< 撒母耳記下 3 >
1 撒烏耳家與達味家間的戰爭相持很久;但達味家逐漸強盛,撒烏耳家卻日趨衰弱。
Kulikuwa na vita ya mda mrefu kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi. Daudi akaendelea kupata nguvu zaidi, lakini nyumba ya Sauli iliendelea kudhoofika na kuthoofika.
2 達味在赫貝龍生的兒子:長子阿默農,是依次勒耳人阿希諾罕所生;
Wana wakazaliwa kwa Daudi huko Hebron. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu wa Yezreeli.
3 次子基肋阿布,是曾作加爾默耳人納巴耳妻子的阿彼蓋耳所生;
Mwanawe wa pili, Kileabu, alizaliwa kwa Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. Wa tatu, Absalomu, alikuwa mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri.
4 四子阿多尼雅,是哈基特所生;五子舍法提雅,是阿彼塔耳所生;
Mwana wa nne wa Daudi, Adoniya, alikuwa mwana wa Hagithi. Mwanawe wa tano alikuwa Shefatia mwana wa Abitali,
5 六子依特蘭,是達味妻子厄革拉所生:以上是達味在赫貝龍所生的兒子。
na wa sita, Ithreamu, alikuwa mwana wa Egla mkewe Daudi. Hawa wote walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni.
6 撒烏耳家同達味家戰爭期間,阿貝乃爾獲得操縱撒烏耳家的權柄。
Ikawa wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi Abneri akajifanya mwenye nguvu katika nyumba ya Sauli.
7 撒烏耳有一妾名叫黎茲帕,是阿雅的女兒,阿貝乃爾娶了她;依市巴耳對阿貝乃爾說:「你為什麼親近我父親的妾﹖」
Sauli alikuwa na suria jina lake Rispa, binti Aiya. Ishboshethi akamuuliza Abneri, “Kwa nini umelala na suria wa baba yangu?”
8 為了依市巴耳這句話,阿貝乃爾勃然大怒說:「莫非我是猶大的狗頭﹖直到今天我憐恤你父親撒烏耳,和他的兄弟以及他的朋友,沒有使你落在達味手裏;你今天竟為了一個女人挑我的錯!
Hata ikawa Abneri akakasirika sana kutokana na maneno ya Ishboshethi naye akasema, “Je mimi ni kichwa cha mbwa wa Yuda? Ninaonesha uaminifu kwa nyumba ya Sauli, baba yako, kwa jamaa yake, na rafiki zake, kwa kutokukuweka katika mkono wa Daudi. Na bado leo unanishutumu kuhusu mwanamke.
Mungu na anifanyie hivyo, Abneri, na kuzidi, ikiwa sitafanya kwa Daudi kama Yahwe alivyomwapia,
10 廢除撒烏耳家的王位,建立達味的寶座,使他由丹直到貝爾舍巴,統治全以色列和猶大,願天主如此,並加倍地懲罰我! 」
kuuhamisha ufalme kutoka nyumba ya Sauli na kukisimika kiti cha enzi cha Daudi juu ya Israeli na juu ya Yuda, kutoka Dani hadi Beersheba.”
11 依市巴耳因為怕阿貝乃爾,連一句話也不敢回答。
Ishboshethi hakuweza kumjibu Abneri neno tena, kwani alimuogopa.
12 阿貝乃爾立即派使者到赫貝龍見達味說:「這地是誰的﹖」是說:「只要你與我訂立盟約,我必伸手援助你,使全以色列都歸順你。」
Kisha Abneri akatuma wajumbe kwa Daudi kusema, “Nchi hii ni ya nani? Fanya agano nami, nawe utaona kwamba mkono wangu uko nawe, kuiIeta Israeli yote kwako.”
13 達味答說:「好! 我願與你訂立盟約,但是,我要求你一個條件:就是你來見我時,若不把撒烏耳的女兒米加耳帶來,你休想見我。」
Daudi akajibu, “Vema, nitafanya agano nawe. Lakini neno moja ninalolitaka kutoka kwako ni kwamba hautauona uso wangu usipomuleta kwanza Mikali, binti Sauli, unapokuja kuonana nami.”
14 隨後,達味就派使者到撒烏耳的兒子依市巴耳那裏說:「請把我的妻米加耳歸還給我,她是我以一百培肋特舍人的包皮聘定的。」
Kisha Daudi akatuma wajumbe kwa Ishboshethi, mwana wa Sauli, kusema, “Nipe Mikali, mke wangu niliyetoa kwa ajili yake govi mia moja za Wafilisti.”
15 依市巴耳就派人,從拉依士的兒子帕耳提耳,她丈夫那裏把她帶來。
Hivyo Ishboshethi akatuma kwa Mikali na kumchukua kutoka kwa mme wake, Paltieli mwana wa Laishi.
16 她的丈夫與她同行,一邊走一邊哭,送她到了巴胡凌。阿貝乃爾向他說:「你回去罷! 」他就回去了。
Mme wake akafuatana naye, huku akilia, akaendelea hadi Bahurimu. Kisha Abneri akamwambia, “basi sasa rudi nyumbani.” Hivyo akarudi.
17 阿貝乃爾同以色列的長老商議說:「你們早已渴望達味作你們的君王。
Abneri akaongea na wazee wa Israeli kusema, “Zamani mlitaka Daudi awe mfalme wenu.
18 現在你們就進行罷! 因為上主曾論及達味說:我要藉我的僕人達味,從培肋舍特人及一切仇敵手中,拯救我的百姓以色列。」
Basi sasa fanyeni hivyo. Kwa maana Yahwe alisema kuhusu Daudi kusema, “Kwa mkono wa Daudi mtumishi wangu nitawaokoa watu wangu Israeli kutoka katika mkono wa Wafilisti na kutoka katika mkono wa adui zao wote.”
19 阿貝乃爾也遊說了本雅明人;以後阿貝乃爾去赫貝龍見達味,向他報告以色列和本雅明全家共同贊成的事。
Pia Abneri akasema na watu wa Benjamini ana kwa ana. Kisha Abneri akaenda kuongea na Daudi huko Hebroni akaeleza kila jambo ambalo Israeli na nyumba yote ya Benjamini walitamani kulitimiza.
20 阿貝乃爾遂率領二十人去赫貝龍見達味。達味設宴款待了阿貝乃爾和他的隨員。
Wakati Abneri na watu ishirini kati ya watu wake walifika Hebroni kumuona Daudi, Daudi akaandaa sherehe kwa ajili yao.
21 阿貝乃爾向達味說:「我要動身去號召全以色列,來擁護我主大王,使他們與你立約:這樣你能依照你的心願來統治一切。」事後,達味放阿貝乃爾平安走了。
Abneri akamweleza Daudi, “Nitainuka na kukukusanyia Israeli wote, bwana wangu mfalme, ili kwamba wafanye agano nawe, kwamba utawale juu ya yote unayotaka.” Hivyo Daudi akamruhusu Abneri kuondoka, Abneri akaondoka kwa amani.
22 達味的臣僕和約阿布出征回來,帶回了很多戰利品。那時,阿貝乃爾已不在赫貝龍達味那裏了,因為達味放他平安走了。
Kisha askari wa Daudi na Yoabu wakarudi kutoka katika kuteka nyara na wakaja na nyara nyingi. Lakini Abneri hakuwepo Hebroni pamoja na Daudi. Daudi alikuwa amemruhusu kuondoka, na alikuwa ameondoka kwa amani.
23 約阿布和他率領的軍隊一來到,就有人告訴他說:「乃爾的兒子阿貝乃爾曾來到君王前,君王放他平安走了。」
Wakati Yoabu na Jeshi lote walipofika, Yoabu aliambiwa, “Abneri mwana wa Neri alikuja kwa mfalme, na mfalme amemruhusu kuondoka, naye Abneri ameondoka kwa amani.”
24 約阿布就去見君王說:「你作的是什麼事﹖阿貝乃爾到你這裏來,你為什麼放他平安走了﹖
Kisha Yoabu akaja kwa mfalme na kusema, “Umefanya nini? Tazama, Abneri alikuja kwako! Kwa nini umemruhusu kuondoka, naye amenda?
25 你豈不認識乃爾的兒子阿貝乃爾﹖他來是為欺騙你,願探聽你的出入,知道你的一切行動。」
Haujui kwamba Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kupeleleza hali yako na kuangalia kila unalofanya?”
26 約阿布離開達味就打發差役去追趕阿貝乃爾。他們從息辣的旱井旁,把他帶回來,。達味一點也不知道。
Yoabu alipoondoka kwa Daudi, alituma wajumbe kumfuatia Abneri, nao wakamrudisha kutoka katika kisima cha Sirah, lakini Daudi hakulijua hili.
27 阿貝乃爾一回到赫貝龍,約阿布就領他到大門旁,彷彿要與他暗地交談,就在那裏一刀剌穿了他的肚腹,他立即死了;這樣替他兄弟阿撒耳報了血仇。
Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kati ya lango ili aongee naye faraghani. Hapohapo Yoabu alimchoka tumboni na kumuua. Hivyo, akalipa kisasi cha damu ya Asaheli nduguye.
28 事後,達味一聽說這事,就說:「我和我的國家,對乃爾的兒子阿貝乃爾的血案,在上主面前,永遠是無罪的!
Daudi alipolisikia jambo hili akasema, “Mimi na ufalme wangu hatuna hatia mbele za Yahwe daima, kuhusiana na damu ya Abneri mwana wa Neri.
29 願這罪歸在約阿布的頭上和他父的全家! 願約阿布家中不斷有患淋症,長癩病,只會紡線,喪身刀下和缺糧的人! 」
Hatia ya damu ya Abneri na iwe juu ya Yoabu na nyumba yote ya baba yake. Na asikosekane katika familia ya Yoabu mtu mwenye vidonda, au mwenye ukoma, au kirema atembeaye kwa fimbo au aliyeuawa kwa upanga au mwenye kukosa chakula.”
30 約阿布和他的兄弟阿彼瑟暗殺了阿貝乃爾,是因為他在基貝紅打仗時,殺死了他們的兄弟阿撒耳。
Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamwua Abneri, kwa sababu alimwua Asaheli ndugu yao vitani huko Gibeoni.
31 達味向約阿布和同他在一起的民眾說:「要撕裂你們的衣服,穿上喪服,為阿貝乃爾舉哀! 」達味王也跟在靈柩後送葬。
Daudi akamwambia Yoabu na wote waliokuwa pamoja naye, “Rarueni mavazi yenu, jivikeni nguo za magunia, na muomboleze mbele ya mwili wa Abneri.” Na mfalme Daudi akaufuata mwili wa Abneri wakati wa mazishi.
32 他們在赫貝龍埋葬了阿貝乃爾;君王在阿貝乃爾墓旁放聲大哭,民眾也都哭了。
Wakamzika Abneri huko Hebroni. Mfalme akalia kwa sauti katika kaburi la Abneri, na watu wote pia wakalia.
33 君王作哀歌弔阿貝乃爾說:「阿貝乃爾豈應像傻瓜一樣死去﹖
Mfalme akamwombolea Abneri naye akaimbo, “Je ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu?
34 你的手並未束拷,你的腳也沒帶鐐,怎麼你斃命,竟如兇犯斃命一樣! 」為此民眾更加痛哭。
Mikono yako haikufungwa. Miguu yako hakuwa imefungwa minyororo. Kama mtu aangukavyo mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.” Watu wote wakamlilia zaidi.
35 隨後,眾人前來勸君王進食,那時還是白天,達味卻發誓說:「若我在日落前進食,或嘗什麼東西,願天主如此,並加倍地懲罰我!」
Watu wote wakaja kumtaka Daudi ale wakati kungali mchana, lakini Daudi akaapa, “Mungu na anifanyie hivyo, na kuzidi, ikiwa nitaonja mkate au chochote kabla jua halijazama.”
36 眾人見到此事,都心悅誠服,因為凡君王所行的,無不叫眾人心悅誠服。
Watu wote wakaiona huzuni ya Daudi, na ikawapendeza, hivyo kila alichokifanya mfalme kikawapendeza.
37 如此,眾人和全以色列當天都知道,殺乃爾的兒子阿貝乃爾,不是出於君王的命令。
Hivyo watu wote na Israeli wote wakatambua siku hiyo kwamba haikuwa nia ya mfalme Abneri mwana wa Neri afe.
38 達味向他的臣僕說:「你們不知道今天在以色列喪失了一位將領和偉人嗎﹖
Mfalme akawaambia watumishi wake, “je hamjui kuwa mtu mkuu ameanguka leo hii katika Israeli?
39 我今天雖是傅油的君王,仍年幼無力,責魯雅的兒子們又比我剛強;願上主依照人所行的邪惡,來施行報復! 」
Nami leo nimedhoofika, japokuwa nimetiwa mafuta kuwa mfalme. Watu hawa, wana wa Seruya ni hatari sana kwangu. Yahwe na amrudishie mwovu kwa kumlipa kwa ajili ya uovu wake kama anavyostahili.