< 列王紀下 23 >
1 君王於是派人召集猶大和耶路撒冷所有的長老來到他跟前。
Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.
2 君王同所有的猶大人、耶路撒冷的居民、眾司祭、眾先知、全體人民,不分貴賤大小,上了上主聖殿,將在上主殿內尋獲的約書上的一切話,讀給他們聽。
Akapanda kwenda hekaluni mwa Bwana pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu la Bwana.
3 君王站在高台上,在上主面前立約,要全心全意跟隨上主,遵守祂的誡命、典章和法律,履行這卷書上所記載的盟約的話;全體人民也一致接受了這盟約。
Mfalme akasimama karibu na nguzo, na kufanya upya agano mbele za Bwana: yaani kumfuata Bwana na kuzishika amri zake, maagizo na sheria kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, hivyo kuyathibitisha maneno ya agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Kisha watu wote wakajifunga wenyewe kwa kiapo katika agano.
4 君王於是吩咐大司祭希耳克雅和副大司祭以及守門的,將那些為巴耳,為阿舍辣和為天上萬象所製造的祭器,都從上主殿內搬出,在耶路撒冷外克德龍谷的田野中焚燒了,把灰燼帶到貝特耳去。
Mfalme akamwamuru Hilkia kuhani mkuu, makuhani waliomfuata kwa cheo, na mabawabu kuondoa kutoka kwenye Hekalu la Bwana vyombo vyote vilivyofanywa kwa ajili ya Baali na Ashera na jeshi lote la mianga ya angani! Akavichoma nje ya Yerusalemu katika mashamba ya Bonde la Kidroni, na kuyachukua hayo majivu mpaka Betheli.
5 君王廢除了以前猶大王派定在猶大各城,和耶路撒冷周圍高丘上的焚香的僧侶,以及向巴耳、太陽、月亮和黃道帶,並天上萬象焚香的人;
Akawafukuza makuhani wa kipagani waliokuwa wameteuliwa na wafalme wa Yuda kufukiza uvumba katika mahali pa juu pa kuabudia miungu katika miji ya Yuda na ile iliyozunguka Yerusalemu, yaani wale waliofukiza uvumba kwa Baali, kwa jua na mwezi, kwa makundi ya nyota, na jeshi lote la angani.
6 又將木偶從上主的殿內搬到耶路撒冷城外克德龍谷,在克德龍谷焚燒了,磨碎成灰,將灰撒在平民的墳墓上;
Akaiondoa nguzo ya Ashera kutoka kwenye Hekalu la Bwana, na kuipeleka kwenye Bonde la Kidroni nje ya Yerusalemu, akaiteketeza huko. Akaisaga hadi ikawa unga na kusambaza hilo vumbi juu ya makaburi ya watu wa kawaida.
7 拆毀了上主殿內廟倡的房舍,婦女們為木偶編織衣服的地方。
Akabomoa pia nyumba za mahanithi wa mahali pa ibada za miungu, zilizokuwa ndani ya Hekalu la Bwana na mahali wanawake walipofuma kwa ajili ya Ashera.
8 又從猶大各城將所有的司祭召來,破壞了司祭們焚香的高丘,從革巴直到貝爾舍巴;拆毀了城門左邊,市長約叔亞門前的羊神祭壇。
Yosia akawaleta makuhani wote wa Bwana kutoka miji yote ya Yuda, na kunajisi mahali pa juu pa kuabudia miungu, kuanzia Geba hadi Beer-Sheba, mahali pote ambapo hao makuhani wa miungu walifukiza uvumba. Akabomoa mahali pa kuwekea vitu vya ibada za miungu palipokuwa katika malango, kwenye ingilio la Lango la Yoshua, mtawala wa mji, lililoko upande wa kushoto wa lango la mji.
9 無論如何,高丘的司祭,不能上耶路撒冷上主的祭壇,只能在自己的兄弟中間分食無酵餅。
Ingawa makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu hawakuhudumu katika madhabahu ya Bwana katika Yerusalemu, walikula mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao.
10 約史雅又破壞了本希農山谷中的托斐特,免得再有人火祭子女,獻給摩肋客。
Kisha mfalme akanajisi Tofethi, palipokuwa katika Bonde la Ben-Hinomu, ili mtu yeyote asiweze kupatumia kumtoa kafara mwanawe au binti yake katika moto kwa mungu Moleki.
11 又將以前猶大王在上主聖殿門前,靠近太監乃堂默肋客住宅的廊房裏,獻於太陽的駿馬除去;也用火燒掉了奉獻給太陽的車輛。
Akaondoa kutoka kwenye ingilio la Hekalu la Bwana wale farasi ambao wafalme wa Yuda walikuwa wamewaweka wakfu kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye ua karibu na chumba cha afisa aliyeitwa Nathan-Meleki. Basi Yosia akayachoma moto yale magari yaliyokuwa yamewekwa wakfu kwa jua.
12 猶大王在阿哈次的樓房頂上所建築的祭壇,和默納舍在上主聖殿兩庭院內建築的祭壇,君王也都拆掉搗毀,把碎塊倒在克德龍谷裏。
Alizivunja madhabahu ambazo wafalme wa Yuda walikuwa wamezijenga kwenye paa la ghorofa ya Ahazi, pia madhabahu alizokuwa amezijenga Manase katika nyua mbili za Hekalu la Bwana. Akaziondoa huko, akazivunja vipande vipande, na kutupa hicho kifusi katika Bonde la Kidroni.
13 從前以色列王撒羅滿在耶路撒冷東,橄欖山南,為漆東人的可惡之物阿市托勒特,為摩阿布的可惡之物革摩士,為阿孟子民的可惡之物米耳公所建立的高丘,君王一概破壞了;
Mfalme pia akanajisi mahali pa juu pa kuabudia miungu, palipokuwa mashariki ya Yerusalemu upande wa kusini wa Kilima cha Uharibifu, pale ambapo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amejenga kwa ajili ya Ashtorethi mungu mke chukizo la Wasidoni, kwa ajili ya Kemoshi mungu chukizo la Wamoabu, na kwa ajili ya Moleki mungu chukizo la watu wa Amoni.
14 又打碎了石柱,砍斷了木偶,用人骨填滿了那些地方。
Yosia akapasua yale mawe ya kuabudiwa na kuzikatakata nguzo za Ashera. Kisha akafunika hayo maeneo kwa mifupa ya wanadamu.
15 此外,那使以色列陷於罪惡的乃巴特的兒子雅洛貝罕,在貝特耳所立的祭壇和高丘,約史雅也將這祭壇拆毀,將丘壇的石塊打碎成灰,燒了木偶。
Hata madhabahu yaliyokuwa huko Betheli, mahali pa juu pa kuabudia miungu palipokuwa pamejengwa na Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye aliwafanya Israeli watende dhambi, alibomoa hata hayo madhabahu na mahali pa juu pa kuabudia miungu. Alipateketeza kwa moto hapo mahali pa juu pa kuabudia miungu na kupasaga hadi pakawa vumbi, na kuichoma hiyo nguzo ya Ashera pia.
16 約史雅轉身,看見山上墳墓,就派人掘出墳裏的骨骸,放在祭壇上焚燒,污辱了這祭壇,應驗了天主的人,當雅洛貝罕在慶節日站在這祭壇上時,所說的的話。約史雅再戔身遙望,看見曾預言這些事的天主的人的墳墓,
Kisha Yosia akatazama huku na huko, naye alipoona makaburi yaliyokuwa huko kwenye kilima, akaamuru mifupa itolewe humo na akaichoma juu ya madhabahu ya Betheli ili kupanajisi. Hili lilitokea kulingana na neno la Bwana lililosemwa na mtu wa Mungu ambaye alitangulia kusema mambo haya.
17 就問說:「看見的是誰的墓碑﹖」城中的人回答說:「是天主的人的墳墓,他從猶大來,預言了你剛才對貝特耳祭壇所行的事」。
Mfalme akauliza, “Lile kaburi lenye mnara wa ukumbusho ninaloliona ni kwa ajili gani?” Watu wa mji wakasema, “Hii ni alama ya kaburi la mtu wa Mungu aliyekuja kutoka Yuda, naye akanena dhidi ya hii madhabahu ya Betheli mambo yale yale uliyoifanyia leo.”
18 君王遂說:「讓他安息吧! 誰也不要移動他的骨骸! 」因此人沒有移動他的骨骸,也沒有移動那撒瑪黎雅先知的骨骸。
Akasema, “Liacheni, msiliguse. Msimruhusu mtu yeyote kuiondoa mifupa yake.” Basi wakaiacha mifupa yake pamoja na ile ya yule nabii ambaye alikuwa amekuja kutoka Samaria.
19 從前以色列王在e口城內所建築,而激怒上主的高丘廟宇,約史雅也一律除去,對這些廟宇所行的,完全像在貝特耳所行一樣。
Kama alivyokuwa amefanya huko Betheli, Yosia akabomoa na kunajisi mahali pa kuabudia miungu kwenye mahali pa juu ambapo wafalme wa Israeli walikuwa wamejenga ndani ya miji ya Samaria, ambayo ilikuwa imemghadhibisha Bwana.
20 凡在那裏所有的高丘司祭,他都在祭壇上殺了,並且在祭壇焚燒了人骨,然後回了耶路撒冷。
Yosia akawachinja makuhani wote wa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika madhabahu zao wenyewe, na kuchoma mifupa ya wanadamu juu yake. Kisha akarudi Yerusalemu.
21 君王吩咐全體人民說:「你們要按照這約書所記載的,向上主你們的天主舉行逾越節」。
Mfalme akatoa agizo hili kwa watu wote: “Adhimisheni Pasaka kwa Bwana Mungu wenu, kama ilivyoandikwa katika Kitabu hiki cha Agano.”
22 實在,自從民長統治以色列時日以來,和在以色列各君王及猶大王當政期間,從來沒有舉行過像這樣的一個逾越節,
Hapakuwahi kuwepo na adhimisho lingine la Pasaka kama hilo tangu nyakati za Waamuzi walioongoza Israeli, wala katika nyakati zote za wafalme wa Israeli na wafalme wa Yuda.
23 只有在約史雅王十八年,在耶路撒冷向上主舉行了這樣的逾越節。
Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Yosia, Pasaka hii iliadhimishwa kwa Bwana huko Yerusalemu.
24 此外,凡在猶大地和耶路撒冷所見到的那些招魂的,行邪術的,忒辣芬和偶像,以及可憎之物,約史雅一概掃除,履行了司祭希耳克雅在上主殿內,所發見的書上所記載的法律。
Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa waaguzi, wanaoabudu mizimu, sanamu za kuagulia, sanamu za kuabudiwa, na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana huko Yuda na Yerusalemu. Aliyafanya haya ili kutimiza matakwa ya sheria iliyoandikwa ndani ya kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikipata ndani ya Hekalu la Bwana.
25 在他以前沒有人一個君王像他這樣按照梅瑟的法律,全心全意全力歸向上主;在他以後也沒有一個像他一樣的。
Kabla wala baada ya Mfalme Yosia hapakuwepo na mfalme mwingine yeyote ambaye alimpenda Bwana kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Sheria yote ya Mose.
26 雖然如此,上主仍未息向猶大所發的盛怒烈火,因為默納舍種種行事,太激怒了上主,
Hata hivyo, Bwana hakuacha ghadhabu yake iliyowaka dhidi ya Yuda kwa sababu ya yale yote ambayo Manase alikuwa amefanya kumghadhibisha.
27 因此上主說:「我仍要由我面前除去猶大,如同我除去了以色列一樣;我要拋棄我所選擇的這座耶路撒冷城,和我所說我名必留其間的殿」。
Hivyo Bwana akasema, “Nitamwondoa Yuda mbele zangu kama nilivyomwondoa Israeli, nami nitaukataa Yerusalemu, mji niliouchagua, na Hekalu hili, ambalo nilisema, ‘Jina langu litakaa humo.’”
28 約史雅其餘的事蹟,他的一切作為,都記載在猶大王實錄上。
Matukio mengine ya utawala wa Yosia na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda?
29 約史雅年間,埃及王法郎乃苛上到幼發拉的河,亞述王那裏,約史雅出兵與他對抗,初次會戰,就在默基多陣亡。
Yosia alipokuwa mfalme, Farao Neko mfalme wa Misri akapanda mpaka Mto Frati kumsaidia mfalme wa Ashuru. Mfalme Yosia akatoka kwenda kupigana naye, lakini Neko akamkabili na kumuua huko Megido.
30 他的臣僕將他的屍體,用車從默基多運到耶路撒冷,葬在他自己的墳墓裏;當地的人民推舉約史雅的兒子約哈次,給他傅油,繼承父位為王。
Watumishi wa Yosia wakauleta mwili wake katika gari la vita kutoka Megido hadi Yerusalemu, wakamzika kwenye kaburi lake mwenyewe. Nao watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta na kumfanya mfalme mahali pa baba yake.
31 約哈次登極時年二十三歲,在耶路撒冷為王三個月,他的母親名叫哈慕塔耳,是里貝納人耶勒米雅的女兒。
Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miezi mitatu. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia kutoka Libna.
32 他行上主視為惡的事,完全像他祖先所行的一樣。
Akafanya maovu machoni mwa Bwana, kama baba zake walivyofanya.
33 法郎乃苛將他幽禁在哈瑪特的黎貝拉,不要他在耶路撒冷作王,並要那地方繳約一百「塔冷通」銀子和十「塔冷通」金子作賠款。
Farao Neko akamfunga kwa minyororo huko Ribla katika nchi ya Hamathi ili asiweze kutawala huko Yerusalemu, naye akatoza kodi ya talanta mia moja za fedha, na talanta moja ya dhahabu katika Yuda.
34 以後,法郎乃苛立了約史雅的兒子厄里雅金繼他父親約史雅為王,給他改名叫約雅金;後將約哈次帶到埃及去了,約哈次就死在那裏。
Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia kuwa mfalme mahali pa baba yake Yosia, na kulibadilisha jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua Yehoahazi na kumpeleka Misri, naye akafia huko.
35 約雅金將金銀付給法郎,但為交付的求要賠款,只得國家徵稅,要本國人民每人依照自己的家業,繳納金銀,送給法欴乃苛。
Yehoyakimu akamlipa Farao Neko ile fedha na dhahabu aliyodai. Ili kuweza kufanya hivyo, Yehoyakimu akatoza nchi kodi na kulipiza fedha na dhahabu kutoka kwa watu wa nchi kulingana na makadrio ya mapato yao.
36 約雅金登極時年二十五歲,在耶路撒冷為王十一年;他的母親名叫則步達,是魯瑪人培達雅的女兒。
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Zebida binti Pedaya kutoka Ruma.
37 他行了上主視為惡的事,全像他祖先所行的一樣。
Naye akafanya maovu machoni mwa Bwana, kama baba zake walivyokuwa wamefanya.