< 使徒行傳 5 >

1 有一個人,名叫阿納尼雅,同他的妻子撒斐辣賣了一塊田地。
Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja.
2 他扣留了一部分價錢,妻子也表同意,就帶了一部份去放在宗徒腳前。
Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume.
3 伯多祿說道:「阿納尼雅!為什麼撒殫充滿了你的心,使你欺騙聖神,扣留了田地的價錢呢﹖
Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja?
4 田地留下不賣,不是還是你的嗎﹖既賣了,價錢不是還屬於你權下嗎﹖為什麼你心中打算了這事﹖你不是欺騙人,而是欺騙天主!」
Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.”
5 阿納尼雅一聽這話,就跌倒斷了氣。凡聽見的人,都十分害怕。
Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia.
6 年輕人就起來,把他裹起,抬去埋葬了。
Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakamchukua nje kumzika.
7 大約隔了三個時辰,他的妻子進來了,還不知所發生的事。
Saa tatu baadaye mkewe Anania akaingia, naye hana habari ya mambo yaliyotukia.
8 伯多祿問她說:「你告訴我:你們賣田地的價錢就是這麼多嗎﹖」她說:「是,就是這麼多。」
Petro akamuuliza, “Niambie, je, mliuza kiwanja kwa thamani hii?” Akajibu, “Ndiyo, tuliuza kwa thamani hiyo.”
9 伯多祿便說:「你們為什麼共謀試探主的神呢﹖看,埋葬你丈夫者的腳已到門口,他們也要把你抬去。」
Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje mkakubaliana kumjaribu Roho wa Bwana? Tazama! Nyayo za vijana waliomzika mumeo ziko mlangoni, wewe nawe watakuchukua nje.”
10 她立刻跌倒在他腳前,也斷了氣。年輕人進來,見她死了,就抬去埋葬在她丈夫旁邊。
Saa ile ile akaanguka chini miguuni mwake na kufa. Nao wale vijana wakaingia, wakamkuta amekufa, wakamchukua wakamzika kando ya mumewe.
11 全教會和一切聽見這些事的人,都十分害怕。
Hofu kuu ikalipata kanisa lote pamoja na watu wote waliosikia juu ya matukio haya.
12 宗徒們在百姓中行了許多徵兆,顯了許多奇蹟。眾信徒都同心合意地聚在撒羅滿廊下,
Mitume wakafanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Walioamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Solomoni.
13 其他的人沒有一個敢與他們接近的;但是百姓都誇讚他們。
Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kuambatana nao ijapokuwa waliheshimiwa sana na watu.
14 信主的人越來越增加,男女的人數極其眾多。
Hata hivyo, waliomwamini Bwana wakazidi kuongezeka, wanaume na wanawake.
15 宗徒們行了這樣多的奇蹟,以致有人把病人抬到街上,放在床上或褥子上,好叫伯多祿走過的時候,至少他的影子能遮在一些人身上。
Hata wakawa wanawaleta wagonjwa na kuwalaza kwenye magodoro na kwenye vitanda barabarani ili yamkini Petro akipita kivuli chake kiwaguse baadhi yao.
16 還有許多耶路撒冷四周城市的人,抬著病人和被邪魔所纏擾的人,齊集而來,他們都得了痊癒。
Pia watu wakakusanyika kutoka miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu. Hao wote wakaponywa.
17 大司祭和他的一切同人,即撒杜塞黨人,都起來,嫉恨填胸,
Kisha kuhani mkuu na wenzake wote waliokuwa pamoja naye, waliokuwa wa kundi la Masadukayo, wakajawa na wivu.
18 下手拿住宗徒,把他們押在公共拘留所內。
Wakawakamata mitume na kuwatia gerezani.
19 夜間,有上主的天使打開了監獄的門,領他們出來說:「
Lakini wakati wa usiku, malaika wa Bwana akaja, akafungua milango ya gereza na akawatoa nje. Akawaambia,
20 你們去,站在聖殿裏,把一切有關生命的話,講給百姓聽。」
“Nendeni, mkasimame Hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu mpya.”
21 他們領了命,天一亮就進入聖殿施教。大司祭和他的同人來召開公議會,即以色列子民全長老議會,差人去監裏把宗徒們提出來。
Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani.
22 差役來到,在監獄中沒有找到他們,便回去報告,
Lakini wale walinzi wa Hekalu walipokwenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari.
23 說:「我們確實看見監獄關鎖的非常牢固,衛兵也站在門前,但一打開,裏面沒有找到一個人。」
Wakasema, “Tumekuta milango ya gereza imefungwa sawasawa na askari wa gereza wamesimama nje ya mlango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu yeyote ndani.”
24 聖殿警官和司祭長一聽這些話,十分納悶,不知發生了什麼事。
Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje.
25 忽有一個人來向他們報告說:「看,你們押在監獄裏的人,站在聖殿裏,教訓百姓。」
Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Tazameni watu mliowatia gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.”
26 聖殿警官就同差役去把他們領來,但未用武力,因為怕百姓用石頭砸他們。
Ndipo yule mkuu wa walinzi wa Hekalu wakaenda pamoja na askari wakawaleta wale mitume, lakini bila ghasia kwa sababu waliogopa kupigwa mawe na watu.
27 他們把宗徒領來之後,叫他們站在公議會中,大司祭便審問他們,
Wakiisha kuwaleta mitume wakawaamuru kusimama mbele ya baraza ili kuhani mkuu awahoji.
28 說:「我們曾嚴厲命令你們,不可用這名字施教。你們看,你們卻把你們的道理傳遍了耶路撒冷,你們是有意把這人的血,引到我們身上來啊!」
“Tuliwaonya kwa nguvu msifundishe kwa jina hili, lakini ninyi mmeijaza Yerusalemu yote mafundisho yenu na tena mmekusudia kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.”
29 伯多祿和宗徒們回答說:「聽天主的命應勝過聽人的命。
Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
30 我們祖先的天主復活了你們下毒手懸在木架上的耶穌。
Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu, ambaye ninyi mlimuua kwa kumtundika kwenye msalaba.
31 天主以右手舉揚了他,叫他做首領和救主,為賜給以色列人悔改和罪赦。
Mungu alimtukuza, akamweka mkono wake wa kuume kuwa Kiongozi na Mwokozi ili awape Israeli toba na msamaha wa dhambi.
32 我們就是這些事的證人,並且天主給那些服從他的人所賞的聖神,也為此事作證。」
Nasi tu mashahidi wa mambo haya, vivyo hivyo na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii.”
33 他們一聽這話,大發雷霆,想要殺害他們。
Wale wajumbe wa baraza la wazee waliposikia haya, walijawa na ghadhabu, wakataka kuwaua mitume.
34 有一個法利塞人,名叫加瑪里耳,是眾百姓敬重的法學士,他在公議會中站起來,命這些人暫時出去。
Lakini Farisayo mmoja, jina lake Gamalieli, aliyekuwa mwalimu wa sheria, aliyeheshimiwa na watu wote, akasimama mbele ya baraza akaamuru mitume watolewe nje kwa muda.
35 他便向議員們說:「諸位以色列人!你們對這些人,應小心處理!
Ndipo alipowaambia wajumbe wa baraza, “Enyi watu wa Israeli, fikirini kwa uangalifu mnayotaka kuwatendea watu hawa.
36 因為在不久以前,特烏達起來,說自己是個大人物,附和他的人數約有四百;他被殺了,跟從他的人也都散了,歸於烏有。
Kwa maana wakati uliopita, aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda, alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao 400 walioambatana naye. Lakini aliuawa, na wafuasi wake wote wakatawanyika, wakawa si kitu.
37 此後,加里肋亞人猶達,當戶口登記的日子,起來引誘百姓隨從他;他喪亡了,跟從他的人也都四散了。
Baada yake, alitokea Yuda Mgalilaya wakati wa kuorodhesha watu, naye akaongoza kundi la watu kuasi. Yeye pia aliuawa, nao wafuasi wake wakatawanyika.
38 對現今的事,我奉勸你們:不要管這些人,由他們去罷!因為,若是這計劃或工作是由人來的,必要消散;
Kwa hiyo, kwa habari ya jambo hili nawashauri, jiepusheni na watu hawa. Waacheni waende zao! Kwa maana kama kusudi lao na shughuli yao imetokana na mwanadamu, haitafanikiwa.
39 但若是從天主來的,你們不但不能消滅他們,恐怕你們反而成了與天主作對的人。」他們都贊成他的意見。
Lakini ikiwa imetoka kwa Mungu, hamtaweza kuwazuia watu hawa. Badala yake mtajikuta mnapigana na Mungu.”
40 他們遂把宗徒們叫來,鞭打了以後,命他們不可再因耶穌的名字講道,遂釋放了他們。
Wakapokea ushauri wa Gamalieli. Wakawaita mitume ndani, wakaamuru wachapwe mijeledi, kisha wakawaagiza wasinene tena kwa jina la Yesu, wakawaachia waende zao.
41 他們喜喜歡歡地由公議會前出來,因為他們配為這名字受侮辱。
Nao mitume wakatoka nje ya baraza, wakiwa wamejaa furaha kwa sababu wamehesabiwa kustahili kupata aibu kwa ajili ya jina la Yesu.
42 他們每天不斷在聖殿內,或挨戶施教,宣講基督耶穌的福音。
Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema kwamba Yesu ndiye Kristo.

< 使徒行傳 5 >