發他到你們那裏去,為叫你們知道我們的情形,並叫他安慰你們的心。
Nimemtuma kwenu kwa kusudi hili maalumu, ili kwamba mjue mambo kuhusu sisi, aweze kuwafariji mioyo yenu.
23 願平安、愛德和信德由天主父和主耶穌基督賜與眾弟兄!
Amani na iwe kwa ndugu, na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu baba na Bwana Yesu Kristo.
24 恩寵與那些以永恆不變的愛愛我們的主耶穌基督的人同在!
Neema na iwe pamoja na wote wanampenda Bwana Yesu Kristo kwa pendo lile lisilo kufa.

< 以弗所書 6 >