< 歷代志下 32 >

1 [亞述來犯]這些忠貞之事作完之後,亞述王散乃黑黎布來進攻猶大,包圍一切堅城,企圖攻破,佔為己有。
Baada ya mambo haya na matendo haya ya uaminifu, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja na kuingia Yuda. Alipiga kambi kwa ajili ya kuivamia miji yenye ngome, ambayo alikusudia kuiteka kwa ajili yake.
2 希則克雅見散乃黑黎市前來,決意要進攻耶路撒冷,
Sedekia alipoona kwamba Senakeribu amekuja na kwamba amedhamiria kupigana zidi ya Yerusalemu,
3 便與自己的將領和勇士商議,將城外的水泉杜塞;他們都贊成;
aliwashirikisha viongozi wake na watu wake wenye nguvu kuyazuia maji ya chemichemi yaliyokuwa nje ya mji; waalimsaidia kufanya hivyo.
4 於是召集許多人,將水泉和通過田間的水渠都杜塞,說:「為什麼讓亞述王來,得到這樣多的水! 」
Kwa hiyo watu wengi wakakusanyika na kuyazuia maji ya chemichemi zote na mikondo yote amabayo ilikuwa inatiririka katikati ya nchi. wakasema, “Kwa nini mfalme wa Ashuru aje na kupata maji mengi?”
5 希則克雅遂加強防禦工事,重修所有破裂的城牆,上面建上城樓,城外又築了一道牆,加強達味城的米羅,製造了許多箭矢和盾牌。
Hezekia akijipa ujasiri na kuujeenga ukuta wote uliokuwa umeangushwa chini. Akaijenga minara mirefu, na pia ukuta mwingine nje. Pia akaiimarisha Milo katika mji wa Dudi, na akafanya kiasi kikubwa cha silaha na ngao. (Maanshi ya kale yanasema hivi: “Badala ya, “akajenga minara amirefu”, baadhi ya matoleo ya zamani na kisasa yanasema, “akajenga minara mirefu juu yake”, Hii ni juu ya ukuta).
6 然後派了將官率領軍民,將他們集合到城門廣場他自己面前,鼓勵他們說:「
Akaweka maamri jeshi juu wa watu. Akawakusanya pamoja kwake katika sehemu pana kwenye lango la mji na akasema kwao kwa ujasiri. Akasema,
7 你們應該勇敢大膽,不要害怕,不要因亞述王和他所統領的大軍而膽怯,因為那與我們同在的比與他同在的,更有能力。
“Muwe imara na wenye ujasiri mzuri. Msiogope wala kukata tamaa kwa sababu ya mfalme wa Ashuru na jeshi lote ambalo liko naye, kwa maana kuna mtu yuko pamoja nasi ambaye ni mkuu kuliko
8 那與他同在的只是血肉的手臂,那與我們同在的卻是天主,我們的天主,他必要協助我們,為我們作戰。」眾人都因猶大王希則克雅這番話而得到鼓勵。[亞述王的侮辱]
walio naye mfalme wa Ashuru. walionaye ni jeshi la mwili tu, lakini aliye nasi ni Yahwe, Mungu wetu, kwa ajili ya kutusaidia, na kupiagana vita vyetu.” Kisha watu wakajifariji wenyewe kwa maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.
9 此後,亞述王散乃黑黎布派自己的臣僕到耶路撒冷來,─他本人偕全軍駐在拉基士─向猶大王希則克雅,和在耶路撒冷所有的猶大人說:「
Baada ya hayo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, aliwatuma watumishi wake kwenda Yetusalemu (sasa alikuwa mbe ya Lakishi, na jeshi lake lote lilikuwa pamoja naye), kwa Hezekia, mfaalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walikuwa Yerusalemu. Akasema,
10 亞述王散乃黑黎布這樣說:你們在耶路撒冷受困,還依靠什麼呢﹖
“Hivi ndivyo Senakeribu, mfalme wa Ashuru, anasema: Ni kitu gani mnategemea kwa ajili ya kuhimili uvamizi katika Yerusalemu?
11 希則克雅曾對你們說過:雅威我們的天主必要救我們脫離亞述王的手,這豈不是誘惑你們,使你們餓死渴死嗎﹖
Je, Hezekia hawapotoshi ninyi, ili kwamba awatoe kufa kwa njaa na kiu, anapowaambia, “Yahwe Mungu wetu atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru?
12 希則克雅豈不是將高丘和鄉壇推翻,且吩咐猶大和耶路撒冷人說:你們應在一個壇前朝拜,單在這上面焚香嗎﹖
Je, siyo Hezekia yule yule ambaye amezipeleka juu sehemu zake na madhabahu zake na kuwaamuru Yuda na Yerusalemu, juu ya madhabahu moja lazima muabudu, na juu yake lazima mchome sadaka zenu?
13 難道你們不知道我與我的祖先,對各列邦民所作的事嗎﹖列邦各地的神,是否曾能拯救自己的國土,脫離我的手﹖
Je, hamjui mimi na babu zangu tulifanya nini kwa makundi ya wote wa inchi zingine? Je, miungu ya watu wa hizo nchi iliweza kwa njia yoyote kuziokoa nchi zao zidi ya nguvu zangu?
14 我祖先所消滅的那些邦國的諸神中,有那一個曾能夠拯救自己的百姓,脫離我的手﹖難道你們的神就能拯救你們脫離我的手嗎﹖
Miongoni mwa miungu yote ya mataifa hayo amabayo babu zangu waliwatekeza, je, kulikuwa na muungu yeyote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu? Itakuwaje Mungu wenu aweze kuwakoa ninyi zidi ya nguvu zangu?
15 所以現在,不要讓希則克雅這樣欺騙你們,迷惑你們;你們也不要相信他,因為任何一個國家,一個民族的神,都不能拯救自己的百姓,脫離我的手,和我祖先的手;何況你們的神﹖他更不能拯救你們脫離我的手! 」
Sasa msimuruhusu Hezekia awadanganye au kuwashawishi katika njia hii. Msimwamini, kwa maana hakuna muungu wa taifa lolote au ufalme amewahi kuwaokoa watu wake nje ya mkono wangu, au nje ya mkono wa babu zangu. Sembuse na Mungu wenu kwa namna gani atawaokoa na mkono wangu?
16 散乃黑黎布的臣僕,還說了許多譭謗上主天主,和他僕人希則克雅的話。
Watumishi wa Senakeribu hata walinena mabaya zaidi juu ya Yahwe Mungu na juu ya mtumishi wake Hezekia.
17 散乃黑黎布也寫信嘲笑上主以色列的天主,侮辱他說:「就如列邦民族的神沒有拯救自己的百姓脫離我的手,同樣希則克雅的神也不能救自己的百姓脫離我的手。」
Senakeribu pia akandika barua ili kumdhihaki Yahwe, Mungu wa Israeli, na kunena kinyume naye. Alisema, “Kama ambavyo miungu ya mataifa haikuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu, hivyo hivyo na Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu.”
18 隨後,他們用猶大方言向耶路撒冷城牆上的軍民呼喊,想驚嚇他們,令他們恐懼,以便奪取京城。
Wakawalilia kwa lugha ya Wayahudi watu wa Yerusalemu waliokuwa juu ya ukuta, ili kuwaogopesha na kuwasumbua, ili kwamba waweze kuuteka mji.
19 他們論及耶路撒冷的天主,好似論及列邦民族的神一樣,當作了人手的造物。[希則克雅祈禱獲允]
Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu kama walivyowanenea miungu wa Dunia, ambao ni kazi ya mikono ya wanadamu tu.
20 希則克雅王與阿摩茲的兒子依撒意亞先知為此巷天祈求呼籲。
Hezekia, mfalme, na Isaya mwana wa Amozi, nabii, wakaomba kwa sababu ya jambo hili na wakalia hadi mbinguni.
21 上主便派一位天使進入亞述王的營爭,將所有的兵士、將軍和統帥,予以殲滅,使亞述王含羞回了本國。當他進入自己的神廟時,為他親生的兒子用劍所殺。
Yahwe akatuma malaika, ambaye aliwaua wanaume wa kupigana vita, majemedari, na maakida wa mfalme katika kambi. Kwa hiyo Senakeribu akarudi katika nchi yake akiwa na uso wa aibu. Alipokuwa ameenda katika nyumba ya muungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua huko kwa upanga.
22 這樣,上主救了希則克雅和耶路撒冷的居民,脫離了亞述王散乃黑黎布和所有敵人的手,使他們四境獲得了安寧。
Katika namna hii, Yahwe akamwokoa Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka kwenye mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na kutoka kwenye mikono ya wengine, na akawapa pumzika juu ya kila upande. (Maandishi ya kale yanasema hivi: badala ya “akawapa pumziko juu ya kila pande”, baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasema, “akawaongoza juu ya kila pande”).
23 眾人就都到耶路撒冷向上主獻上禮品也贈予猶大王希則克雅禮物;從此以後,希則克雅乃為個國所敬重。
Wengi walikuwa wakileta sadaka kwa Yahwe katika Yarusalemu, na zawadi za thamani kwa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa hiyo aliinuliwa mbele za macho ya mataifa yote toka wakati huo na kuendelea.
24 那時,希則克雅害病要死,他哀求了上主,上主便應允了他,給了他一個異兆。
Katika siku hizo Hezekia akaugua hadi hatua ya kufa. Akaomba kwa Yahwe, ambaye alisema kwake na kumpa ishara kwamba angeponywa.
25 但是,希則克雅不但沒有照他所受的恩惠還報,反而心高氣傲,於是上主的怒火降於他和猶大並耶路撒冷。
Lakini Hezekia hakumlipa Yahwe kwa ajili ya msaada uliotolewa kwake, kwa maana moyo wake uliinuliwa juu.
26 以後,希則克雅抑制了自己的驕傲,他和耶路撒冷居民都自謙自卑,因此上主的怒氣,在希則克雅生時,沒有向他們發作。[希則克雅一生概略]
Kwa hiyo hasira ikaja juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu. Hata hivyo, baadaye Hezekia alijinyenyekesha mwenyewe kwa jali ya kiburi cha moyo wake, wote Yeye na wakaaji wa Yerusalemu, hivyo hasira ya Yahwe haikuja juu yao wakati wa siku za Hezekia.
27 希則克雅享盡富貴榮華,建造了府庫,儲藏金銀、寶石、香料、盾牌和各種珍器;
Hezekia alikuwa na utajiri mwingi sana na heshima kubwa. Alijipatia mwenyewe vyumba vya kuhifadhia kwa ajili ya fedha, dhahabu, vito vya thamani, na kwa ajili ya manukato, na kwa ajili ya ngao na na vyombo vyote vya thamani pia.
28 修建了倉廩,儲藏五穀、新酒和油;修蓋了棚欄,為養各類牲畜;為羊群修了羊棧;
Pia alikuwa na nyumba za maghala kwa ajili ya mavuno ya nafaka, divai mpya, na mafuta, na malisho kwa ajili ya aina zote za wanyama.
29 又畜養了驢,以及許多大小牲畜;天主實在賜給了他極多的財物。
Pia alikuwa na makundi katika mazizi. Zaidi ya hayo, alijipatia mwenyewe miji na makundi ya na ng'ombe kwa wingi, kwa maana Mungu alaikuwa amempa afya tele. (Maandishi ya kale yanasema hivi: Badala ya “miji” baadji ya matoleo ya kisasa yanasema “punda”, na baadhi mengine ya kisasa yanaacaha neno nzima)
30 希則克雅堵住基紅泉上邊的水,將水直引到達味城西。希則克雅所作所為無不順利。
Alikuwa ni Hezekia huyu huyu ambaye alisimamisha chemi chemi ya juu ya maji ya Gihoni, na aliye ileta moja kwa moja chini upande wa magharibi mwa mji wa Daudi. Hezekia alifanikiwa katika miradi yake yote.
31 甚至巴比倫王公大人派使者來見希則克雅,詢問他國內發生的奇事時,天主也讓他自由,藉以考驗他,好知道他心中的一切。
Hata hivyo, katika jambo la mabolozi wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuwauliza waliofahamu, kuhusu ishara za miujiza iliyokuwa imefanywa katika nchi, Mungu alimwachia mwenyewe, ili kumjaribu, na kujua yote yaliyokuwa katika moyo wake.
32 希則克雅其餘的事蹟,以及他的善行,都記載在阿摩茲的兒子依撒意亞先知的神視錄及猶大和以色列列王實錄上。
Kwa mambo mengine kuhusu Hezekia, pamoja na matendo yake ya uaminifu wa agano, unaweza kuona kwamba yameandikwa katika Maono ya Nabii Isaya Mwana wa Amozi, na katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.
33 希則克雅與他的祖先同眠,葬在達味子孫墓地的斜坡上;他死了,全猶大和耶路撒冷居民都為他舉哀致敬;他的兒子默納舍繼位為王。
Hezekia akalala pamaoja na babu zake, na wakamzika katika mlima wa makaburi ya vizazi vya Daudi. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakamheshimu katika kifo chake. Manase mwanaye akawa mfalme katika nafasi yake.

< 歷代志下 32 >