< 申命記 33 >
1 這是天主的人,梅瑟死前賜予以四色列子民的祝福。
Hii ni baraka ambayo Musa mtu wa Mungu aliwabariki watu wa Israeli kabla ya kifo chake.
2 他說:「上主由西乃而來,從色依爾光照他的百姓,由帕蘭山射出光輝,從卡德士的默黎巴前進,由他的右邊有烈火發出。
Alisema: Yahwe alikuja kutoka Sinai na akainuka kutoka Seiri juu yao. Aling'ara kutoka mlima wa Paramu, na akaja na elfu kumi ya watakatifu. Katika mkono wake wa kuume radi zilimulika.
3 你實在愛你的人民,眾聖者都在你手中;他們俯伏在你腳前,領受你的教導。
Kweli, anawapenda watu; watakatifu wake wote wapo mikononi mwako, na walimsujudu mguuni mwake; walipokea maneno yako.
Musa alituamuru sheria, urithi kwa kusanyiko la Yakobo.
5 人民的首領與以色列支派會合時,上主在耶叔戎中作了王。
Kisha pakawa na mfalme Yeshurumu, pale ambapo wakuu wa watu walipokusanyika, makabila yote ya Israeli pamoja.
6 願勒烏本生存,不至滅亡! 願他的人數不再減少! 」
Acha Rubeni aishi na asife, lakini wanaume wake wawe wachache.
7 他論及猶大這樣說:「上主! 願你俯聽猶大的聲音,領他重歸自己的民族;以你的手為他交戰,協助他抵抗他的仇敵! 」
Hii ni baraka ya Yuda. Musa akasema: Sikiliza sauti ya Yuda, Yahwe, na umlete kwa watu wake tena. Mpiganie; kuwa msaada dhidi ya maadui wake.
8 論及肋未說:「願你將你的「突明」賜給肋未,將你的「烏陵」,賜給對你虔誠的人,就是你在瑪撒曾試探過,在默黎巴水旁曾考驗過的人,
Kuhusu Lawi, Musa akasema: Thumimu yako na Urimu yako ni ya mtakatifu wako, yule uliyemjaribu kule Masa, ambaye ulishindana naye katika maji ya Meriba.
9 也就是那些論及自己的父母說:我沒有顧及他們,對自己的兄弟不加重視,對自己的子女也漠不關心的人! 他們只遵守你的話,持守你的盟約。
Mtu aliyesema juu ya baba na mama yake, “Sijawaona.” Wala hakuwatambua kaka zake, wala hakuzingatia juu ya watoto wake wenyewe. Kwa maana alilinda neno lako na kushika agano lako.
10 他們要將你的誡命教給雅各伯,將你的法律授給以色列;在你面前獻上馨香,在祭壇上獻上全燔祭。
Anafundisha Yakobo maagizo yako na Israeli sheria yako. Ataweka ubani mbele yako na sadaka kamili ya kuteketezwa juu ya dhabahu lako.
11 上主! 願你祝福他的勇力,悅納他手中的作為;對反抗他的人,願你打斷他們的腰,使惱恨他的人,再也不得起立! 」
Bariki mali zake, Yahwe, na kubali kazi ya mikono yake. Vunja viuno vya wale wanaoinuka dhidi yake, na wale watu wanaomchukia, ili wasiinuke tena.
12 論及本雅明說:「上主所鍾愛的,他必安居樂業;至高者日日庇護他,住在他兩肩之間。」
Kuhusu Benyamini, Musa akasema: Yule anayependwa na Yahwe anaishi kwa usalama kando yake; Yahwe anamkinga siku nzima, naye huishi katikati ya mikono ya Yahwe.
13 論及若瑟說:「願他的地蒙受上主的祝福! 願天上甘露,地下深藏的淵泉,
Kuhusu Yusufu, Musa akasema: Nchi yake na ibarikiwe na Yahwe na vitu vya thamani vya mbinguni, na umande, na kina kilalacho chini.
Nchi yake na ibarikiwe na vitu vya thamani mavuno ya jua, na vitu vya thamani mazao ya miezi,
kwa vitu vizuri vya milima ya zamani, na kwa vitu vya thamani vya milima ya milele.
16 地上的寶物及其富藏,以及住在荊棘叢中者的恩惠,都臨到若瑟頭上,降在兄弟中為首者的頭頂上!
Nchi yake ibarikiwe na vitu vya thamani vya ardhi na wingi wake, na kwa mapenzi mema ya yule aliyekuwa kichakani. Baraka na ifike juu ya kichwa cha Yusufu, na juu ya kichwa cha yule aliyekuwa mwana wa mfalme kwa kaka zake.
17 他的健壯有如頭胎的公牛,他的雙角像是野牛的雙角,用以抵觸萬民,直到地極。這是厄弗辣因的萬軍,即是默納協的勁旅。」
Mzawa wa kwanza wa ng’ombe, katika utukufu wake, na pembe zake ni pembe za ng’ombe mwitu. Kwa hawa atawasukuma watu, wote, hadi mwisho wa ulimwengu. Hawa ni maelfu makumi ya Efraimu; hawa ni maelfu wa Manase.
18 論及則步隆說:「則步隆! 你要在旅途中喜樂;至於你、依撒加爾! 你要在帳幕內歡樂。
Kuhusu Zabuloni, Musa alisema: Furahi, Zabuloni, katika kutoka kwako, na wewe, Isakari, katika mahema yako.
19 他們要邀請人民上山,在那裏奉獻應獻的祭祀,因為他們要吸收海洋的富饒,沙中潛藏的珠寶。」
Watawaita watu hadi milimani. Huko watatoa sadaka za utakatifu. Maana watanyonya wingi wa bahari, na mchanga wa ufukweni.
20 論及加得說:「那使加得擴張的,應受讚美! 他臥下彷彿一隻母獅,撕裂了人的手臂和頭顱。
Kuhusu Gadi, Musa alisema: Abarikiwe yule amkuzaye Gadi. Ataishi pale kama simba jike, naye atanyakua mkono au kichwa.
21 他為自己選取了為首的一分,因為那原是為首領保留的一分。他走在人民之前,執行了上主的法令,和他對以色列的旨意。」
Alitoa sehemu nzuri kwake mwenyewe, maana kulikuwa na fungu la ardhi la kiongozi lililohifadhiwa. Alikuja na vichwa vya watu. Alitekeleza haki ya Yahwe na maagizo yake pamoja na Israeli.
Kuhusu Dani, Musa alisema: Dani ni mwana wa simba arukaye kutoka Bashani.
23 論及納斐塔里說:「納斐塔里,飽受恩愛,充滿上主的祝福,海和南部將是他的產業。」
Kuhusu Naftali, Musa alisema: Naftali, aliyeridhika na fadhila, na kujaa kwa baraka za Yahwe, miliki nchi iliyopo magharibi na kusini.
24 論及阿協爾說:「眾子中最受祝福的是阿協爾;願他獲得兄弟的恩待,在油中洗腳!
Kuhusu Asheri, Musa alisema: Abarakiwe Asheri Zaidi ya watoto wengine wa kiume; naye akubalike kwa kaka zake, na achovye mguu wake ndani ya mafuta ya zeituni.
Vyuma vya mji wako na viwe chuma na shaba; kama vile siku zako zitakavyokuwa, ndivyo usalama wako utakavyokuwa.
26 沒有一個像耶叔戎的天主,他騰空駕雲,在威嚴中來援助你。
Hakuna aliye kama Mungu, Yeshurumu – aliyekamili, anayeendesha katika mbingu kukusaidia, na katika utukufu wake juu ya mawingu.
27 亙古的天主是你的避難所,他永遠的手臂是你的支柱;他由你面前驅走了敵人,是他向你下命說:毀滅罷!
Mungu wa milele ni kimbilio, na chini yake kuna mikono ya milele. Husukuma adui mbele yako, naye alisema, “Angamiza!”
28 因此,以色列能以安居樂業,雅各伯的後裔定居在產糧出酒之地,天也從上降下甘露。
Israeli waliishi katika usalama. Wana wa Yakobo walikuwa salama katika nchi ya nafaka na divai mpya; hakika, mbingu na idondoshe umande juu yake.
29 以色列,你真是有福的;為上主所拯救的人民,有誰相似你﹖他是你護身的盾牌,是使你勝利的刀劍。你的仇敵必將奉承你,而你卻要踐踏他們的背脊。
Baraka zako ni nyingi, Israeli! Nani kama wewe, watu waliokombolewa na Yahwe, ngao ya msaada wako, na upanga wa utukufu wako? Maadui zako watakuja kwako kwa kutetemeka; utakanyanga sehemu zao zilizoinuka.